Articles by "AJALI"
Showing posts with label AJALI. Show all posts
Benki ya CRDB kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii, Aprili 24 - 25, 2024 ilikabidhi madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Kikilo na madarasa mengine mawili katika Shule ya Msingi Isabe zote za wilayani Kondoa, mkoa wa Dodoma yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki hiyo.

Hafla ya kukabidhi madarasa hayo, iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi ambaye aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa pamoja na Maafisa Elimu Sekondari na Msingi.

Katika hafla zote mbili Dkt. Khamis Mkanachi ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali maombi ya ujenzi wa madarasa katika Wilaya ya Kondoa, ambayo yapo katika vijiji vya Kikilo na Bukulu. Huku akitoa rai kwa wanafunzi kusoma kwa bidii kwani mazingira ya shule yanaendelea kuboreshwa.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa, Mashauri Vicent aliyekabidhiwa madarasa hayo ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya elimu pia kuahidi kuwa watahakikisha madarasa hayo yanakuwa ni sehemu ya kuchagiza ongezeko la wanufaika ambayo ni watoto kwenye jamii ya Kondoa.

Kwa upande wa Benki ya CRDB, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay aliyeongozana na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji kwa Jamii pamoja na Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati, amesema kuwa Benki ya CRDB imeweka sera ya uwekezaji kwa jamii inayolenga kuchangia maendeleo mbalimbali katika jamii hasa katika swala la Elimu, Mazingira, Afya, Vijana na Wanawake. Aidha, ametoa rai kwa wazazi wa shule hizo kuendelea kushirikiana kwa karibu na uongozi wa shule katika kuboresha miundombinu ya shule.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt, Ally Laay wakiwa pamoja na viongozi wengine pamoja na Wanafunzi katika moja ya madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB yenye thamani ya shilingi Milioni 40 katika Shule ya Msingi Isabe, iliyopo katika kijiji cha Bukuru, Wilayani Kondoa, katika hafla  iliyofanyika Aprili 25, 202.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi (wanne kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt, Ally Laay muda mfupi baada ya kukaidhi madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB yenye thamani ya shilingi Milioni 40 kwa uongozi wa Halmashauri ya Kondoa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt, Ally Laay (katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wa Benki ya CRDB pamoja na wa Halmashauri ya Kondoa wakiwa katika picha ya paamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikilo, muda mfupi baada ya kukaidhi madarasa mawili katika shule hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Khamis Mkanachi akizungumza wakati wa hafla kukaidhi madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB yenye thamani ya shilingi Milioni 40 kwa uongozi wa Halmashauri ya Kondoa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt, Ally Laay akizungumza wakati wa hafla kukaidhi madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB yenye thamani ya shilingi Milioni 40 kwa uongozi wa Halmashauri ya Kondoa.












Mmoja wa watumishi wa NSSF Mkoa wa Tanga ambaye alipata majeruhi akibebwa kwa ajili ya kuwahishwa katika Hospitali leo
huo Kaimu Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga,Mrakibu wa Jeshi hilo Abrahaman Ntezidyo akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga akiteta jambo na baadhi ya wateja wa mfuko huo mara baada ya kutokea tukio hilo
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga kushoto akimsikiliza kwa umakini Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga Abrahaman Ntezidyo
Na Oscar Assenga,TANGA.

TAHARUKI kubwa imeibuka kwa wateja na watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani Tanga baada ya kuibuka kwa moto kwenye moja ya chumba kilichopo kwenye Jengo lao na hivyo kulazimika kuacha shughuli na kukusanyika eneo moja huku Jeshi la Zimamoto na Ukoaji likifika na kufanikiwa kuzima moto huo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uzimaji wa moto huo Kaimu Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga,Mrakibu wa Jeshi hilo Abrhaman Ntezidyo alitibitisha kutokea kwa moto huo ambapo alisema ulitokea saa 4.4o asubuhi.

Alisema kwamba walipataa taarifa za uwepo wa moto huo ambao ulianza saa nne na dakika arobaini asubuhi baada ya kupokea taarifa ya wito kutoka Jengo la NSSF kuwepo kwa moto kwenye jengo ambao ulitokea kwenye moja ya chumba cha ofisi.

Alisema kwamba katika jengo hilo kilikuwa na vitu kadhaa ikiwemo thamani za ofisi na waliopata hizo walipofika eneo la tukio kutokana na uwepo wa purukushani kutokana na taharuki hiyo mmoja wa watumishi wa mfuko huo alipata majeruhi kutokana na kupata mshutuko na alipelekwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo alisema kwamba chanzo chaa tukio hilo bado hakijafahamika lakini kwa sasa wanaendelea kufanyaa uchunguzi ili kuweza kubaini sabaabu zilizopelekea kutokea kwa moto huo katika moja ya chumba kwenye jengo hilo.

“Tunamshukuru Meneja wa NSSF kwa kutoa taarifa kwa wakati kwa Jeshi letu na tukio hilo kutokana na kuwahi kufika hakuna madhara makubwa kilichohusika ni chumba kimoja cha ofisi ambacho kimeungua vitu vichache kutokana na kuwahi kuzibiti moto usisambae maeneo mengine”Alisema

Alitoa wito kwa wananchi wanapopata matukio ya moto waweze kutoa taarufa kwa mapema ili nao waweze kufika kwa wakati na kuweza kufanya maokozi ambapo pia akitoa pole kwa Meneja na mfanyakazi aliyepata majeruhi apone na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Awali akizungumza,Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Nuhu Mmbaga alilishukuru Jeshi la Zimamoto na Ukoaji na vikosi vinavyohusika na majanga kuwahi kufika kwenye eneo la tukio kweli moto ulitokea na uliweza kudhibitiwsa kikamilifu.

Alisema lakini mfanyakazi mwenzao alipata madhara kidogo na kupelekwa Hospitali natukio hilo limetokea lakini wameweza kulihimili na ni njia mojawapo ya kuweza kuwa na utayari kuweza kuhimili majanga yanapojitokeza.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC inashiriki katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Utaratibu huu wa kushiriki katika maonesho mbalimbali nchini ni sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kutoa elimu ya Mpiga Kura endelevu ambapo wadau mbalimbali wa Tume hufika katika Banda hilo na kupata elimu hiyo.

Maonesho haya ambayo huandaliwa na Mahakama ya Tanzania ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya sheria na kuanza kwa mwaka mpya wa Mahakama.

Mwaka huu maonesho haya yamebeba kauli mbiu isemayo "Umuhimu wa Dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa:Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo Jumuishi wa Haki Jinai" yameanza tarehe 24 Januari,2024 na yanatarajia kumalizika tarehe 30 Januari, 2024.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Cuthbert Mapunda (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Cuthbert Mapunda (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bi.Neseria Leng’ida (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma
Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square.

Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakizungumza na mdau aliyetembelea banda la Tume katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakizungumza na mdau aliyetembelea banda la Tume katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Loshilu Saning’o (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima akifungua mkutano wa Tume na wadau wa uchagaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mapsap Linme iliyopo wilayani Rorya Mkoa wa Mara.
Wakili wa Serikali Mkuu Kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bi. Rose Chilongozi akisoma mada ya uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi wilayani Rorya.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mapsap Linme iliyopo wilayani Rorya Mkoa wa Mara.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mapsap Linme iliyopo wilayani Rorya Mkoa wa Mara.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa baada ya kumalizika kwa mkutano wa Tume na wadau wa uchagaguzi.

Na Mwandishi Wetu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wadau wa uchaguzi kufikisha ujumbe sahihi kwa wananchi wa Kata ya Ikoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ili wananchi wenye sifa ya kuandikishwa na kuboresha taarifa zao wajitokeze kwa wingi kushiriki uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwabainisha waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima wakati akifungua mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mapsap Linme iliyopo wilayani Rorya Mkoa wa Mara.

Aliwaasa wadau wote wa uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika kipindi chote cha uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

“Ni tegemeo la Tume kuona mnafikisha ujumbe sahihi kwa wananchi ambako uboreshaji wa majaribio yatafanyika ili wananchi wenye sifa ya kuandikishwa na kuboresha taarifa zao wajitokeze kwa wingi kushiriki zoezi hili na kuwabainisha waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura.

Pia, nawaasa wadau wote kuendelea kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika kipindi chote cha uboreshaji wa majaribio la Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.”, alisema Bw. Kailima.

Mbali na kuwaasa wadau hao wa uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi alisema kuwa Tume imejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu uboreshaji wa majaribio kwa kutumia njia mbalimbali za kutoa elimu ya mpiga kura zikiwemo; kukutana na wadau wengine wa uchaguzi.

Aliongeza kuwa vyama vya siasa vitashiriki katika uboreshaji wa majariobio kwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo cha kuandikisha wapiga kura, lengo ni kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa majaribio wa Daftari.

Alisisiti kwa kuwaomba wadau wa uchaguzi kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo kwenye mkutano huo ili kufanikisha utekelezaji wa uboreshaji huo.

Mkutano huo wa wadau wa uchaguzi umewashirikisha viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wazee wa kimila, watu wenye ulemavu, wawakilisha wa vijana, wawakilishi wa wanawake na asasi za kiraia kwa ujumla kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi itafanya uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa huu wa Mara na Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, mkoa wa Tabora, utakaofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.