Mkurugenzi wa BRAC Tanzania, Joydeep Sinha Roy akikabidhi msaada wa vifaa muhimu na rasilimaliza elimu kwa Mwenyekiti wa Shule ya Bethasadia Raymond Mashary (kushoto) , wakati wa kuadhimisha miaka 53 toka kuanzishwa kwa Shirika hilo la BRAC .
Shirika lisilo la kiserikali BRAC Tanzania imesherehekea mwaka wake wa 53, kwa kutoa vifaa muhimu na rasilimali za elimu ili kusaidia uwezeshaji wa wasichana na upatikanaji wa elimu bora.
Katika kurudisha kwenye jamii, wafanyakazi wa BRAC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BRAC Tanzania Joydeep Sinha Roy wameshiriki kwa pamoja kutoa vifaa muhimu na rasilimali za elimu kusaidia uwezeshaji wa wasichana na upatikanaji wa elimu bora katika Shule ya Yatima ya Wasichana ya Bethesaida iliyopo Mbezi Mpiiji Magohe.
Akizungumza na wanafunzi hao baada ya kufika Shuleni, Joydeep alisema Kujitolea kwao nchini Tanzania ni katika kuonesha Shirika lao limejikita katika masuala ya kijamii na uwezeshaji wa watoto wa kike kupitia sekta mbalimbali.
Joydeep amesema, wanasherekea mafanikio haya kwa pamoja na kutazamia siku zijazo zilizojaa matumaini, na mabadiliko chanya kupitia Shirika lao ambali limekuwa linajikita katika masuala ya uwezeshaji kiuchumi na kijamii.
"Lengo ni kuendelea kushirikiana na serikali, watunga sera, na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kupunguza umaskini ambapo kupitia Shirika letu tuna huduma za kifedha, Makuzi, Malezi na Maendeleo ya Awali ya Watoto Wadogo, Uwezeshaji wa Vijana, Elimu, Kilimo, na Programu ya Uondoaji Umasikini Uliokithiri," amesema Joydeep.
Mwenyekiti na mwanzilishi wa Shule ya Sekondari Bethsadia , Raymond Machary amewashukuru BRAC Tanzania kwa kuwakumbuka mabinti hao ambapo wengi wao bado wanahitaji msaada huo kwani Shule hiyo inachukua wale wanachukuwa wanafunzi wenye uhitaji ambao wengi wao wakiwa hawana wazazi.
Mashary amesisitiza yapo Mashirika na Taasisi ambazo zinaweza kujitolea kwa ajilo ya wanafunzi hawa, kikubwa ni kuwa na moyo wa kujitolea kama walivyofanya Shirika la BRAC, na yeye kama Kiongozi Mkuu wa Shule hiyo ya wasichana anawakaribisha wakati wowote.
Siku ya BRAC mwaka huu imesherehekewa nchi nzima tarehe 24 machi 2025, kwa kutembelea sehemu mbalimbali wakiwa na Kauli mbiu "Pamoja kama BRAC: Kusherehekea kwa Pamoja," ambapo itajumuisha hotuba za kuhamasisha, majadiliano kuhusu mafanikio ya Shirika lao, na ramani ya kimkakati kwa ajili ya mipango ya baadaye.
Mbali na kusherehekea mafanikio yao, Siku ya BRAC 2025 imekusudia kukuza umoja na ushirikiano wa ndani kupitia mijadala. Mikutano hii itatoa jukwaa kwa wafanyakazi kushiriki mawazo kuhusu changamoto, uvumbuzi, na athari halisi za kazi wanazokutana pamoja na Washiriki kutoa ushuhuda wa hisia kutoka kwa washiriki wa programu na wateja wakionyesha mabadiliko halisi yaliyowezeshwa na programu za BRAC.
BRAC Tanzania ni shirika linalounganisha mashirika mbalimbali ya BRAC, yakiwemo BRAC Maendeleo Tanzania (BMT), BRAC Tanzania Finance Limited (BTFL), na BRAC Enterprises Tanzania Ltd (BETL), ambayo yanafanya kazi za mabadiliko kama vile huduma za kifedha, Makuzi, Malezi na Maendeleo ya Awali ya Watoto Wadogo, Uwezeshaji wa Vijana, Elimu, Kilimo, na Programu ya Uondoaji Umasikini Uliokithiri ambapo takribani watu Milioni 1.4 wanafikiwa na huduma zao.
Mkurugenzi wa BRAC Tanzania, Joydeep Sinha Roy akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bethasaida walipotembelea na kutoa msaada wa vifaa muhimu na rasilimaliza elimu kwa wasichana hao, hilo limefanyika wakati wa kuadhimisha miaka 53 toka kuanzishwa kwa Shirika hilo.



Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bethasadia wakipokea msaada wa vifaa maalumu na rasilimali elimu kutoka Shiroka la BRAC TanzaniaMkurugenzi wa BRAC Tanzania, Joydeep Sinha Roy akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bethasaida walipotembelea na kutoa msaada wa vifaa muhimu na rasilimaliza elimu kwa wasichana hao, hilo limefanyika wakati wa kuadhimisha miaka 53 toka kuanzishwa kwa Shirika hilo.



Toa Maoni Yako:
0 comments: