Jumla ya wanafunzi 567,567 wamefaulu mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011na watafanyiwa mtihani wa majaribio kabla ya kuanza masomo yao rasmi katika shule walizochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Akitangaza matokeo hayo (leo), jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (Mb.) amesema, utaratibu huo wa kufanyiwa majaribio utaanza mwakani 2012, ambapo wanafunzi waliofaulu watafanyiwa majaribio ya kupima stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Wakati huo huo, Baraza la Mtihani la Taifa limefuta matokeo yote ya watahiniwa 9,736 sawa na asilimia 1.0 waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo.
“Mwanafunzi atakayebainika kuwa kajiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Waziri Mulugo.
Akizungumzia kuhusu kiwango cha ufaulu alisema kimeongezeka hadi kufikia asilimia 58.28 ukilinganisha na cha mwaka jana ambacho kilikuwa asimilia 53.52.
Aliongeza kuwa kiwango cha ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hesabu kimepanda . Somo la Kiingereza kutoka asilimia 36.47 mwaka jana hadi asilimia 46.70 kwa mwaka huu , wakati somo la Sayansi ni asilimia 61.33 mwaka huu toka asilimia 56.05mwaka jana na Hesabu asilimia 39.36 mwaka huu toka asilimia 24.70mwaka jana.
Jumla ya wanafunzi 983, 545 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi wa Septemba 2011 na kuonesha kuwa, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 53.52 mwaka jana hadi 58.28. Jumla ya wasichana waliofaulu ni 27,377 na wavulana ni 289,190.
Wakati huo huo, Serikali imesema, kazi ya kuhakiki madai ya walimu imekamilika tangu Desemba 2, mwaka huu na kwamba madai hayo ni kiasi cha sh. bilioni 52.
Akijibu swali lililoulizwa na waandishi kuhusu madai ya walimu, Naibu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba amesema, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 ni za mishahara na bilioni 22 ni za madai mengineyo.
Bw. Gesimba ameongeza kuwa, madai ya malipo mengine yataanza kulipwa mwezi huu (Desemba) na madai ya malipo ya mishahara yatalipwa ifikapo Januari 2012.
Hata hivyo alisema tayari Hazina wameshalipa bilioni 28 za madai ya mishahara kuanzia Julai mwaka jana hadi Novemba mwaka huu.
Na Gradys Sigera & Magreth Kinabo – MAELEZO
TUNASHUKURU KWA TAARIFA ZENU ZIMEKAA VZR NINAOMBA KUTUMIWA MATOKEO YA S/M KASIGA YA KOROGWE TANGA YA 2011 TAFADHARI
ReplyDeleteNinaomba kutumiwa matokeo ya s/m kaswa ya Tabora ya 2011 tafadhari
DeleteNinaomba kutumiwa matokeo ya s/m kaswa ya Tabora ya 2011 tafadhari
DeleteNaomba kutumiwa matokeo ya darasa la Saba mwaka 2011 shule ya msingi madege wilaya ya kilolo mkoa wa iringa
ReplyDeleteGud
ReplyDeleteNaomba matokeo ya kondoa shule keikei
ReplyDeleteNaomb mnitumie matokeo ya la saba 2011
ReplyDeleteNaomba nitumie matokeo ya darasa la saba 2010 shule ya msingi mvumi wilaya ya kilosa mkoa wa morogoro
ReplyDeleteNaomba kutumiwa matokeo ya s/m bulumbela2011
ReplyDeleteNashukuru kwa kazi yenu nzur, nahitaji matokeo ya darasa la Saba shule ya msingi ipoma mkoan mbeya-busokelo ya mwaka 2011, tafadhari
ReplyDeleteNinaomba matokeo ya S/M Rocken hill ya mwaka 2011.
ReplyDeleteNaombeni matokeo s/m matale wilaya meatu mkoan simiyu
ReplyDeleteNaomba matokeo ya darasa la saba s/m Isenga A ya Mwanza 2011
ReplyDeleteSalaam, naomba matokeo ya darasa la saba 2011 S/m Isenga A (Mwanza)
ReplyDeleteNinaomba kutumiwa matokeo ya s/m zahanati yarugusu geita
ReplyDeleteMgeta mwarazi
ReplyDeleteNaomba kutumiwa matokeo yangu ya darasa LA saba
ReplyDeleteNaomba kutumiwa matokeo yangu
ReplyDeleteNaomba kutumiwa matokeo ya darasa la saba 2011 shule ya msingi nyakanazi, mkoa wa kagera
ReplyDeleteMatokeo kigembe primary school naomba
ReplyDeleteNaomba kutumiwa matokeo darasa la saba 2011 s/m Ruruma mkoa singida wilaya iramba
ReplyDeleteSorry naomba kutumiwa matokeo darasa LA saba 2011 kahama shule ya msingi bukooba
ReplyDeleteNaomba matokeo ya s/m bukooba kahama 2011
ReplyDeleteNaomb matokeo y darasa la saba 2011 s/m mafere (muheza)
ReplyDeleteNaomba kutumia matokeo ya s/m kongowe ya kibaha pwani 2011
ReplyDeleteNinomba kutumiwa matokeo ya darasa la Saba 2011 s/m dissa kondoa
ReplyDelete