Jumla ya wanafunzi 567,567 wamefaulu mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011na watafanyiwa mtihani wa majaribio kabla ya kuanza masomo yao rasmi katika shule walizochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Akitangaza matokeo hayo (leo), jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (Mb.) amesema, utaratibu huo wa kufanyiwa majaribio utaanza mwakani 2012, ambapo wanafunzi waliofaulu watafanyiwa majaribio ya kupima stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Wakati huo huo, Baraza la Mtihani la Taifa limefuta matokeo yote ya watahiniwa 9,736 sawa na asilimia 1.0 waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo.

“Mwanafunzi atakayebainika kuwa kajiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Waziri Mulugo.

Akizungumzia kuhusu kiwango cha ufaulu alisema kimeongezeka hadi kufikia asilimia 58.28 ukilinganisha na cha mwaka jana ambacho kilikuwa asimilia 53.52.

Aliongeza kuwa kiwango cha ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hesabu kimepanda . Somo la Kiingereza kutoka asilimia 36.47 mwaka jana hadi asilimia 46.70 kwa mwaka huu , wakati somo la Sayansi ni asilimia 61.33 mwaka huu toka asilimia 56.05mwaka jana na Hesabu asilimia 39.36 mwaka huu toka asilimia 24.70mwaka jana.

Jumla ya wanafunzi 983, 545 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi wa Septemba 2011 na kuonesha kuwa, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 53.52 mwaka jana hadi 58.28. Jumla ya wasichana waliofaulu ni 27,377 na wavulana ni 289,190.

Wakati huo huo, Serikali imesema, kazi ya kuhakiki madai ya walimu imekamilika tangu Desemba 2, mwaka huu na kwamba madai hayo ni kiasi cha sh. bilioni 52.

Akijibu swali lililoulizwa na waandishi kuhusu madai ya walimu, Naibu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba amesema, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 ni za mishahara na bilioni 22 ni za madai mengineyo.

Bw. Gesimba ameongeza kuwa, madai ya malipo mengine yataanza kulipwa mwezi huu (Desemba) na madai ya malipo ya mishahara yatalipwa ifikapo Januari 2012.

Hata hivyo alisema tayari Hazina wameshalipa bilioni 28 za madai ya mishahara kuanzia Julai mwaka jana hadi Novemba mwaka huu.

Na Gradys Sigera & Magreth Kinabo – MAELEZO
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

26 comments:

  1. TUNASHUKURU KWA TAARIFA ZENU ZIMEKAA VZR NINAOMBA KUTUMIWA MATOKEO YA S/M KASIGA YA KOROGWE TANGA YA 2011 TAFADHARI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ninaomba kutumiwa matokeo ya s/m kaswa ya Tabora ya 2011 tafadhari

      Delete
    2. Ninaomba kutumiwa matokeo ya s/m kaswa ya Tabora ya 2011 tafadhari

      Delete
  2. Naomba kutumiwa matokeo ya darasa la Saba mwaka 2011 shule ya msingi madege wilaya ya kilolo mkoa wa iringa

    ReplyDelete
  3. Naomba matokeo ya kondoa shule keikei


    ReplyDelete
  4. Naomb mnitumie matokeo ya la saba 2011

    ReplyDelete
  5. Naomba nitumie matokeo ya darasa la saba 2010 shule ya msingi mvumi wilaya ya kilosa mkoa wa morogoro

    ReplyDelete
  6. Naomba kutumiwa matokeo ya s/m bulumbela2011

    ReplyDelete
  7. Nashukuru kwa kazi yenu nzur, nahitaji matokeo ya darasa la Saba shule ya msingi ipoma mkoan mbeya-busokelo ya mwaka 2011, tafadhari

    ReplyDelete
  8. Ninaomba matokeo ya S/M Rocken hill ya mwaka 2011.

    ReplyDelete
  9. Naombeni matokeo s/m matale wilaya meatu mkoan simiyu

    ReplyDelete
  10. Naomba matokeo ya darasa la saba s/m Isenga A ya Mwanza 2011

    ReplyDelete
  11. Salaam, naomba matokeo ya darasa la saba 2011 S/m Isenga A (Mwanza)

    ReplyDelete
  12. Ninaomba kutumiwa matokeo ya s/m zahanati yarugusu geita

    ReplyDelete
  13. Naomba kutumiwa matokeo yangu ya darasa LA saba

    ReplyDelete
  14. Naomba kutumiwa matokeo yangu

    ReplyDelete
  15. Naomba kutumiwa matokeo ya darasa la saba 2011 shule ya msingi nyakanazi, mkoa wa kagera

    ReplyDelete
  16. Matokeo kigembe primary school naomba

    ReplyDelete
  17. Naomba kutumiwa matokeo darasa la saba 2011 s/m Ruruma mkoa singida wilaya iramba

    ReplyDelete
  18. Sorry naomba kutumiwa matokeo darasa LA saba 2011 kahama shule ya msingi bukooba

    ReplyDelete
  19. Naomba matokeo ya s/m bukooba kahama 2011

    ReplyDelete
  20. Naomb matokeo y darasa la saba 2011 s/m mafere (muheza)

    ReplyDelete
  21. Naomba kutumia matokeo ya s/m kongowe ya kibaha pwani 2011

    ReplyDelete
  22. Ninomba kutumiwa matokeo ya darasa la Saba 2011 s/m dissa kondoa

    ReplyDelete