Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo SSP. Zauda Mohamed (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Maafisa, Wakaguzi na Askari kutoka kikosini wakipokea vifaa vya TEHAMA kwa Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Veronica Ignatus mapema wiki hii jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu.

Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Arusha leo Machi 28, 2025 imekabidhi kompyuta kwa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa ajili ya matumizi ya mifumo ambayo inatummiwa kwa sasa na kikosi hicho katika kutoa huduma.

Vifaa hivyo vine kabidhiwa na Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Veronica Ignatus na kupokelewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo SSP. Zauda Mohamed pamoja na Maafisa, Wakaguzi na Askari kutoka kikosini hapo.

Aidha SSP Zauda amebainisha kuwa vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya kiutendaji ndani ya kikosi hicho ambacho kimejikita zaidi katika matumizi ya mifumo katika utoaji huduma.

Huu ikiwa ni muendelezo wa kwani mwazoni mwa mwezi machi Kamati hiyo ya Usalama barabarani mkoa wa Arusha iliweza kukabidhi Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha Machi 06, 2025 magari matano aina ya Toyota Probox kwa ajili ya matumizi ya Kikosi cha Usalama barabarani.

Magari hayo yamekabidhiwa na Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Veronica Ignatus na kupokelewa na Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP. Debora Lukololo na kushuhudiwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo SSP. Zauda Mohamed pamoja na Maafisa, Wakaguzi na Askari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: