Jijini Dar es Salaam jana kulishuhudiwa mjadala muhimu uliowakutanisha wadau wa tasnia ya muziki kupitia jukwaa la AfroExchange, lililodhaminiwa na Johnnie Walker, kwa lengo la kujadili namna ya kuufikisha muziki wa Tanzania kwenye masoko ya kimataifa.

Mkutano huo ulikuwa mwanzo wa mfululizo wa mazungumzo chini ya AfroExchange, unaolenga kubaini njia za kuweza kukuza na kusambaza sanaa na muziki wa Afrika nje ya mipaka yake. Katika hatua ya kwanza, mjadala uliwaweka DJs katikati, ukitambua nafasi yao muhimu kama wachochezi wa ladha ya muziki, waunganishaji wa masoko na daraja la kuifikisha sauti ya Afrika watu wengi zaidi.
Washiriki walijadili kwa kina changamoto zinazokwamisha muziki wa Tanzania kupenya katika soko la kimataifa, huku wakisisitiza fursa zilizopo kwa DJs katika kusukuma muziki huo kuvuka mipaka.

Mbali na mazungumzo, AfroExchange pia ilitangaza hatua ya utekelezaji. Kupitia mpango huo, DJs wa Tanzania watadhaminiwa kushiriki kwenye tukio la DJ Consequence nchini Nigeria, fursa itakayomuwezesha kupata uzoefu wa kimataifa pamoja na kujenga mtandao.
Hatua hii inaashiria mwanzo wa juhudi za kuimarisha ushirikiano ndani ya tasnia ya muziki barani Afrika, huku ikifungua milango kwa vipaji vya Tanzania kufikia masoko mapya.

AfroExchange inaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha wadau, kuchochea mazungumzo yenye tija, na kuleta fursa zitakazosaidia muziki wa Tanzania kusikika kimataifa.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: