Articles by "BURUDANI"
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Kumekuwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na Timu ya Tabora United zikimuhusisha Kocha Mkuu Denis Laurence pamoja na msaidizi wake Masoud Juma kuwa wanataka kuondoka kwa kile kinachoelezwa hawajaridhishwa na mazingira lakini pia hawajasainishwa mikataba yao ya kazi.

Kwanza kabisa Klabu inapinga vikali upotoshwaji wa taarifa hizi kwa baadhi ya watu ambao hawanania njema na Timu ya Tabora United. Ikumbukwe kuwa Tabora United inaongozwa na viongozi ambao wanatambua na kufahamu umuhimu wa mfanyakazi kwa kila idara.

Tukianza na suala la Kocha Mkuu Denis Laurence ni kwamba kabla ya kuwasili kwa Kocha Laurence akiwa Ufaransa amekuwa akiifuatilia Timu ya Tabora United kupitia video za mechi mbalimbali lakini pia anaifahamu Timu kutokana na mazungumzo ambayo yalikuwa fakifanyika baina yake na viongozi wa klabu.

Lakini pia Kocha Laurence amewahi kufanya kazi na Msaidizi wake ambaye wanafanya kazi pamoja ndani ya Tabora United Masoud Juma na ndiye aliyempendeza hivyo hata suala la mazingira tafsiri yake ni kwamba analifahamu kwa kuwa anaifahamu vyema Timu ya Tabora United.

Kuhusu mikataba kwa hali ya kawaida hakuna mtumishi yoyote ambaye anaweza kuanza kufanya kazi pasipo kusainishwa mkataba wake hicho kitu hakiwezekani na hakijawahi kutokea tangu Dunia imeumbwa.

Kocha Laurence pamoja na Msaidizi wake Masoud walipewa mkataba na kusaini kulingana na taratibu za kazi zinavyotaka na ndio mana waliweza kuanza kazi mara moja na hadi sasa wanaendelea na majukumu yao kama kawaida ikiwa ni siku ya sita tangu walipotambulishwa.

Na hili jambo linafahamika kabisa kuwa mtu anapoanza kufanya kazi maana yake ni kwamba tayari walishakubalina na mwajiri hivyo kusema Kocha Mkuu na msaidizi wake wanaweza kuacha kazi hizo ni taarifa za uzushi na uongo na tunaomba mzipuuze.

Kuhusu mishahara ya wachezaji, viongozi pamoja na Benchi la ufundi, hakuna ambaye anadai hadi sasa na kwamba mara nyingi uongozi umekuwa ukijali masilahi ya watumishi wa idara zote kwa kuhaikisha kuwa stahiki zao wanalipwa kwa wakati.

Uongozi wa Tabora United umekuwa ukifanya mrejesho wa matumizi ya fedha zinazotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB kupitia kwa mzamini Mkuu wa haki za matangazo Azam Media kila mwezi na kwamba tumekuwa tukipokea fedha hizo. Hivyo kusema kwamba Tabora United haipatiwi fedha za haki ya matangazo huo ni upotoshwaji na kutaka kutugombanisha na mamlaka husika.

Kuhusu wachezaji wa Timu ya vijana Under 20, wote waliwasili tangu juzi Tabora wakitokea Geita ambapo walikuwa na mchezo wa Ligi ya vijana hatua ya makundi hivyo wachezaji hawajakwama sehemu yoyote.

Hivyo kauli ya Klabu ni kwamba mashabiki na wadau wote wampira ambao wanaiunga mkono Timu ya Tabora United wapuuze taarifa hizo kwani zinalenga kuchafua Brandi ya Klabu kwa makusudi hivyo kama uongozi unatambua thamani na umuhimu wa kila mmoja ndani na nje ya Klabu.

Timu inaendelea kujifua kwa ajili ya michezo ya Michuano ya kombe la Azam Sports Federation ASFC dhidi ya Singida Fountaingat pamoja na Ligi ya NBC soka Tanzania Bara itakayoendelea baada ya kumalizika kwa kalenda ya FIFA.

Imetolewa leo Machi 27
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tabora United.
Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro kushoto akimkabidhi Kombe la Mashindano ya Odo Ummy Cup Nahodha wa timu ya Kiomoni FC mara baada ya kuibuka Mabingwa kwa kuifunga Nguvumali FC penati 3-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga juzi ambapo mshindi huyo alipatiwa pia kitita cha Sh Milioni 3,pikipiki ya magurudumu matatu,Ng’ombe,Jezi Seti pamoja na mpira kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya ambaye ndie muandaaji wa Mashindano hayo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman
Na Oscar Assenga, TANGA

TIMU ya Kiomoni FC wametawazwa kuwa Mabingwa wapya wa Michuano ya Kombe la Odo Ummy Cup baada ya kuibamiza timu ya Nguvumali FC penati 3-1 katika mchezo wa Fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga.

Kutokana na ushindi huo waliweza kujinyakulia kitita cha Sh.Milioni 3,Pikipiki yenye Magurudumu matatu,Ng’ombe,Jezi Seti pamoja na mipira huku Mshindi pili timu ya Nguvumali FC waliweza kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 2.5 na Mpira na Jezi Seti 1.

Michuano hiyo ya Odo Ummy Cup huchezwa kila mwaka kwa kushirikisha kata zote za Jimbo la Tanga yakiwa na lengo la kuibua vipaji na kukuza kiwango cha soka kwa vijana ambao kupitia mpira wanaweza kujikwamua kiuchumi.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ambapo kila timu iliingia uwanjani hapo ikitaka kuibuka na ushindi ili kuweza kuchukua ubingwa wa michuano hiyo ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko zilitoka sare tasa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliingia ikiwa na hari kubwa kutokana na kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake ili kuweza kujiimarisha kwa lengo la kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Wakionekana kucheza kwa umahiri mkubwa Kimoni FC walianza kwa kulishambulia lango la wapinzani wao bila kuwepo kwa mafanikio yoyote ambapo kila wachezaji walipokuwa wakipiga mashuti langoni mwao liligonga mwamba na kutoka nje.

Kutokana na ushindani wa mchezo huo ulizilazimu timu zote kutoka uwanjani dakika 90 bila kuona milango ya kila mmoja na hivyo mwamuzi wa mchezo huo kulazimika kupelekea mchezo huo kwenye mikwaju ya penati ambao ndipo kiomoni waliposhinda mabao hayo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mcheo huo wa Fainali Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni aliwapongeza waandaaji wa mashindano hayo huku akieleza kwamba mashindano ikiwemo Mbunge Ummy Mwalimu.

“Ukiona vyaelea ujue vimeundwa hili ya leo tuna kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Mbunge wetu Ummy Mwalimu niseme kama Waziri mwenye thamana ya michezo nimeshahudhuia mashindano yanayoandaliwa na wabunge mwengi sana sijaona mashindano mazuri kama haya”Alisema

Alisema mashindano haya ni mazuri na makubwa ambayo sijapata kuyaona katika maeneo mengine na Mbunge Ummy ana sifa ya kipekee kwa kuwajali wananchi wa Jimbo lake kutokana na kuhakikisha anawapigania ili kuweza kuondoa kero zenu.

Aidha alisema wanaposema michezo ni ajira wanaamini pia ni uchumi na wao kama Wizara wamemua hivi sasa michezo ni ajira na uchumi hivyo mashindano kama hayo watashirikiana na waandaaji kuhakikisha wanaibua vipaji na kuviendeleza.

Hata hivyo alisema kwamba mkoa wa Tanga ndio chimbuka la vipaji na wao serikali wataendelea kuiangalia Tanga huku akieleza kwamba Mbunge Ummy amepeleka ombi kwao kwamba uwanja huo wa Lamore ambao umechezewa fainali hiyo upandwe nyasi uwe mzuri ili fainali za mwakani ziwe nzuri .

“Na mimi nimemuhaidi Mbunge Ummy kwamba nitawaleta wataalamu kufanya tathimini ili uwanja uweze kuwa katikaa hali nzuri kutokana na kwamba umuhimu wa mashindano hayo ya Odo Ummy Cup”Alisema

Awali akizungumza katika fainali hiyo ,Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya alisema kwamba suala la Odo Ummy Cup ni mchango wake katika kutekeleza ilani ya CCM ibara ya 243 ambayo inawataka kuwekeza kwenye mpira wa migu hasa kwa vijana.

Alisema wanamshukuru pia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajab Abdurhaman kutokana na kwamba amekuwa akiwasaidia na kuwaleta na kuwaongoza kwenye kutekeleza ilani.

Aidha alisema mashindano hayo lengo ni kuwaleta pamoja vijana wa Tanga mjini na yameleta moja,mshikamano na hamasa ya kumweka karibu na vijana huku akishukuru timu zote kutoka Kata 27 ambazo zilishiriki kwenye michuano hiyo.

“Lakini pia nishukuru kamati za Siasa za CCM kwa kujitoa kusimamia mashindano hayo pamoja na timu ya Hamasa ya UVCCM pia niwashukuru wadhamini wetu kwa kuuunga mkono wakiwemo wadau wetu Assemble Insurance kwa kutuunga mkono”Alisema

Hata hivyo kwa upande wake,Mwenyeiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajab Abdurhaman atumia fursa hiyo kuwataka wabunge na madiwani wa mkoa huo wahakikisha wanaendelea michezo katika maeneo yao.

“Kwani kufanya hivyo ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ambayo tumehaidi kuendeleza michezo hivyo lililofanyika linatafsiri ilani kwa vitendo hivyo wabunge na madiwani hakikisheni hili linatekelezwa”Alisema.




Na Oscar Assenga,TANGA.

WAZIRI wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Dkt Damas Ndumbaro amepongeza Mashindano ya Oddo Ummy Cup huku akieleza kwamba watayatumia kuangalia vipaji vya wachezaji na baadae aone namna ya kumpigia simu Kocha wa timu ya Taifa ili kuona namna ya kuwapeleka kwenye Taifa ya Taifa.

Dkt Ndumbaro aliyasema hayo Machi 10 mwaka huu Jijini Tanga ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Fainali ya Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Oddo Ummy Cup ambayo yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kwa lengo la kuibua vipaji vya wachezaji wachanga.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya Lamore Jijini Tanga na yanashirikisha timu mbalimbali kutoka kwenye Jimbo la Tanga Mjini linaongozwa na Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya

“Leo nimekuja Tanga kwa lengo la kuja kuangalia viwango vya wachezaji ili baadae nimpiga simu kocha wa timu ya Taifa kuona namna nzuri ya kuweza kuwajumuisha kwenye timu zetu za Taifa”Alisema Waziri Ndumbaro.

Katika Fainali hiyo timu za Nguvumali na Kiomoni zilitinga hatua hiyo kwa kufanya vizuri kwa kila mmoja kumtoa mpinzani mwenzake na hivyo kulazimika kukutana kwenye hatua hiyo ya kumsaka Bingwa ambapo Bingwa alikuwa ni timu ya Kiomoni

“Kwa heshima ya Waziri Ummy Mwalimu nimeacha shughuli zote nimekuja Tanga mimi Waziri wa michezo ili niweze kuona vipaji vilivyopo hapa Tanga kwa maana historia ya mpira ni kubwa na nimeambiwa Juma Mgunda yupo hapa hivyo tunaweza kutumia mashindano haya kupata wachezaji wa timu ya Taifa”Alisema Waziri Ndumbaro.

Akubali Ombi la Mbunge Ummy

Katika hatua nyengine Waziri Ndumbaro amekubali ombi la Mbunge Ummy Mwalimu ambaye alimuomba atafute shule mmoja mkoani humo waifanye kuwa ya vipaji vya michezo.

Akijibu Ombi hilo Waziri Dkt Ndumbaro alisema kwamba yeye akisema wataona namna ya kwenda kulitekeleza ili uwepo wa shule hiyo uweze kupatikana mkoani Tanga.

“Mh Ummy nimepokea ombi lao wewe ukisema mimi ni utekelezaji tu hivyo nitakwenda kulifanyia kazi”Alisema.

Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kimefanya hafla ya kufunga Kozi mbili za ‘Area Control Procedure’ namba 35 na Kozi ya Ndege nyuki (Drone) namba 16 kwa wakufunzi hao kuhimizwa juu ya kufanya kazi kwa weledi.

Nasaha hizo zimetolewa Machi 08, 2024 na Mkuu wa Chuo cha CATC, Aristid Kanje wakati wa kufunga kozi hizo mbili ambazo zimeambatana na mafunzo ya weledi yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Mashirika ya Ndege nchini (TAOA) Bi Lathifa Sykes.

CATC moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.












Mtwara. Kwa kutambua ugumu unaowakabili baadhi ya wanafunzi kukidhi mahitaji yao muhimu, taasisi ya Dido Mwanafunzi Initiative (DMI) kwa kushirikiana na Female Future Program Cohort 9 imetoa msaada wa sare za shule, madaftari na viatu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani Mtwara.

Msaada huo uliotolewa kwa Sekondari za Naliendele, Mikindani na Nanyamba pamoja na Shule za Msingi Mwenge na Mtawanya pia umejumuisha taulo za kike, vesti, mabegi ya shule na vifaa vya kujifunzia zikiwamo kalamu.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa DMI, Rehema Moses, amesema baada ya serikali kufuta ada na michango mingine shuleni uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza hata wale wanaojiunga kidato cha kwanza umekuwa mkubwa hivyo kuibua changamoto nyingine zinazohitaji ushiriki wa wadau kuzitatua.

“Serikali inajitahidi kukuza elimu nchini ila, familia nyingi haziwezi kukidhi baadhi ya mahitaji muhimu hasa ya wanafunzi kama vile sare za shule, madaftari au taulo za kike vitu ambavyo havitolewi na serikali. Sisi tunayo programu ya mvishe aende shule inayolenga kusaidia kutatua baadhi ya changamoto hizi. 

Leo tupo hapa Mtwara kesho tutakuwa mkoa mwingine,” amsema Rehema Moses.

Kwa upande wake, Rais wa Female Future Program Cohort 9, Maureen Njeri amesema wakati wanahitimu shahada ya juu katika Taasisi ya ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) mwaka 2022 waliona wanayo kila sababu ya kusaidia kutatua kero na changamoto wanazokabiliana nazo wanawake wenzao katika jamii hivyo kushirikiana na DMI katika kampeni ya Mvishe Aendee Shule.
“Leo ni mwendelezo wa juhudi tunazozifanya ili kuisaidia jamii. Vifaa tulivyovitoa vimetokana na michango tunayoitoa. Ni kidogo lakini tunaamini inasaidia kupunguza tatizo. Iwapo wadau wengine watajitokeza, tunaweza kumaliza baadhi ya changamoto zilizopo nchini, na kuunga juhudi za serikali katika kuimarisha elimu” amesema Maureen.

Female Future Program iliyozinduliwa mwaka 2016 na Rais Samia Suluhu Hassan kipindi akiwa Makamu wa Rais, ipo chini ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ikisimamiwa na Shule ya Biashara ya ESAMI, inalenga kuwawezesha wanawake wengi zaidi kuingia kwenye nafasi za uongozi ili kushiriki kutoa uamuzi wa masuala mbalimbali. 

“Lengo hilo halitowezekana iwapo mwanamke na mwanamme hawatoandaliwa tangu wakiwa wadogo. Elimu ndio msingi wa kila kitu ndio maana tunakwenda mpaka shule za msingi kusaidia kuwakuza wasichana na wavulana wenye changamoto za kijamii,” ameongeza Maureen.
Akipokea taulo za kike,  Sofia Bakari, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Sekondari ya Mikindani amesema wasichana wasio na uwezo hushindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa kwenye siku zao hivyo kuwapa changamoto ya kukimbizana na wenzao ili wasiachwe nyuma.
 
“Kuna wasichana wanaopoteza mpaka siku saba kila mwezi kutokana na hedhi. Msaada huu ni muhimu mimi na wenzangu tulioupokea tunajua thamani yake. Tunawashukuru sana kwa kutukumbuka,” amesema Sofia.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mikindani Sekondari, Yonas Boniface Mtimbati, amesema kuna wanafunzi wengi katika shule hiyo ambao wazazi au walezi wao hawana uwezo wa kumudu mahitaji yote ya watoto wao hivyo wanapojitokeza wadau kama DMI na Female Future Program kusaidia inaongeza moyo wa kujifunza kwa wanafunzi hao.
“Wapo wanafunzi wasio na viatu wengine hawana au wanavaa sare zilizochakaa. Wadau wa elimu wanahitajika kusaidia vifaa hivi ili kuwapa moyo wa kujifunza bila kuhisi kunyanyapaliwa na wenzao wenye mahitaji yote,” amesema Mwalimu Yonas.
Mkurugenzi wa Dido Mwanafunzi Initiative, Rehema Moses (kushoto) na Dkt. Riziki Suleiman, wakimvisha viatu mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge iliyopo katika Kata ya Naliendele mkoani Mtwara.
Rehema Moses, Mkurugenzi Mtendaji Dido Mwanafunzi Initiative, Doreen Dominic, Mkuu wa Kitengo cha Umma, Benki ya Stanbic na Maureen Njeri, Rais wa Darasa la Female Future Program Cohort 9 katika hafla ya kugawa mabegi, sare za shule, chupi na viatu vya shule kwa wanafunzi wakiume na wakike, katika kata ya Naliendele, mkoani Mtwara.
Na Andrew Chale, Zanzibar.
MTOTO wa gwiji wa muziki wa Afrika, Hayati Oliver Mutukudzi, Selmor Mutukudzi amekonga nyoyo za mashabiki mbalimbali waliofurika viunga vya Ngome Kongwe ndani ya Mambo Club Unguja, Zanzibar, katika usiku wa tamasha la 21, lililoanza leo Februari 9-11, 2024.

Selmor Mutukudzi ambaye alipanda jukwaani na bendi yake, aliweza kuanza na vionjo vya nyimbo maarufu za Baba yake ikiwemo‘Neria’ na Todii’ ambavyo viliamasha hisia za mashabiki wengi waliolipuka kwa shangwe na kuimba nae pamoja.

Kando ya jukwaa hilo, awali, Selmor Mutukudzi amesema kuwa, ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kushiriki tamasha la Sauti za Busara ambapo amekuwa akituma maombi ya kushiriki ila akikosa nafasi.

‘’Nimekuwa, nikiomba kushiriki Sauti za Busara, muda mrefu ila nikikosa nafasi. Nashukuru kwa mwaka huu kwani imenipa hali kubwa ya kuonesha owezo wangu.

Selmor Mutukudzi kipaji chake kilioneka tokea akiwa na miaka 10, baada ya baba yake kumuingiza kwenye muziki na kuonesha nyota yake ambapo akaweza kuwa na nyimbo mbalimbali ikiwemo Albamu aliyoipa jina la ‘Shungu’ aliyoitoa mwaka 2008 huku ikiwa na nyimbo kama Chiro,Iwewe, Neni, Shungu na kibao cha Handiende.

Hadi sasa ameweza kufikisha Albamu Sita ambazo zikiwa na nyimbo mbalimbali, aidha mbali ya muziki pia ni mwanaharakati wa utetezi wa mabinti wa kike na hata kuungana kuimba wimbo wa ‘’Strong Girls’’ ikiwa ni harakati za kutetea mabinti hao Afrika.
Burudani ikiendelea...
Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe kulia akikabidhi vifaa vya Tehama wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Mark Tanda akifuatiwa na Mratibu wa GIZ Apolinary Primus
Sehemu ya Vifaa hivyo

Na Oscar Assenga, KOROGWE.

Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limetoa msaada wa vifaa vya tehama katika Hospitali ya Mji wa Korogwe ya Manundu na kuweka miundombinu ya Intaneti,Ufugaji wa Mfumo wa kieletroniki ambao ni mfumo wa taarifa za usimamizi wa Hospitali za Serikali ya Tanzania (GoTHOMIS) pamoja na kufanya mafunzo endelevu kwa watumishi.

Ambapo hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 150 katika hospitali ya Korogwe tayari wamefundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa GoTHOMIS ambapo uwekezaji wake wa awali umegharimu Milioni 200,000,000 uliofanywa na GIZ hadi sasa na msaada zaidi ya kuifundi umepangwa ili kuhakikisha lengo linafikiwa ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza wvakati wa makabidhiano rasmi ya vifaa vya Tehama, Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe amesema kuwa mpango huo unalenga kubadilisha taratibu za kiutawala na kiafya katika hospitali hii kwa kuondoa matumizi ya kumbukumbu za karatasi, kuboresha uhifadhi na upatikanaji wa takwimu za wagonjwa, kuongeza hospitali ufanisi na kupunguza makosa katika takwimu.

Alisema kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani ambao ni wafadhili wao lakini pia wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wadau kwa mkoa wa Tanga kwa miaka tisa kwa awamu ya miaka mitatu mitatu.

Msoffe alisema kuwa mara nying wamekuwa kwenye awamu uliyoanza mwaka 2023 na itakwenda mpaka 2026 kwa mkoa wa Tanga na wana jumla ya Hospoitali 18 wanazozisaidia lakini katika eneo la Tehama pamoja na kwamba huyko nyumba wamefanya kazi na Hospitali nne kwenye eneo hilo lakioni watawasapoto kuweka miunbdombi na kuwafanya mafunzo watumishi waweze kuutumia.

“Kwanini tupo Korogwe kuhakikisha sisi kama wadau na Serikali ikiwemo Hospitali wanaweza kufanya juhudi za kipekee kuona ni gharama gani zinahitajika ili kuitoa Hospitali ya wilaya kutoka kwenye matumiz ya mifumo ya katarasi na kwenda katika asilimia 100 ya matumizi ya Kiletroniki”Alisema

Alisema katika mafanikio yatakayopatikana katika hospitali ya Korogwe, yatatumiwa na serikali ya Tanzania kuongeza mageuzi haya ya kidijitali kwa hospitali nyingine chini Tanzania.

“GIZ inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya kisera na kutoa msaada wa kitaalamu katika kuboresha huduma za afya chini Tanzania”Alisema.

Alisema maboresho hayo yanayoendelea katika mifumo ya kidigitali na hasa mfumo wa GOTHOMIS ambao ni moja ya mifano tosha ya dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kusaidia vituo vya afya kuboresha huduma za afya kupitia teknolojia ya kidijitali.

Hatua hiyo ni moja ya mambo ya msingi ya kuongeza ufanisi Hospitali ya Mji wa Korogwe inatangaza kwa fahari uamuzi wake wa kuachana na mifumo inayotumia makaratasi kabisa. Hospitali hiyo inakumbatia manufaa ya teknolojia katika kuimarisha huduma za afya na kurahisisha shughuli mbali mbali.

Uamuzi huo umekuja baada ya ongozi na wafanyakazi kutambua changamoto zinazoendelea kukabili mfumo wetu wa huduma za afya zikiwemo uhaba wa watumishi, kazi kubwa inayowakabili watumishi kwa kujaza karatasi nyingi, takwim duni lakini pia muda mrefu ambao wagonjwa hukaa hospitalini kupata huduma.

Kwa hiyo hospitali ya Korogwe imejitolea kutumia maendeleo ya kidijitali ili kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wake. Kuachana na matumizi ya makaratasi na kuharnia mifumo ya kidigitali ni tatua muhim katika kufikia lengo hili.

Deutsche Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kupitia mpango wake wa afya wa Kuboresha Huduma ya Afya Tanzania (ICP) ni mshirika wa muda mrefu na wamekuwa wakisaidia mkoa wa Tanga na haswa hospitali ya Korogwe kutekeleza afua za afya za kidijitali ambazo zinalenga kuongeza fanisi na ubora wa huduma za afya.

Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mji wa Korogwe Dkt Heri Kilwale alisema kuwa kubadilika kutoka matumizi ya karatasi na kutumia mifumo ya kidijitali itawasaidia watoa huduma za afya kuweza kupata taarifa za mgonjwa kwa wakati na salama.

Alisema pia kutapunguza muda ambao wafanyakazi hutumia kufanya kazi za kujaza makaratasi mengi na hivyo wataalamu wa afya wataelekeza zaidi muda katika kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa.

Korogwe ni miongoni mwa hospitali chache ambazo zimeanza kutumia toleo jipya la GoTHOMIS na kva msaada wa mara kwa mara kutoka kwa serikali, ongozi wa hospitali na washirika wa maendeleo, inatarajiwa kuwa hospitali ya Korogwe itafanikiwa katika dhamira yake ya mabadiliko kutoka matumizi ya karatasi Kwenda katika mifumo ya huduma za kidijitali na kwamba. Serikali itapanua msaada huo kwa hospitali zingine baada ya hapo.