Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki na mjasiriamali maarufu, Gigy Money, amesema tayari ameolewa kwa muda sasa lakini ameamua kuweka ndoa yake faraghani ili kulinda mahusiano yake dhidi ya changamoto za hadharani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Gigy alisema kuwa watu wamezoea kumuona kwenye mahusiano mbalimbali, lakini safari hii amechagua utulivu na maisha ya kifamilia bila kelele za mitandaoni. Alisisitiza kuwa mambo mazuri yanahitaji kulindwa, akifananisha ndoa na kitu cha thamani ambacho kikifichwa hudumu zaidi kuliko kinapowekwa wazi kwa kila mtu.

Msanii huyo pia alieleza kuwa baada ya kuolewa amebadili mwenendo wa maisha, akisema sasa ameanza ukurasa mpya wa utulivu na kujitambua zaidi. Aidha, alibainisha kuwa amepewa jina jipya la Rahuya na mume wake, jambo alilolipokea kwa furaha kama ishara ya mwanzo wa maisha mapya.

Gigy alimalizia kwa kusema anachotamani zaidi kwa sasa ni amani ya moyo na ndoa yenye utulivu, akieleza kuwa amechoka kupitia misukosuko ya mahusiano ya zamani na sasa anatafuta maisha ya kudumu na yenye heshima.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: