Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Accattino, amewasili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo na kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Polycarp Kardinali Pengo kilichotokea Februari 19, 2026.

Katika ziara hiyo ya maombolezo, balozi huyo alitoa pole kwa Thaddaeus Ruwa'ichi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, pamoja na Kanisa Katoliki nchini na waumini wote walioguswa na msiba huo mkubwa.

Balozi Accattino alipokelewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Henry Mchamungu, aliyemkaribisha na kumshukuru kwa kuonesha mshikamano wa kiroho na kidiplomasia katika kipindi hiki cha majonzi kwa Kanisa na Taifa.
Akizungumza kwa ufupi baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, balozi huyo alieleza kuwa Kardinali Pengo alikuwa kiongozi wa kiroho mwenye mchango mkubwa katika kulijenga Kanisa na Taifa, akisisitiza kuwa urithi wake utaendelea kuishi katika mioyo ya waumini na jamii kwa ujumla.

Ibada za kumuombea marehemu zinaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini huku waumini wakiendelea kuungana katika sala, wakimuombea apumzike kwa amani ya milele.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: