Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughle, ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na Watanzania kwa ujumla katika kuomboleza kifo cha Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, marehemu Polycarp Cardinal Pengo.Diwani Choughle alifika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, lililopo Kata ya Kivukoni, ambapo alitoa salamu za pole na kusaini kitabu cha maombolezo kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, alisema kuwa msiba huo si wa Kanisa Katoliki pekee bali ni wa taifa zima, akieleza kuwa Kardinali Pengo alikuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika masuala ya kiroho, maadili na mshikamano wa jamii.
Aidha, alimpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddeus Ruwa’ichi, pamoja na viongozi na waumini wote wa Kanisa Katoliki, akiwataka Watanzania kuendelea kumuombea marehemu ili Mungu amlaze mahala pema peponi.





Toa Maoni Yako:
0 comments: