Mjasiriamali na mfugaji wa kuku kutoka Mapinga, Bagamoyo, Raphael Emmanuel, amejishindia pikipiki kupitia promosheni ya “Shinda Boda” inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya PigaBet.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya zawadi hiyo yaliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Raphael alimshukuru Mungu pamoja na PigaBet kwa kumpatia fursa hiyo akisema ushindi huo utamsaidia kupunguza changamoto za usafiri na kufungua milango ya mafanikio katika shughuli zake za kiuchumi.
“Pikipiki hii itanirahisishia maisha, hasa katika usafiri wa kila siku. Nimekuwa nikitumia gharama kubwa kusafiri, hivyo zawadi hii ni msaada mkubwa kwangu,” alisema Raphael, ambaye anaishi Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa PigaBet, Hemed Msonge, alisema kampuni hiyo imeanza rasmi mpango wa kuwainua Watanzania kiuchumi kupitia zawadi za pikipiki mbili zitakazotolewa kila wiki kwa muda wa wiki sita mfululizo.
Alisema promosheni hiyo inalenga kuwapa washiriki fursa ya kujiongezea kipato kupitia shughuli za usafiri wa bodaboda, huku akisisitiza umuhimu wa kushiriki michezo kwa uwajibikaji.
Msonge aliwahimiza Watanzania wengi zaidi kushiriki promosheni hiyo, akieleza kuwa droo zitaendelea kufanyika kila wiki hadi mwisho wa kampeni, huku akisisitiza kaulimbiu ya kampeni hiyo kuwa ni “Cheza, shinda bodaboda na ubadilishe maisha yako.”





Toa Maoni Yako:
0 comments: