Articles by "MUZIKI"
Showing posts with label MUZIKI. Show all posts
Wanamuziki waliokuwa wakiunda kundi la Akudo Impact wameandaa Tamasha la Pamoja litakaloitwa  Akudo Impact Reunion litakalofanyika Desemba 23, 2023 ndani ya Kibozote Pub, Mbezi Malamba Mawili - Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jode Musica na Kibozone Pub, Bw. Denis Mutegeki amesema kuwa wakati umefika wa kuwapa wapenzi w dansi burudani ambayo wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu.

"Tumeandaa Tamasha hilo ili kuweza kuwapa wapenzi wa dansi burudani ya uhakika ambayo wamekuwa wakiikosa kwa muda mtefu kwa vile hao wanamuziki ni mara chache sana kuwakuta pamoja kwa vile kwa sasa wamekuwa wanapiga katika bendi zao," amesema Mkurugenzi Mutegeki.

Amesema kuwa wanamuziki hao watatoa burudani kwa muda wa saa 5 bila kupumzika kwa vile wananyimbo nyingi za kutosha.

Kwa upande wake Mwanamuziki Tarsiss Masela amewakaribisha wapenzi wa muziki wa dansi kujumuika nao katika Tamasha.

Ameongeza kuwa Akudo Impact Reunion itawajumuisha wanamuziki wote waliounda kundi la Akudo Impact wakati huo akiwemo yeye mwenyewe Tarsiss Masela, Christian Bella, Fabric Kulialia, Zagreb pamoja na Katoto Maya.

Tamasha hilo limeandaliwa na Kibozone Pub.

  Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone amewasili nchini Tanzania kwaajili ya kutumbuiza katika Tamasha kubwa la 'SERENGETI LITE OKTOBA FEST', litakalofanyika  Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Mapokezi hayo yaliyopambwa na Kinywaji cha Serengeti LITE kiliweza kuonyesha umahili wake baada ya msanii huyo kupewa na kuonyesha alama ya upendo.
Tamasha la "SERENGETI LITE OKTOBA FEST" litajumuisha wasanii lukuki kutoka hapa Nchini Tanzania wakiongozwa na Alikiba, billinas, Chino kidd, Gnako na Msanii kutoka nchini kenya Nyamari ongegu "Nyashiski pamoja na Jose Chameleone.
Msanii wa Kenya Nyashiski amefurahi kuja kutumbuiza Jukwaa moja na msanii wa Tanzania, AliKiba maana itamfungulia milango ya kufanyakazi ya muziki na wasanii wa Tanzania.
Akizungumzia mara baada ya kuwasili leo jijini Dar es Salaam Msanii Nyashinski amesema kuwa kupata nafasi ya kutumbuiza jukwaa moja na wasanii mbalimbali wakubwa nchini Tanzania kama Alikiba ni jambo zuri ambalo litasaidia kufungua milango ya kufanya kazi na wasanii wa hapa kwa sababu ni matamanio makubwa kwa kila wanamuziki wa Kenya.
"Kwasasa wasanii wa Tanzania wamekuwa na majina makubwa na hata kupelekea mziki kwenda mbali zaidi, sasa hii fursa niliyoipata itafungua milango kwangu na kunifanya kuwa nao karibu," amesema Nyashiski.

Msanii maarufu nchini Kenya Nyamari Ongegu "Nyashinski" amewasili Tanzania kwa ajili ya tukio kubwa lililoandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti "OKTOBA FEST" ambalo litafanyika Oktoba 21, 2023 Coco Beach Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo la "SERENGETI LITE OKTOBA FEST" litajumuisha wasanii lukuki kutoka hapa Nchini Tanzania wakiongozwa na Alikiba, billinas, Chino kidd, Gnako na Msanii kutoka nchini Uganda Jose Chameleon.
Meneja wa Club Benbistro Hamisi Hassan akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu walivyojipanga kuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 kwa staili ya aina yake ikiwemo kuwashukuru wateja wao kushoto ni Marton wa Club hiyo Sarah Patrick
Meneja wa Club Benbistro Hamisi Hassan akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu walivyojipanga kuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 kwa staili ya aina yake ikiwemo kuwashukuru wateja wao kushoto ni Marton wa Club hiyo Sarah Patrick
Marton wa Club hiyo Sarah Patrick akizungumza namna walivyojipanga kushoto ni Msimamizi wa Club hiyo Silvester Kasembe
Marton wa Club hiyo Sarah Patrick akizungumza namna walivyojipanga kushoto ni Msimamizi wa Club hiyo Silvester Kasembe
Msimamizi wa Club Ben Bistro Lounge Silvester Kasembe

Na Oscar Assenga,Tanga.
MADJS Maarufu kutoka Jijini Dar es Salaam na wakishirikiana na wenyeji wa Jiji la Tanga wanatarajia kuuwasha moto Club Maarufu Jijini Tanga “BEN BISTRO” siku ya mkesha wa kuuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 kwa staili ya aina yake ikiwemo kuwashukuru wateja wao

Akizungumza leo na waandishi wa Habari Jijini Tanga Meneja wa Benbistro Hamisi Hassan alisema kwamba burudani hizo zitaanza siku ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka 2023 na wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wateja wao wanapata burudani kali.

Alisema kwamba Pamoja na uwepo wa burudani hizo lakini wanawashukuru wateja na wadau wao tokea walipoanza mpaka sasa na kikubwa wamejiandaa kikamilifu na vitu ni vingi upande wa jikoni na club huku akieleza watahakikisha pia usalama unaimarishwa lengo kuwawezesha wadau wao na wateja kusheherekea mwaka mpya

“Kikubwa ni shukrani kwa wateja wetu na wadau wanaotusapoti tokea tumeanza mpaka sasa na tunawaambia mkesha wa Jumamosi na Jumampili kutokuwa na burudani kutoka kwa madjs kutoka Dar na tunaufunga mwaka “Alisema

Aidha alisema kwamba wanawahaidia wateja wao kuendelea kuboresha huduma zao ikiwemo kuhakikisha suala la usalama wao linaendelea kuwepo kila wakati na muda wote.

Awali akizungumza Mdau wa Club Benbistro Kamafa Forever alisema kwamba uwepo wa Club hiyo ambayo imekuwa tofauti na zile za awali umewasaidia wapenda burudani Jijini Tanga kupata ladha za uhakika ambazo hapo awali walikuwa wakizikosa

“Kinachofanyika Club Benibistro ni spesho sana na sehemu nzuri ambayo wadau wa burudani wataendea kupata burudani ya kuufunga mwaka na sababu za kupeleka uwepo wa madjs wapya ni kupata ladha tofauti ambazo zitakuwa na vionjo vya aina yake “Alisema

Naye kwa upande wake Matron wa Club hiyo Sarah Patrick alisema kwamba upande wa huduma ipo vizuri sana na wamejipanga kuhakikisha wanawahudumia wateja wao kama ilivyokuwa kawaida na kuhakikisha hakuna mtu ambaye anakosa vinywaji kutokana na aina ya wahudumu wachangamfu waliopo.

Hata hivyo msimamizi wa Club hiyo Silvester Kasembe alisema kwamba mwaka 2023 wanatarajia kufanya mambo makubwa Zaidi na sehemu hiyo ni nzuri ya Kwenda kupata burudani hivyo wanawakaribisha wateja wao kutoka ndani na nje ya Jiji la Tanga.
Following a successful debut in 2021 that saw Kenah release an EP ‘3:05 Musing’ and a series of hit singles, the rising Nigerian born star has today released her second EP titled ‘UNCOVER’, with the lead track “Mind” featuring one of the UK’s most exciting new talents, Amaria BB.

Watch “Foreigner” on YouTube: https://www.youtube.com/watch?v=4vXFE7lZBL4

‘Uncover’ can be described as a celebration of soothing vocals, mixed sounds, sultry lyricism and versatility, littered with sweet R&B tones, steady Afrobeat groves, Amapiano vibes, groovy trap and infectious synergy, it’s safe to safe there’s definitely something in ‘Uncover’ for everyone. With production credits by top producers like Krizbeatz, Killertunes and fast rising producer Hulla, the EP boost a blend of great beats, rhythmic percussion, heart piercing piano chords, soulful backing melodies and emotive synths, which provokes Kenah to deliver something equally as beautiful on every track.

Having made an exceptional introduction to the music world, Kenah has claimed a space of her own thanks to her soft, gliding vocals that sit as a hybrid of her choral experiences and the art of rap. Daringly bold and energetic as it is smooth and sensual, Kenah’s sound has an elegance and rarity to it that is refreshingly unique, seeing her supported with music gatekeepers including DJ Edu, Adesope Olajide, Jeremiah and DJ Davda. bringing Kenah into a whole new world of discovery.

Demonstrating her unique prowess and divine musical qualities, Kenah delivers ‘UNCOVER’ the EP.
Programu inayoongoza kwa upakuaji wa muziki katika bara la Afrika, Mdundo imezindua chapa mpya ya ‘Mdundo Brand Lift’ ambayo itawawezesha kuendelea kujitangaza zaidi katika tasnia ya muziki.

Huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa watangazaji, katika huduma ya Mdundo Lift, itakuwa pia inatoa vipimo vinne muhimu vya chapa ambavyo ni uhamasishaji, kuzingatia, kupendekeza na manunuzi kwa jamii ambapo itafikisha taarifa kwa wakati katika tovuti ya www.mdundoforbrands.com.

Uzinduzi wa chapa hiyo umekuja miezi kadhaa baada ya Mdundo kutangaza kuwa iliwaingiza katika rekodi watumiaji hai milioni 31 Afrika nzima katika robo ya kwanza ya mwaka 2022, ikiwa ni ukuaji wa 49% ikilinganishwa na robo iliyopita.

Mkuu wa Biashara ya Ubia barani Afrika wa Mdundo, Rachel Karanu alisema kuwa chapa hiyo ni kipimo ambacho kitawawezesha washiriki wake kufanya maamuzi kulingana na ufahamu wa wateja unaotokana na utafiti walioufanya hadi sasa.

"Tumewekeza katika sehemu kubwa ya umiliki wa chapa hii, ili kuhakikisha inasaidia watangazaji kupima utendaji kazi kwa kupitia mashindano baina yao ambapo kuna watumiaji zaidi ya milioni 33 Afrika nzima kwa utoaji huduma wa yetu zetu kupitia mtandao na intaneti. Chombo hiki hutoa maarifa kwa wakati muafaka na kwa wale wanaotaka kujiongezea kipato na uwekezaji,” alisema.

Aliongeza, Mdundo inakuwa kwa kasi zaidi kwa kutoa huduma ya upakuaji wa muziki na kwa urahisi Afrika, imekuwa ikiwarahisishia watangazaji na watumiaji wa muziki kupata huduma wanazozitaka kwa muda mwafaka.

Mdundo iliyoanzishwa mwaka 2013, imesharuhusu watumiaji wa simu mahiri kupata zaidi ya nyimbo milioni 1.9 kutoka kwa wasanii 100,000 barani Afrika bila malipo. Huduma hiyo imekuwa ikitoa huduma halali ya muziki japokuwa kuna tatizo la baadhi ya watu kupakua muziki kwa na kuutumia kinyume na utaratibu.
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi (kushoto) akiwa pamoja na msanii mkongwe wa kizazi kipya Faridi kubanda (FID Q) wakionesha nembo ya Tamasha la Muziki la Serengeti la 2022 ambalo litafanyika mwezi Machi mwaka huu jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akieleza mikakati ya uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 11,2022 katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam

Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda (FID Q) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam

Mkutano wa Waandishi habari ukiendelea wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo adhimu litakalofanyika Mwezi Machi jijini Dodoma. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Na John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi leo Februari 11, 2022 amezindua Tamasha la Muziki la Serengeti la mwaka huu jijini Dar.

Akizindua Tamasha hilo mbele ya Waandishi wa Habari, Dkt. Abbasi amesema tamasha la mwaka huu linakusudia kutangaza Utamaduni na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

Aidha amesema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya wasanii 50 na litashirikisha wasanii wa lebo zote.

Ameongeza kuwa wasanii wakongwe na wachanga watashiriki ili kuleta ladha tofauti tofauti.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Fareed Kubanda amepongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatumia wasanii kutangaza miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Serikali ya Tanzania ndiyo Serikali pekee duniani ambayo inawatumia zaidi wasanii katika utekelezaji wa kazi za Serikali". Amefafanua Kubanda

#MADEINTANZANIA
Aggy Baby
Malkia kwenye muziki wa Bongo fleva Agness Suleiman maarufu Aggy Baby anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya wa Kamnyweso aliomshirikisha msanii Stompion.
Apple Music launches its Spirits Rejoice campaign, which celebrates the best and brightest Gospel voices with exclusive playlists from South Africa’s Joyous Celebration, Ntokozo Mbambo, Hle and Dr. Tumi, as well as Nigeria’s Sinach, Mercy Chinwo, Nathaniel Bassey, Tim Godfrey and Ada Ehi. The music selections seek to inspire, uplift and encourage, with a whole host of local and international artists including Fred Hammond, Kirk Franklin and Donald Lawrence.

As one of the top-streaming genres on the African continent, Gospel music is characterised by emotion, choral voices and soulful sound that conveys a range of emotions that move the listener with every note. Gospel music has its roots firmly in Africa with its call-and-response style originating from numerous African tribes.

Black gospel, Southern gospel, country gospel music, Bluegrass gospel, Celtic gospel and British black gospel have each developed their own style and characteristics over the years anchored in celebration. On the other side of the world, African Gospel has become one of the most popular genres on the continent over the last few decades, specifically in South Africa, Ghana and Nigeria.

African gospel is uplifting, rhythmic, and spiritual with lyrics that reflect diverse world views, theologies, cultures and experiences of Africans from all backgrounds. This is highlighted by the exclusive artist playlists created for Spirits Rejoice.

Join Apple Music and celebrate this Easter season alongside Africa’s most inspiring gospel artists. http://apple.co/SpiritsRejoiceRoom

Katibu Mkuu wa Umoja Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) , Stella Joel

Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) wametoa salamu za rambi rambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021katika Hospitali ya Mzela jijini Dar es Salaam.

Salamu hizo za rambi rambi pia wamezitoa kwa Waziri Mkuu, viongozi mbalimbali, mjane wa marehemu Janeth Magufuli ,Rais wa Zanzibar na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema kifo cha Rais Magufuli wamekipokea kwa mshituko mkubwa na kuwa watamkumbuka milele daima.

"Tunamshukuruaa Mungu kwa ajili ya maisha ya Rais Magufuli ambaye katika uongozi wake aliinua Tasinia ya Muziki kwa kuwasaidia wasanii kwa kutatua changamoto zao mbalimbali" alisema Joel.

Alisema Rais Magufuli alifanikiwa kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kwa kuwa jali wanamuziki hao upande wa kiafya kwa Kuwapatia Bima ya Afya ya NHIF kwa gharama nafuu kwa ajili ya vipimo na matibabu katika Hospitali za Serikali na za Binafsi.

Joel alisema alikuwa katika maandalizi ya kufanya maboresho mengi ili wanamuziki waweze Kufaidika na kazi zao.

" Hakika tutamkumbuka Magufuli kwa mema mengi aliyoyafanya enzi za uhai wake kama Rais wa Tanzania"alisema Joel.

Stella alisema kwa niaba ya TAMUFO ana mpongeza Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa wana amini atayaendeleza yale yote ambayo Hayati Rais Magufuli aliyokuwa ameyaanzisha ambapo wanatambua kwamba kazi hiyo walishirikiana Pamoja.

" Tunakuombea Rais Mama Samia Mungu awe pamoja naye katika kutekeleza yale yote na sisi wanamuziki tumepokea kwa furaha kwa kuapishwa na kuwa Rais wa kwanza Mwanamke katika nchi yetu." alisema Joel.
East Africa, 12 March 2021: In celebration of his new album, The 4th Republic, Apple Music has announced prolific producer and house DJ Prince Kaybee as the next Isgubhu cover star. Prince Kaybee’s takeover of the playlist includes a premier selection of dance music from all over Africa with homegrown talent Black Motion, Caiiro, Sculptured Music and Chymamusique, as well as Nigerian artists Olamide and Niniola amongst a host of others.

“It is an honour to be featured as this month’s Isgubhu hero artist, especially considering that the playlist represents the culture of house music.” - Prince Kaybee.

Launched last month, Isgubhu is the definitive home of African Dance and Electronic music on Apple Music and spotlights and elevates the work of African Electronic DJs, producers and creatives. Isgubhu, a Zulu word meaning beat and used to refer to a banging song, pays homage to an evergreen set of genres and the African artists who have played a pivotal role in shaping the Dance and Electronic scene across the world.

Taking over Isgubhu By… this month is DJ, radio presenter and label owner, Kid Fonque, in celebration of his new album with UK DJ and longtime collaborator, Jonny Miller, Connected.

“Here are my 16 electronic picks from South Africa's forward thinking producers, rappers & singers. These records have stood out to me over the past 20 years, albums that have and will continue to shape the South African underground electronic scene,” said Kid Fonque.

Isgubhu also houses a collection of playlists including Spotlight On - a focus on boutique labels like Soul Candi, House Afrika, Stay True Sounds and Uganda’s Hakuna Kulala & Nyege Nyege Tapes and Isgubhu Voices - a focus on the best Dance and Electronic tracks that feature vocals.

Listen to Isgubhu only on Apple Music http://apple.co/Isgubhu

For a limited time, new customers to Apple Music in Nigeria and South Africa on iOS and Android can enjoy all of this great content with 6 months of free Apple Music through the Shazam app. Returning customers get 3 months of free Apple Music.
 Stella Joel akitafakari ukuu wa Mungu baada ya kutoa wimbo huo ambao unabamba hivi sasa hapa nchini.

Na Dotto Mwaibale

BAADA ya kimya cha muda mrefu, Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Tanzania, Stella Joel ameachia wimbo wa kuhamasisha maendeleo unaoitwa Tanzania ya Maendeleo.

Mara ya mwisho Stella aliachia wimbo wa Hakuna Mwanamke mbaya alioshirikiana na malkia wa muziki wa Injili, Rose Muhando.

Stella ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) alisema, imefika hatua kwa wasanii kuhamasisha nyimbo zinazochochea maendeleo na kuisaidia jamii kutatua changamoto zake.

“Baada ya Tanzania kufikia uchumi wa kati nikaona ni vyema niweke hilo kwenye muziki, nyimbo za aina hii zinachangia sana kupiga hatua za kimaendeleo zaidi,” alisema Stella.

Stella aliwashauri wanamuziki nchini kubadilisha mtizamo wao, kutojikita kwenye  jumbe za mapenzi peke yake badala yake waangalie changamoto nyingi za kijamii kama masuala ya lishe, ukatili wa kijinsia na mengine.

*Mosha kujenga orodha ya wasanii na kuongeza kazi za kimataifa katika ukanda huo

*Mosha analeta miaka 15 aliyoikusanya katika masoko Afrika, muziki na uzoefu kwenye burudani katika kazi hiyo

East Africa, Disemba 16, 2020 – Sony Music Entertainment Africa imemteua Christine Mosha, anayejulikana zaidi kama ‘Seven’, kuongoza kitengo cha Masoko na Maendeleo ya Wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akianza kazi rasmi, Mosha atajenga orodha ya kampuni ya vipaji vya eneo hilo na kukuza kazi zake za kimataifa na zilizopo katika eneo hilo kutokea makazi yake nchini Tanzania. Ataripoti moja kwa moja kwa Sean Watson, Mkurugenzi Mtendaji, Sony Music Africa.

“Seven ametumia maisha yake mengi kuchangia katika tasnia ya burudani ya Afrika. Ni mtetezi mwenye mapenzi makubwa katika kila kitu ambacho Afrika Mashariki inaweza kuipa dunia,” amesema Sean Watson, Mkurugenzi Mtendaji, Sony Music Africa. “Kwa miaka kadhaa tayari amekuwa mshirika muhimu kwetu, akitupa utambuzi wa kipekee wa njia sahihi za kufanya kazi Afrika Mashariki, ambako ni kitovu chenye nguvu na kilichochangamka kwa muziki barani. Hivyo tumefurahi kuwa naye, akisaidia kupanua orodha yetu ya wasanii wa Afrika Mashariki na kuonesha mkusanyiko wetu wa kazi za kimataifa kwenye hadhira mpya.”

“Sony Music ina historia kubwa kwenye tasnia ya muziki duniani, kwahiyo kuwa sehemu ya kampuni hii katika wakati huu wa kazi yangu inaonekana ni toshelezo zuri ambapo nitaleta uzoefu na utalaamu wangu kibiashara kwenye kampuni nzima,” ameongeza Mosha. “Nimefurahia sana kuhusu kujiunga na Sony Music Africa, natazamia kuendelea kuleta matokeo chanya kwenye tasnia ya burudani, sio tu Afrika Mashariki bali katika bara zima.”

Mosha analeta uzoefu wa miaka 15 katika tasnia ya muziki ya Afrika katika kazi hiyo na amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Sony Music Africa kwa miaka mingi. Mwaka 2017 alianzisha lebo yake binafsi ya muziki na kampuni ya kusimamia vipaji, Rockstar Africa, ambako alichochea mafanikio kibiashara kwa wasanii wengi wa muziki wa Afrika Mashariki wakiwemo Lady Jaydee, Ray C, TID, Rose Muhando, Xtatic, Alikiba na Ommy Dimpoz. Tangu 2010, Mosha ameiongoza pia ROCKSTAR 4000 MUSIC ENTERTAINMENT, kampuni ya kwanza ya muziki ya Afrika inayojitegemea pamoja na mtandao wa utayarishaji wa maudhui, kidigitali na matukio.

Huko, alisimamia uchapishaji wa muziki, mikataba ya muziki na leseni za maudhui akiwa na Sony Music Africa, ikiwemo kufanya kazi kwenye kampeni kwaajili ya kombe la dunia la FIFA 2010 lililofanyika Afrika Kusini.

Mosha alianza kazi yake mwaka 2006 kama mtangazaji wa redio wa kipindi cha asubuhi, promota na gwiji wa masoko Clouds Media Group, shirika la habari linaloongoza Tanzania kabla ya kuhamia MTV mwaka 2005, ambako aliongoza kitengo cha wasanii na kazi pamoja na biashara barani Afrika, alizindua kituo cha MTV Base Tanzania, na akifanya kazi kwenye miradi ikiwemo Staying Alive Campaign akiwa na Kelly Rowland nchini Tanzania pamoja na ziara ya Water for Life iliyoshirikisha Umoja wa Mataifa, Clouds Media na Jay Z.

Katika miaka mitano iliyofuata hadi alipoanzisha Rockstar Africa, Mosha alikuza orodha ya kazi alizofanya kuwajumuisha wasanii kama Alikiba (Best African Act katika MTV Europe Music Awards mwaka 2016) na Ommy Dimpoz (Best Male East Africa katika tuzo za AFRIMA mwaka 2019), pamoja na watayarishaji wa muziki, wanamichezo na waigizaji.

 

Mtanzania ambaye unahitaji kufungua kituo cha Redio Nchini na unafikiria wapi pa kuchukua mzigo huo tafadhali  wasiliana nasi uweze kupata vifaa hivyo leo. 

VIFAA VYA STUDIO AMBAVYO VINAUZWA NI PAMOJA NA 
1. Mixer- njia 10
2. Microphone 3
3, stand mic 3
4. Headphones 3
5. Telex- kupiga simu 1
6. Audio Recorder 2
7.CD player( mp3& USB)
8. Power monitor 2
9. Tuner 1
10. Sign on AIR( taa) 1

KWA MAWASILIANO 0755373999


African pop diva Yemi Alade releases a new single & video. Titled TRUE LOVE, this single commands love and positivity. The Vtek produced tribal dance anthem serves as the second single for her forthcoming fifth studio album. Yemi comes blazing with her towering vocals and a pulsating guitar-driven instrumentation on this triumphant song preaching happiness, joy and dancing in the rain of true love.

Once again, Yemi delivers another spectacle with rich videography for the single.

Watch TRUE LOVE music video on YouTube: https://www.youtube.com/watch?v=XkgMHudaKdA


TRUE LOVE is a true African pop gem, and sets the throne for the successor of “Woman of Steel”. With the massive success of her urban-influenced hit BOYZ released three months ago, the video has already garnered over 2 million views on YouTube. Yemi’s upcoming fifth studio album is still in the works and slated for a 2020 release. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza akimsisitiza msanii wa bongofleva Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz kufanya kazi kwa bidii na kuwa mbunifu huku akimhakikishia kuwa serikali ipo tayari kumpa ushirikiano alipokuwa akifanya kikao nae leo jijini Dodoma.
Msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz akimweleza Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza (kulia) kuwa mapema wiki ijayo anatarajia kutoa video ya wimbo wake wa Beautiful na pia atatunga wimbo wa kuhusu Corona katika kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza akiwa akimsisitiza msanii wa bongofleva Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz kuwa wizara ipo tayari kumpa ushirikiano wakati wowote na kikubwa ni msanii huyo kujituma na kuonyesha umma kweli ameachana na matumizi ya madawa ya kulevya mara baada ya kikao leo jijini Dodoma. 

Na Anitha Jonas – WHUSM.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amwaahidi ushirikiano msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu Chidbenz.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipofanya kikao na msanii huyo ambapo Chid benz alimuhakikishia kuwa kwa sasa amebadilika na anataka kuwaonyesha watanzania amefanikiwa kujikwamua katika matumizi ya madawa ya kulevya na hataki tena kurudi huko kwani anazaidi ya miezi mitatu sasa hajatumia madawa hayo kabisa.

“Kati ya wasanii wenye kukubalika na mashabiki zao wewe Chid benz ni mmoja wao na mashabiki zako ni wengi hivyo ningependa kukuona kwanzia sasa unalijenga zaidi jina lako kwa kuonyesha kuwa umebadilika,katika kipindi hichi nitafurahi zaidi kukuona unasonga mbele na hurudi tena katika matumizi ya madawa ya kulevya wizara ipo pamoja na wewe kukusaidia wakati wowote ,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho mheshimiwa Shonza alimsisitiza msanii huyo kuwaonyesha watanzania kuwa anaweza na hata akipewa nafasi anaweza kujitumia vyema na kuonyesha juhudi yake katika kufanya kazi na kuwa mbunifu katika kufanya kazi zake za usanii.

Naye Msanii huyo wa Bongofleva Chid benz alieleza kuwa kwa sasa hautarudi nyuma tena sababu tayari amekwisha acha kutumia matumizi ya madawa hayo na ninaelewa bahati haiji mara mbili lakini kwangu naiona imekuja zaidi ya mara moja kwa maana ya kuwa nimekuwa nimekuwa na anguka nainuka narudi kwa mashabiki wananipokea nakuendelea kukubali muziki wangu hakika najiona niwakati wa kuwafurahisha zaidi mashabiki na sitawaangusha.

“Ombi langu kwa serikali ni kupata ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao Beautiful ambao nimeuiamba nikisifu uzuri wa mwanamke na kufuatia janga la Corona ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili ya Corona ,”Chid benz. 

Pamoja na hayo nae Chid benz alitoa wito kwa watanzania kuacha kufanya mzaha katika mitandao ya jamii kuhusu suala la ugongwa Corona sababu hili ni tatizo ni janga linalosumbua dunia kwa sasa hivyo jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kutoka kwa wataalamu wa afya.
Mwimbaji wa Muziki wa Dansi Mwinjuma Muumini (Kocha) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha bendi yake mpya iitwayo Sadai sambamba na wanamuziki wa bendi hiyo.
 Rapa wa muziki wa Dansi Fugerson akizungumza machache wakati wa utambulisho.
Mwimbaji wa muziki wa dansi Mubela akitoa kionjo.
Mwimbaji wa muziki wa dansi Rama Pentagon akitoa kionjo.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mwimbaji wa Muziki wa Dansi Mwinjuma Muumini (Kocha) ametambulisha bendi yake mpya iitwayo Shadai wana Tikisa Tikisa yenye makazi yake Bagamoyo, Pwani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwanamuziki Mwinjima amesema kuwa bendi yao ni mpya na imeweza kusajili wanamuziki tofauti toka bendi mbali mbali.

'Nimekaa nikajipanga nimekuja upya na bendi yangu baada ya ukimya wa muda mrefu mno hivyo naomba Watanzania mnipokee kwa mikono miwili,' amesema Mwimbaji Muumini Mwinjuma.

Aliongeza kuwa kwa kipindi chote ambacho amekuwa akijinoa na bendi yake mpya ya Shadai na kuingia studio kufanikiwa kurekodi albamu aliyoipatia jina la 'Nimefulia'.

Ujio wangu huu wa Nimefulia umeweza kunishusha cheo changu na wale wote waliozoea kunitambua Muumini Mwinjuma a.k.a Kocha Wa Dunia nimeliondoa na kwa sasa niite Kocha tu.

Amesema kuwa bendi ya Sadai inatarajiwa kuzinduliwa jijini Dodoma mwishoni mwa mwezi huu katika Ukumbi wa 4G ambapo bendi ya Gold, bendi ya Sky na Bendi na Badi Bakule, mpaka sasa wameshaandaa Albabu ya Nimefulia iliyobeba nyimbo 8, ikiwemo Nimefulia, Nitumbue, Alikasusu, Mwanadamu Halidhiki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy ( kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya msanii huyo iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy ( kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya msanii huyo iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia)akisoma moja ya vyeti vya usajili wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya Msanii mziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti usajili toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019, kushoto ni Afisa Sanaa toka BASATA, Bi. Bona Masenge.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akiwakabidhi vyeti vya usajili toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wasanii wa Hightable Studio wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio inayomilikiwa na Msanii wa mziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy mapema hii leo Julai 17, 2019.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akikagua vyeti usajili toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy (kulia) iitwayo Hightable Studio mapema hii leo Julai 17, 2019.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya msanii huyo iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Hightable Studio wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio inayomilikiwa na Msanii wa mziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy mapema hii leo Julai 17, 2019.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akipokea moja ya albamu ya Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy (kulia) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya msanii huyo iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019. Picha na WHUSM - DSM.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akikaribishwa na mwenyeji wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Barnaba Elias maarufu kama Barnaba Boy wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua rasmi studio ya msanii huyo iitwayo Hightable Studio na kukabidhi vyeti toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema hii leo Julai 17, 2019.