Na John Mapepele
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi leo Februari 11, 2022 amezindua Tamasha la Muziki la Serengeti la mwaka huu jijini Dar.
Akizindua Tamasha hilo mbele ya Waandishi wa Habari, Dkt. Abbasi amesema tamasha la mwaka huu linakusudia kutangaza Utamaduni na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.
Aidha amesema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya wasanii 50 na litashirikisha wasanii wa lebo zote.
Ameongeza kuwa wasanii wakongwe na wachanga watashiriki ili kuleta ladha tofauti tofauti.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Fareed Kubanda amepongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatumia wasanii kutangaza miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Serikali ya Tanzania ndiyo Serikali pekee duniani ambayo inawatumia zaidi wasanii katika utekelezaji wa kazi za Serikali". Amefafanua Kubanda
#MADEINTANZANIA
Toa Maoni Yako:
0 comments: