Programu inayoongoza kwa upakuaji wa muziki katika bara la Afrika, Mdundo imezindua chapa mpya ya ‘Mdundo Brand Lift’ ambayo itawawezesha kuendelea kujitangaza zaidi katika tasnia ya muziki.
Huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa watangazaji, katika huduma ya Mdundo Lift, itakuwa pia inatoa vipimo vinne muhimu vya chapa ambavyo ni uhamasishaji, kuzingatia, kupendekeza na manunuzi kwa jamii ambapo itafikisha taarifa kwa wakati katika tovuti ya www.mdundoforbrands.com.
Uzinduzi wa chapa hiyo umekuja miezi kadhaa baada ya Mdundo kutangaza kuwa iliwaingiza katika rekodi watumiaji hai milioni 31 Afrika nzima katika robo ya kwanza ya mwaka 2022, ikiwa ni ukuaji wa 49% ikilinganishwa na robo iliyopita.
Mkuu wa Biashara ya Ubia barani Afrika wa Mdundo, Rachel Karanu alisema kuwa chapa hiyo ni kipimo ambacho kitawawezesha washiriki wake kufanya maamuzi kulingana na ufahamu wa wateja unaotokana na utafiti walioufanya hadi sasa.
"Tumewekeza katika sehemu kubwa ya umiliki wa chapa hii, ili kuhakikisha inasaidia watangazaji kupima utendaji kazi kwa kupitia mashindano baina yao ambapo kuna watumiaji zaidi ya milioni 33 Afrika nzima kwa utoaji huduma wa yetu zetu kupitia mtandao na intaneti. Chombo hiki hutoa maarifa kwa wakati muafaka na kwa wale wanaotaka kujiongezea kipato na uwekezaji,” alisema.
Aliongeza, Mdundo inakuwa kwa kasi zaidi kwa kutoa huduma ya upakuaji wa muziki na kwa urahisi Afrika, imekuwa ikiwarahisishia watangazaji na watumiaji wa muziki kupata huduma wanazozitaka kwa muda mwafaka.
Mdundo iliyoanzishwa mwaka 2013, imesharuhusu watumiaji wa simu mahiri kupata zaidi ya nyimbo milioni 1.9 kutoka kwa wasanii 100,000 barani Afrika bila malipo. Huduma hiyo imekuwa ikitoa huduma halali ya muziki japokuwa kuna tatizo la baadhi ya watu kupakua muziki kwa na kuutumia kinyume na utaratibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: