Msanii wa Kenya Nyashiski amefurahi kuja kutumbuiza Jukwaa moja na msanii wa Tanzania, AliKiba maana itamfungulia milango ya kufanyakazi ya muziki na wasanii wa Tanzania.
Akizungumzia mara baada ya kuwasili leo jijini Dar es Salaam Msanii Nyashinski amesema kuwa kupata nafasi ya kutumbuiza jukwaa moja na wasanii mbalimbali wakubwa nchini Tanzania kama Alikiba ni jambo zuri ambalo litasaidia kufungua milango ya kufanya kazi na wasanii wa hapa kwa sababu ni matamanio makubwa kwa kila wanamuziki wa Kenya.
"Kwasasa wasanii wa Tanzania wamekuwa na majina makubwa na hata kupelekea mziki kwenda mbali zaidi, sasa hii fursa niliyoipata itafungua milango kwangu na kunifanya kuwa nao karibu," amesema Nyashiski.

Msanii maarufu nchini Kenya Nyamari Ongegu "Nyashinski" amewasili Tanzania kwa ajili ya tukio kubwa lililoandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti "OKTOBA FEST" ambalo litafanyika Oktoba 21, 2023 Coco Beach Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo la "SERENGETI LITE OKTOBA FEST" litajumuisha wasanii lukuki kutoka hapa Nchini Tanzania wakiongozwa na Alikiba, billinas, Chino kidd, Gnako na Msanii kutoka nchini Uganda Jose Chameleon.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: