Articles by "UJUMBE WA LEO"
Showing posts with label UJUMBE WA LEO. Show all posts
WANAWAKE laki moja ni Asasi iliyoanzishwa kwa kufuata sheria na taratibu za Nchi mnamo mwezi wa Kwanza 2020.

Lengo lake kuu ni Kuunganisha Wanawake wote Nchini Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Umaskini.

Mpaka sasa mtandao huu una wanachama katika Mikoa 17 Nchi nzima na kila Mkoa una uongozi ambao una Mwenyekiti, Katibu na Mwekahazina.

Mnamo tarehe 5/12/2020 Asasi ina kwenda kuzinduliwa ndani ya Ukumbi wa Banki kuu (BOT) Mkoani Mwanza kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni kwa kiingilio cha Shilingi elfu ishirini tu.

Kwa atakayetaka kushiriki na kuwa mwanachama anaweza ku wasiliana kwa njia ya WhatsApp kwa kutuma ujumbe kwa Katibu wa Mtandao Bi Josephine Ngoda kwa namba..0620765411


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na makundi mbalimbali ya vijana waliohudhuria katika Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye eneo la Chuo cha Uhasibu mkoani hapa.


Mwakilishi wa Vijana Omary Mwangi, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi zawadi ya Kitabu cha Historia ya Mwalimu Nyerere.

Vijana mkoani hapo wakimkabidhi mama Nchimbi picha ya Mwalimu Nyerere iliyochorwa kwa umahiri mkubwa na vijana wa mkoa.

Kongamano likiendelea.


Mmoja wa Wawezeshaji wa Kongamano hilo, Jacob Kanka akitoa mada .

RC Nchimbi akikabidhi zawadi ya Rozari Takatifu kwa vijana waliohudhuria Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwenye Chuo cha Uhasibu mkoani hapa, kama ishara ya heshima kwa mama huyo wa Yesu, ambaye Waumini wa Kanisa Katoliki na marafiki wa karibu hupata fursa ya kumkumbuka kwa kusali rozari kila ifikapo mwezi Mei na Oktoba kila mwaka.

Mratibu wa Kongamano hilo na Afisa wa Vijana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Frederick Ndahani akizungumza na vijana wa mkoa huo kabla ya kumkaribisha RC Nchimbi kufungua kongamano.

Washiriki wakisikiliza kwa makini nasaha za Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani)

Washiriki wakisikiliza kwa makini nasaha za Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani)

Kongamano likiendelea.

Washiriki wakisikiliza kwa makini nasaha za Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani)


Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amewataka vijana kuanza kufikiri ‘sawa-sawa- katika muktadha wa kuongozwa na tafakuri ya kina kujua na kuona sawa-sawa historia ya taifa la Tanzania lilipotoka, lilipo na linapoelekea.

Alisema kama vijana watafikiri sawasawa ni lazima watakuwa na upeo mkubwa wa jicho la kuona sawasawa mnyororo mzima wa hatua kadhaa za kimaendeleo zilizofikiwa hatua kwa hatua tangu uhuru

Nchimbi alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na vijana mbalimbali jana, kupitia  ‘Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa 2020, lililofanyika jana kwenye Chuo cha Uhasibu mkoani hapa

“Tusipofanya tafakuri ya kina hata tafsiri ya vitu vinavyofanywa na serikali hatutaviona, na matokeo yake itakuwa ni rahisi sana kudanganywa na wapotoshaji wasiolitakia mema taifa letu,” alisema Nchimbi na kuongeza: “Kijana ukifikiri sawasawa utaona sawasawa, utatekeleza sawasawa na utaamua sawasawa.”

Mkuu wa Mkoa aliwaambia vijana kuwa bila ya kumfahamu vizuri na kumtazama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kamwe hawawezi kuwa kiunganishi mahiri kwenye mnyororo wa kiuchumi kutoka kwenye Uchumi wa Kati kwa sasa, kuelekea uchumi wa Juu wa Kati

“Vijana ndio watendaji, na kumbukeni miradi yote hii mikubwa ya kitaifa inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na kipenzi chetu Rais John Pombe Joseph Magufuli inafanyika kwa fedha zetu za ndani na zaidi ni kwa manufaa yenu vijana…fikirini sawasawa ili muone sawasawa,” alisema

Mama Nchimbi alisema Tanzania ni urithi wetu tulioachiwa na Baba wa Taifa, hakuna urithi mwingine, hivyo vijana wanapomkumbuka wana jukumu la kumuenzi kwa kusimama vizuri, kuwa na uzalendo na kujifunza historia ya nchi, ili hatimaye kwenda kwa kasi na tija inayodhihirika katika kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa juu wa kati

“Kijana huwezi kujiangalia wewe bila ya kumtazama Baba wa Taifa…Nyerere ni alama muhimu sana, ili tushiriki ipasavyo kwenye uchumi huu wa kati ni lazima tuijue historia ya tulipotoka kati ni dhahiri tutakuwa na majawabu ya je…hatua hii ya uchumi wa kati, amani na uhuru vinaamanisha nini?..na ni lazima twende katika fikra zitakazotuonyesha sisi ni taifa la Tanzania na sio vinginevyo,” alisema Nchimbi.

Awali, Mratibu wa Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa 2020, Frederick Ndahani, alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema “Mjenga nchi ni Mwananchi na Mvunja nchi ni Mwananchi” hivyo kama vijana wanathamini sana amani, na kamwe hawatavunja miiko wala kutumika na yeyote kwa maslahi yake binafsi, kuvuruga amani na utulivu uliopo.

“Sisi vijana wa mkoa huu tumeshuhudia maono ya Baba wa Taifa yakiwa yanatekelezwa kwa kasi katika serikali hii ya Awamu ya Tano kwenye Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Madini, Mawasiliano, Miundombinu, Nishati na miradi mingine mingi…hii inatupa taswira na matumaini makubwa kama vijana katika mustakabali wa maisha yetu kwa sasa na vizazi vijavyo,” alisema Ndahani.

Ndahani ambaye ni Afisa Vijana wa Mkoa, na mmoja wa vijana shupavu waliokimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima kwa mwaka 2017, alisema kama vijana wanajivunia na kutambua mchango mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali, uliofanywa na viongozi wa Taifa la Tanzania kuanzia Mwalimu Nyerere mpaka sasa chini Rais John Magufuli.

“Tunawashukuru sana viongozi wetu kwa maono na hatimaye kutufikisha kwenye uchumi huu wa kati. Na kipekee kwa niaba ya vijana wa mkoa huu namshukuru sana Rais Magufuli kwa busara na hekima za alizojaliwa Mwenyezi Mungu kwa namna alivyofanikiwa kulivusha salama taifa hili dhidi ya janga hatari la Corona,” alisema Ndahani na kuongeza:

“Miongoni mwa wahanga wakubwa wa gonjwa hili tulikuwa ni sisi vijana, lakini leo hii kwa ushupavu na ujasiri wa Rais Magufuli tunaendelea kama kawaida na masomo yetu kwenye shule na vyuo vyote nchi nzima, lakini pia tunaendelea kujiachia kwa kukusanyika kama hivi leo…katika kujadili na kukumbushana majukumu yetu kama vijana kwa mustakabali chanya wa Taifa letu,” alisisitiza Ndahani.

Nimebahatika kupata fursa kadhaa kukaa na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa enzi za uhai wake.

Fursa ambayo sitaisahau ni ile ya masaa 10 ya mazungumzo kati yetu alipokuja shambani kwake Turiani Morogoro mwezi Novemba 2014, wakati huo nikiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero.

Masaa 10 na Rais Mkapa, muda ambao ni nadra sana kwa yeye kumpatia mtu kwa mazungumzo yalinijenga na kunikomaza kiuongozi. Nilipata fursa ya kujifunza mengi kutoka kwake na kupata ufafanuzi juu ya maoni mengi juu yake niliyoyasoma kwenye magazeti. Tulizungumza mambo mengi sana yahusuyo uongozi na hatma ya nchi yetu.

Nilitumia wasaa huo kumuuliza ikiwa anayaona yale aliyoyazungumzia kwenye hotuba zake kabambe ikiwemo ile aliyoitoa kwenye Halmashauri Kuu ya CCM ya Agosti 2004 maarufu kama "Ushupavu wa Uongozi" (The Courage of Leadership); na ile hotuba yake aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa 2005 wa kuchagua Mgombea Urais wa CCM zitakidhi matakwa ya siasa za 2015.

Nilitaka pia kujua maoni yake kuhusu mtazamo na hisia juu ya uamuzi wa kuwaondoa wazee (Wenyeviti Wastaafu, Makamu Wenyeviti Wastaafu na Makatibu Wakuu Wastaafu) kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM. Jibu lake lilikuwa uamuzi ule ulitokana na mapendekezo yao wazee kuomba wapumzishwe kwenye vikao hivyo vya juu vya chama. Sababu zao kubwa zilikuwa mbili. Kwanza, waliona busara kumpatia Rais na Mwenyekiti wa Chama aliyeko madarakani uhuru zaidi wa kuongoza.

Pili, kuondoa dhana iliyokuwa ikijitokeza kila walipopata udhuru na kutohudhuria kuhisiwa na vyombo vya Habari kwamba wamesusia vikao vya Mwenyekiti. Ushauri wao ulikuwa ni kuundwa kwa Baraza la Wazee ili kukidhi dhima yao ya kutoa ushauri. Aidha, uamuzi ule uliwaondoa tu kuwa wajumbe wa kudumu wa vikao vya chama lakini haukuondoa uwezekano wa wao kualikwa kwenye vikao hivyo kwa mwaliko maalum.

Udadisi wangu haukuishia hapo. Nilimuuliza pia mtazamo wake juu ya maoni ya wengi dhidi ya mafanikio ya sera yake ya ubinafsishaji. Alinifurahisha kujua kuwa, amekuwa akisoma na kuona namna ambavyo jambo hilo lilivyopokelewa na wachambuzi mbalimbali.

Kilichomshangaza yeye ni namna ambavyo wapinzani wa sera hiyo ama kwa makusudi au kwa kupitiwa walijikita tu kwenye mifano ya maeneo ambayo ubinafsishaji haukwenda vizuri. Alishangaa kwa nini watu hao hawakutoa pia mifano mizuri ya ubinafsishaji kama ile ya Benki ya NBC iliyozaa Benki ya NMB, Kiwanda cha Sigara (TCC), baadhi ya viwanda vya sukari vinavyofanya vizuri na maeneo mengine. 

Tukiwa bado kwenye eneo hilo, nilimuuliza kwa nini aliamua kubadili noti na sarafu alipoingia madarakani. Jibu lake lilikuwa, uamuzi ule ulilenga kuwashawishi wale waliokuwa wamehodhi fedha majumbani mwao kuzirudisha benki. Kwa maelezo yake, uamuzi ule ulikuwa wa mafanikio kwani fedha iliyorudi benki ambayo ilikuwa nje ya mzunguko ilikuwa ni zaidi ya ile iliyokuwapo katika benki zetu.

Jambo lingine nililotaka kupata mtazamo wake ni ule utamaduni wa kukabidhi kofia ya uenyekiti wa Chama kwa Rais mpya (kuunganisha kofia mbili) kabla ya miezi 24 ya kwanza kuisha, yaani kabla ya Mkutano Mkuu wa Chama kikatiba. Maelezo yake yalikuwa kwamba kipindi hicho ndio muafaka zaidi wakati Rais mpya akiwa bado kwenye fungate ya kisiasa (political honeymoon). 

Baada ya muda huo, Rais huwa ameelemewa na mambo mengi. Nikataka pia kujua kwa nini hapendi kuongea chochote kama mzee mstaafu wakati ambao CCM walipitia mambo mengi kati ya 2008-2014. Jibu lake lilikuwa kwamba silaha nzuri kwa kiongozi mstaafu duniani ni kukaa kimya maana upo mstari mwembamba sana kati ya kushauri na kutoa maoni kwa upande mmoja, na kukosoa na kuingia kwa upande mwingine.

Mazungumzo yetu yaliendelea na kwa kweli sikumpatia wasaa wa kupumzika. Nikataka kujua iweje hakuwahi kumteua Comrade Abdulrahman Kinana katika nafasi yoyote ilihali alikuwa meneja wa kampeni zake za urais mara mbili. Jibu lake lilikuwa alitamani kumteua lakini Ndugu Kinana alimkatalia. Alifanya hivyo tena ilipofufuliwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kumuomba ampendekeze kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki jambo ambalo alilikubali. 

Tukaendelea, nikamuuliza, katika siku ya kwanza ya urais wake baada ya kuapishwa na kurejea Ikulu ni jambo gani la kwanza alilolifanya? Akaniambia, alimwandikia mtangulizi wake Rais Ali Hassan Mwinyi barua kwa mwandiko wa mkono wake bila kuichapa, akimshukuru sana kwa mchakato mzima wa kumpata Rais na kuahidi kuendelea kuomba ushauri wake katika kuendesha nchi.

Nilipomdadisi juu ya mtazamo wake kwenye kinyang’anyiro cha urais 2015 kilichokuwa mbele yetu wakati huo hakuwa tayari kufunguka. Pengine ni katika kuishi ile dhana ya kuwa ukistaafu unapaswa kujifunza kukaa kimya. Hata hivyo, nilimchokoza kwa kumtajia majina ya wagombea mbalimbali waliokuwa wakitajwa tajwa wakati huo. Nilimtajia majina 13. Wakati nikimtajia jina alikuwa anaitikia tu kwa kutikisa kichwa. 

Yapo majina ya wagombea ambayo hakuwa akiamini kama kweli watagombea na wapo wale alioshia kutabasamu na wapo ambao waliomsisimua. Utulivu wa mzee Mkapa ulikuwa unafanya kutojua hisia zake, lakini unapogusa mahala anapopapenda uliweza ona hata mishipa ya utosi wake ikifurahi. Nililiona hilo nilipolitaja jina la Dkt. John Joseph Pombe Magufuli. Ni dhahiri Rais Mkapa alimpenda sana Dkt. Magufuli. Haikuhitajika tochi kuona mapenzi yake kwa Magufuli. Alichozungumza siku hiyo kilibaki funzo na darasa kwangu.

Tulizungumzia zaidi ya masuala ya siasa. Nilipenda pia kufahamu maisha yake nje ya siasa na uongozi. Mmoja wa wasaidizi wa Mzee Mkapa, wakati huo marehemu Mkude ambaye alikuwepo usiku ule hakusita kueleza hisia zake kwangu. Aliniambia kuwa mimi ni mwenye bahati kupata wasaa mrefu vile na Mzee Mkapa. Kuonyesha furaha yangu, nikamwambia kaka Mkude fursa ile itabaki kwenye kumbukumbu za maisha yangu kama Novemba Kuu (The Great November). Marehemu Mkude ndiye aliyenipiga picha na Mzee Mkapa usiku ule Mtaka wa mwezi Novemba baada ya mazungumzo yetu yaliyoanza saa kumi jioni na kumalizika saa saba usiku.

Mbali na mazungumzo yetu, nimekuwa msomaji mzuri wa hotuba zote za Mzee Mkapa alizotoa kila mwisho wa mwezi akiwa madarakani na zile alizotoa katika shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Niliendelea kuwa mtoto na rafiki wa Mzee Mkapa hata nilipohamishiwa Wilaya ya Hai na baadae kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Bado nilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu, japo sikuwahi kuyapata tena masaa 10 kama ilivyotokea Turiani. Mzee Mkapa aliendelea kuwa rafiki yangu, Mwalimu wangu na kila tulipoonana hatukuacha kuzungumza na kwa kweli nilimdodosa na kujifunza mengi.

Leo Mzee Mkapa hayupo nasi. Niseme nini zaidi? Nimempoteza baba, rafiki na mtu aliyependa kuniona nikifanya vizuri kwenye kazi zangu na hasa akinisisitiza kuwasaidia wananchi wanyonge kutoka kwenye umaskini na kuwatatulia shida zao.

Hakika nchi imepoteza mzee mwenye maono, msimamo na mwana mageuzi wa kweli aliyeipenda nchi yake kwa dhati ya moyo wake.

Miaka 10 ya utawala wake alitufikisha mahala pazuri, alijenga taasisi ambazo zitaishi daima mioyoni mwa Watanzania, aliipenda imani ya kanisa lake na kuheshimu imani za watu wengine.

Natoa pole kwa Mama Anna, watoto wake na nampa pole Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumpoteza Kiongozi Mashuhuri kwenye nchi na mlezi wake aliyemuamini na kumpa dhamana ya unaibu waziri akiwa na umri ulio chini ya miaka 40.Nampa pole kiongozi wangu wa zamani Ndugu William Erio, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ambaye kupitia yeye, Mzee Mkapa alinipenda na kuniamini. Nampa pole nyingi dada yangu Dkt.Ellen Senkoro, Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation ambaye wakati wote wa shughuli za Mzee Mkapa alipenda kunialika kwenye shughuli za Mzee wangu huyu.

Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele Mzee Mkapa. Hii dunia sisi ni wapitaji. Miaka yetu hakika ni ya kukopeshwa. Pumzika baba yangu, pumzika rafiki yangu, pumzika kiongozi wetu, Tutaonana kwenye ile asubuhi njema na iliyo kuu.

Mwanao
Anthony Mtaka.
Baada ya siku chache kupita tangia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Ubungo kumuamini Prof Alexander Kitila Mkumbo kwa kumpa kura nyingi za kutosha kuongoza katika kinyang'anyilo hicho.

Kura hizo nyingi alizozipata Prof Kitila Mkumbo ni kura za maoni za kumpendekeza kuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Ubungo ambapo kura hizo za maoni zitasaidia vikao vya uteuzi kufanya uteuzi wake.

Wahitimu mbali mbali waliopita mikononi mwa Prof Kitila Mkumbo toka Shule Kuu ya Elimu (SOED) Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii na sehemu nyingine nyingi kumuunga mkono mwalimu wao na kufurahishwa na uaminifu wa wajumbe kwa mwalimu wao Prof Kitila Mkumbo.

Prof Kitila Mkumbo alikuwa ni mwalimu wa masomo ya saikolojia ndani ya shule kuu ya elimu Chuo Kikuu Cha DSM ambapo alihudumu hadi 2017 kabla ya kuaminiwa na Mhe Rais Ndg Dr John Joseph Pombe Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Wahitimu hao ambao ni wanafunzi wake wameahidi kumuunga mkono kwa kila hatua itakayofuatia ikitokea vikao vya uteuzi vitapendekeza jina lake kuwa mgombea wa CCM jimbo la Ubungo.


Na,
Hamis Abeid Baruani
0769808725
Kiongozi wa wahitimu wa 2017 SOED-UDSM
Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli. mfano : Matapeli wanaweza kukuuzia sim ya wizi ya bei kubwa ya kiasi cha shilingi laki nane ( 800,000/=) kwa fedha ndogo ya elfu sabini( 70,000/=) ili kukuingiza kingi ukiingia tu imekula kwako

Kwani simu hiyo unayouziwa ni ya mmoja wao (matapeli) na wanakuwa wamekopi Imei number ya simu hiyo sehemu.

Baada ya wiki wanakupigia ili kuangalia kama uko hewani. Huku wameshatoa ripoti polisi kuwa begi limeibiwa kwenye gari pamoja na vitu vingine na hiyo simu ikiwa ni mojawapo kati ya vitu vilivyoibiwa.

Na watatoa maelezo polisi thamani ya vitu vilivyoibiwa niTshs zaidi ya Milioni 7 (katika maelezo yake atakuwa ametaja laptop, fedha taslim na simu tatu au nne.)

Wanapewa mpelelezi na hapo ndipo Jeshi letu linajikuta limeingizwa kingi bila ya kujijua.

Mpelelezi anaomba msaada cyber crime kuitafuta simu hiyo.

Ikipatikana biashara inaanza . Unawekwa chini ya ulinzi kulipa vitu vyote ambavyo hujawahi hata kuviona na kesi ya wizi unayo.

Uongozi wa group unalishauri jeshi la polisi kuwa makini sana na hizi kesi za cyber. Labda mtakuja gundua kuwa simu hizi zinazotumika kutapelia watu zimekwisha ripotiwa mara mbili au tatu ndani ya miezi mitatu.

Ndugu zangu wanachama wa group hili msikubali kuuziwa simu mkononi ambayo ni used, na kama utanunua simu hiyo ambayo ni used basi mlipe kwa cheque, kagueni Imei number na umpige picha huyo aliyekuuzia pindi unapomkabidhi kiasi hicho cha Malipo.

Ikiwa hataki achana nae ndiyo salama yako.

Matapeli ni wengi sasa na wanabuni mbinu siku hadi siku ili kuyasukuma maisha yao.

Tunaitajika kuwa makini

Ahsanteni sana.
Nianze kwa kutoa pongezi za dhati kwa Mtandao wa Vodacom Tanzania kwa kuweza kufanikisha zoezi la usajili wa alama za vidole likawa jepesi kwa kuwafuata wateja katika mitaa mbali mbali hapa jijini Dar es Salaam.

Hili jambo nimelishuhudia mwenyewe jinsi vijana wanavyoingia mtaani na kusajili wananchi bila ya kuwatoza pesa yeyote.

Jambo lililonishangaza ni baadhi ya mitandao ya simu za mkononi kuwatoza pesa wananchi pindi wanapotaka kukamilisha usajili wao kwa alama za vidole.

Hili sikubalini nalo nalipinga na ndiyo maana nimeandika waraka huu wa wazi kwa viongozi ili watambue vijana wao wanayoyafanya mtaani.

Inawezekanaje ukamtoza mwananchi Tsh 1,000 kwa mtandao mmoja wa simu alionao??? wakati hili zoezi lilitangazwa na serikali ni bure??? Jambo hili nimelishuhudia baada ya kuwaomba vijana wanisajili walipomaliza nikaambiwa nitoe Tsh 2,000 kwa vile walinisajilia laini zangu mbili nilikataa na wakaanza lalamika nikawambia hili zoezi halipaswi kutozwa mwananchi yeyote, waondoka shingo upande.

Basi niwaombe wahusika wa mitandao ya simu ya Airtel, Tigo na TTCL kuonya vijana waache kutoza pesa ili kuwakamilishia wananchi zoezi la alama za vidole.

Tunaiomba mamlaka husika hasa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kukemea mara moja mchezo unaofanywa na vijana ambao ameona ndiyo njia pekee ya kujipatia pesa.

Ni Mimi Blasio Kachuchu.
Mkazi wa Mbezi Makabe-Dar es Salaam.
Na Amini Mgheni.

Ndio, wakati umefika wa vijana wa Tanzania sasa, tuongezeke kuvuka mipaka kwa wingi katika taaluma mbalimbali na kushika hatamu katika uchumi wa Afrika na hatimaye dunia.

Nasema hivi kwa kuwa sasa nawaona wapo vijana wa Tanzania ambao sasa wameonesha uwezo mkubwa katika kuendesha makampuni makubwa, sasa waanze kuvuka mipaka na kuondoka kwenye kuongoza makapuni makubwa Afrika na nje ya Afrika ilitushindane katika medani za kimataifa na kulitangaza taifa katika uwezo wa vijana na watanataaluma wetu.

Mfano natamani sasa nianze kuona makapuni makubwa ya mitandao ya simu yanaongozwa na vijana mahiri kutoka Tanzania, natamani kuona sasa benki kubwa za Afrika zinaongozwa au moja ya wakubwa wake ni vijana kutoka Tanzania.

Natamani kuona mashirika makubwa ya ujenzi, majengo, mahotel sasa yanaongozwa na vijana wa kitanzania watapakae kuyashika kwa nguvu ndani na nje ya Afrika.

Huu ndio wakati wa sisi kuanza kuonesha dunia uwezo wa vijana na watanzania vijana tusingoje vijana wetu wazeeke katika umri huu kila kijana sasa ajipange kwenda kushika hatamu nje ya mipaka ya nchi yetu, kisha idadi kubwa ya vijana wengine mahiri tubakie nyumbani na kushika uongozi wa mashirika makubwa ya ndani na kutoka nje ambayo yamewekeza ndani tunyanyuke wakati ni sasa.

Wakati umefika kwa wahandisi wetu kuanza kuunda makampuni makubwa na ambao tayari wanayo sasa yavuke mipaka yakachukua miradi mikubwa nje ya Tanzania na katika mataifa makubwa kama vile Wachina alivyotapakaa duniani.

Kwenye michezo na sanaa twendeni kila mmoja awaze sasa kujitambualisha na kuifikia dunia kwa kila kipaji chake, tuutambulishe Utanzania huko kama akina Mbwana Samatta.

Tauche kulalamika hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa kwa kulalamika, kila tatizo lichukue kama changamoto kwako ya kusonga mbele ambayo lazima uishinde usichukulie tatizo kama kikwazo cha kukurudisha nyuma.

Wenye kuelewa na muelewe tuanze kuchukua hatua, kwa viongozi wa serikali walipewa dhamana kupitia ndani na balozi zetu sasa anzeni kwa nguvu kubwa kufanya hili litimie kila kona Watanzania tusimame kuishika dunia wakati ni sasa ndugu zangu.
Palikuwa na mchoraji mmoja ktk moja ya mji mchoraji huyo alikuwa mwenye umri wa utu uzima.

Alikuwa akichora picha nzuri sana na akiziuza kwa gharama kubwa sana.

Siku moja wakamjia maskini na mafukara wa ktk mji ule wakamwambia.

"Wewe unatengeneza kipato kikubwa sana kwa kazi yako hii ni kwa nn hutaki kutusaidia sisi watu wa hali ya chini,,,,,

Watazame wenzako wanaouza nyama ijapokuwa hawana kipato kikubwa lkn kila siku hutoa vipande vya nyama kuwasaidia wasiojiweza."

Mchoraji hakuwajibu chochote ila aliwaonyeshea uso wa furaha tu.

Wale mafukara wa mji ule waliondoka wakichukizwa na suala lile la mchoraji.

Ikawa wakitangaziana pale kijijini kuwa mchoraji yule m/mungu amemjaalia kipato lkn ni mbahiri si mwenye kuwasaidia wasiojiweza.

Baada ya muda mchoraji yule alianza kuugua lkn hakuna mwanakijiji yeyote aliye kwenda kumuona mpk akafa.

Baada ya kufa yule mchoraji siku zilipita na ikawa wale wauza nyama hawatoi tena nyama kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza.

Wale wanakijiji ikabidi wawaulize wale wauza nyama ni kwa nn hawawasaidii tena nyama kama zamani.?

Wauza nyama wakawajibu kuwa mchoraji alikuwa akiwapa pesa kila mwezi kwa niaba ya kuwanunulia nyama wasiojiweza.

Na wawape bure kila siku lkn alipofariki likasimama jambo hilo kwani hazikutoka tena pesa za kuwanunulia wao nyama kwa kuwa mchoraji ameshakufa........

Baadhi ya watu huwenda wakawa wanakudhania vibaya lkn na wengine huenda wakakuona msafi kama maji yasiyoharibiwa.

Tambua hawakuzidishii kitu kwa wao kukuona ww kuwa ni msafi

Na wala hawakupunguzii kitu kwa wao kukudhania vibaya.

Kilichomuhimu ni vile akujuavyo mola wako kuwa ww ni mtu wa aina gani kwani yy ndiye anaejua ya siri na ya dhahiri.

Usimuhukumu mtu yeyote kwa muonekano wake wa nje kwani hujui undani wake.

Kwani hujui undani wake kuna baadhi ya matendo ayafanyayo lau kama ungeliyajua ungemuhishimu sana.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiwa ofisini kwake, zilizopo Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dr. Reginald Mengi. 

Na Kadama Malunde – Johannesburg,Afrika Kusini.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele amesema Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP marehemu Dr. Reginald Mengi ni Shujaa na Mwanamapinduzi wa kiuchumi na anastahili kupewa heshima ya kuwa Nembo ya Uwekezaji na Sekta binafsi Tanzania. 

Mhe. Masele ambaye ni mbunge wa Shinyanga Mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa zamani nchini Tanzania amesema hayo leo Jumapili Mei 5, 2019 akiwa nchini Afrika Kusini, wakati akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dr. Reginald Mengi, aliyefariki dunia Mei 2, 2019 huko Dubai. 

“Mzee Mengi ninamtambua kama Mwanamapinduzi wa Kiuchumi kwa sababu ndiye Nembo ya Uwekezaji kwa Wazalendo na ndiyo Nembo ya Sekta Binafsi katika nchi yetu”,ameeleza Masele. 

“Mzee Mengi atakumbukwa zaidi kuwa miongoni kwa Watanzania wa mwanzo kuwekeza nchini na nitafurahi zaidi akipewa heshima ya kwamba yeye ndiye Nembo ya Uwekezaji,Nembo ya Sekta binafsi katika taifa letu”,amesema Masele. 

Masele amemwelezea Mzee Mengi, kuwa alikuwa mtu mnyenyekevu,asiye na majivuno, mwenye kuheshimu watu wote bila kujali nafasi yake katika jamii licha ya kuwa na uwezo wake kifedha aliojaliwa na Mwenyezi Mungu. 

“Nadhani ni vizuri kwa sisi vijana hususani viongozi kujifunza kwamba pamoja na nafasi tulizonazo ni vyema kuwa wanyenyekevu kwa binadamu wenzetu,mbele ya Mungu lakini pia kuheshimiana bila kujali nafasi zetu katika jamii”,ameongeza Masele. 

Masele amewapa pole familia ya Mzee Mengi, marafiki,wafanyakazi wote wa Makampuni aliyokuwa anayaongoza na Watanzania wote kwa ujumla ikiwemo sekta binafsi. 

“Kwa kweli nimepokea taarifa za msiba huu kwa huzuni kubwa,nimehuzunika kuondokewa Mzee wetu nilifanya nae kazi wakati nikiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na yeye akiwa kiongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania,tulifanya kazi kwa ukaribu sana,tulikuwa na vikao mbalimbali kuhusu masuala ya Uwekezaji.. tumuombe Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani Mzee wetu ,Amin”,ameongeza Masele.

Mheshimiwa Masele yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria Kikao cha Pili cha Kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kitakachoanza siku ya Jumatatu Mei 6, 2019 Jijini Johannesburg Afrika Kusini. 

Mgeni rasmi atakayefungua kikao hicho cha Bunge la Afrika ni Spika wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Dk. Amal Abdulla Al Qubaisi ambaye tayari ameshawasili nchini Afrika Kusini.
Na Emmanuel J. Shilatu

Ni miaka 55 imetimia tangu jahazi lililowabeba Watanganyika na Wazanzibar liweke historia ya kung’oa nanga mara baada ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kuzaliwa rasmi mnamo April 26,1964. Hii ilitokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati waliyokuwa nayo waasisi wa Muungano huu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Abeid Aman Karume (Zanzibar).

Hatua hiyo ilifikiwa kutokana na mtiririko wa kimazingira na mahusiano ambayo yalishabihiana kama sio kufanana kabisa kwa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar). Zipo sababu za kijiografia, kisayansi, kitamaduni na kihistoria zilizochangia huu muungano wetu.

Kutokana na sababu za kijiografia na kisayansi inaaminika kabisa kwamba Visiwa vya Zanzibar (Pemba na Unguja) vilikuwa vimeungana na hata kushikamana kwa pamoja pembezoni mwa pwani ya ardhi ya Tanganyika. Hivyo tangu awali tulikuwa ni kitu kimoja, tulio katika ardhi moja na ya pamoja.

Pia kuna historia (isiyo na shaka) ya muingiliano wa kiutamaduni baina ya Wakazi wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hali nzima ya kuoa ama kuolewa ilizidi kushamiri baina yao.

Halikadhalika harakati za kudai ukombozi wa uhuru wetu ili tuweze kujitawala wenyewe kutoka kwa dudu la wakoloni nazo zilichangia kutuunganisha. Inaaminika (na ndiyo ilivyo) ya kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibar walishiriki kwenye harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Mwingereza ambapo kutokana na nia, ushupavu na nguvu ya pamoja walifanikiwa kupata Uhuru wa Tanganyika mnamo Desemba 9, 1961.

Lakini pia licha ya asilimia kubwa ya Wazanzibar kushiriki katika mchakato wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini pia kulikuwepo na asilimia kubwa ya mchango wa ushiriki kutoka kwa Watanganyika. Hatimaye matunda yake yalionekana ya mapinduzi matukufu yaliyofikia kilele katika uwanja wa Gombani Pemba yaliyofanyika Jamhuri 12, 1964, baada ya kuchoshwa na hila na ghiliba za Waarabu uliotamalaki visiwani humo kwa zaidi ya karne mbili na hatimaye waliwaacha wazalendo watwana katika ardhi yao.

Pia tusisahau lengo na nia ya dhati aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere ya kutaka kuiunganisha Afrika mzima kwa hatua lakini jitihada zake zilianza kuzaa matunda ambayo hayatakaa yatokee tena Afrika kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar.

Mnamo April 22, 1964, Maraisi wa nchi hizi mbili ambazo sasa zinaunda Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa Jamhuri ya Tanganyika) na Abeid Amani Karume (wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ) walitia sahihi Mkataba wa kimataifa wa kuunganisha nchi zao, unaojulikana kama “Hati ya Muungano” (Articles of union) na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ama United Republic of Tanganyika and Zanzibar (URTZ) ambao ni muungano sahihi kabisa kisheria na unaotambulika Kikatiba.

Siku ya Jumatatu ya tarehe 26 Aprili, 1964 viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee kwa nia ama lengo moja tu la kubadilishana “Hati za Muungano”.

Wananchi wa Tanzania walipiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kwanza kabisa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 1965.

Kama nilivyodokeza kwamba Muungano wa Tanzania ulifikiwa kwa kutiwa sahihi mkataba unaoitwa Hati ya Muungano (Articles of the Union) na wakuu wa nchi hizi mbili, Mwalimu Nyerere (Tanganyika) na Abeid Karume (Zanzibar) Aprili 22,1964 na kuridhiwa na mabunge ya nchi hizo Aprili 25, 1964 na hatimaye kuwa sheria ya Muungano ya (Acts of Union) ya mwaka 1964.

Kimsingi sheria ya Muungano ndiyo iliyoanzisha na ndiyo iliyopewa haki ya chombo cha kikatiba kinachodhibiti katiba zote mbili za Serikali ya Muungano.

Mwanzoni kabisa Hati ya Muungano (Articles of Union) iliyomo ndani ya sheria ya Muungano iliorodhesha na hata kudadavua mambo 11 ya Muungano. Mambo hayo ni kama vile:- Mambo ya nchi za nje, Ulinzi na usalama (lakini si usalama wa Taifa); Polisi, Uraia, uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika serikali ya Muungano, kodi ya mapato, usimamizi wa fedha, Bandari, Usafiri wa anga, Posta na simu.

Kwa nia safi na malengo mazuri yanayojitokeza Hati ya Muungano imekuwa ikiboreshwa zaidi kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele kwa malengo kusudi ya kuleta umoja, mshikamano, amani na utulivu wetu ule ule tulioanza nao awali na halikadhalika maridhiko yanayoendelea kuufanya Muungano huu uendelee kudumu hadi hii kesho.

Ndio maana mtu timamu hatoshangaa sana kuona Hati ya Muungano ikiendelea kuboreshwa kila siku (na itaendelea hivyo) ambapo ilianzia na mambo 11 ambapo hii leo yamefikia takribani 23.

Mengineyo ama baadhi ya yale yalioongezeka ni kama vile;- Noti; Elimu ya juu,; Maliasili na mafuta (mafuta) yasiyochujwa, bidhaa za mafuta na gesi asilia , ya mwaka 1968; Baraza la Mitihani ya Taifa; utafiti; utabiri wa hali ya hewa; Takwimu,; Mahakama ya Rufaa ya juu ya mwaka 1979; pamoja na uandikishwaji wa vyama vya kisiasa .

Tusisahau mwaka 1965 iliundwa katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interim Constitution of The United Republic of Tanzania) mpaka kufikia mwaka 1977 ndipo ilipoundwa katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo inaendesha nchi hadi sasa.

Kukuru kakara za Wazanzibari zinatookana na madai yao ya kuwa Tanganyika(Bara) imeimeza Zanzibar (Visiwani) katika masuala mazima yahusuyo Muungano. Ikumbukwe Ubaguzi wa dhana ya Tanganyika umeimeza Zanzibar si ya kweli na hii imebainishwa katika katiba ya Muungano kuwa kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Haya ni mapenzi ya dhati waliyoonyesha kwa Wazanzibari kwa kuwaruhusu wawe na serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ikumbukwe Serikali ya Muungano inaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaongozwa na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar na chombo chao cha kutunga sheria kinaitwa Baraza la Wawakilishi.

Ndugu zangu hali ya kupuuzia na hata kuuchezea Muungano wetu ni hatari sana tena ni dhambi iliyotukuka. Mathalani Wazanzibari wakiamua kujiengua kwenye huu Muungano ili wawe kivyao vyao,hawatabaki salama. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kuwa “wakifika kwenye hatua hiyo watagundua kuwa ndani yao kuna Wazanzibari na Wazanzibara”. Nao wataamua kuwafukuza wale wa Wazanzibara, lakini hiyo haitakuwa mwisho. Punde si punde watajigundua kuwa nao (Wazanzibari) wamegawanyika kwani kuna Wapemba na Waunguja, na wakifikia hapo pia hawatakuwa salama ni lazima machafuko yatatokea.

Daima Wazanzibari watambue ya kuwa dhambi ya kutokutamalaki kwa dhana ya Unguja na Pemba unatoka na kufunikwa na kivuli cha mwamvuli cha Muungano. Hivyo umoja, mshikamano, amani na utulivu wao unategemea sana uwepo wa nguzo hii imara ya Muungano huu tulionao.

Vivyo hivyo kwa watu wa Bara (Tanganyika) ni rahisi kwao kutafunwa na dhambi ile ile ya ubaguzi watakayo ianzisha nje ya uwepo wa Muungano ni rahisi sana kwa ukabila, udini, ukanda na hata U-rangi kutamalaki ndani ya jamii wakishafikia hapo, hawatabaki salama kwani watachafuana tu.

Muungano huu tulionao unawafanya wale wageni, mataifa ya nje na watu wote wenye hila, donge, roho ya korosho kuogopa kutugusa na kutuvuruga kutokana na kuwepo kwa nguvu kubwa ya umoja, ushirikiano na mshikamano baina yetu.

Muungano huu wetu unatupatia fursa kubwa ya uhuru wa kusafiri kwa pande zote iwe ni bara ama ni visiwani. Leo hii ni rahisi sana kwa mtu wa bara kwenda Visiwani na hata wale wa Visiwani kuja Bara kwa uhuru zaidi kwani Uhuru huo wa uwepo wa nafasi hiyo umeshalipiwa na huu Muungano wetu tulionao.

Kutokana na uwepo wa uhuru wa kusafiri usio na mipaka baina yetu, pia Muungano wetu tulionao unazidi kutuongezea fursa na nafasi zaidi ya uwanja mpana wa ufanyaji biashara. Hali hii imesababisha uwepo wa mzunguko mkubwa wa pesa ndani yetu kwani si jambo la ajabu kuona pesa zikitoka Visiwani (Zanzibar) kuja Bara (Tanganyika) kupitia mabadilishano ya bidhaa kama vile nafaka, kahawa, matunda, vipuri vya magari na kadhalika.

Pia si jambo geni tena kwa sasa kuona pesa zikivuka Bahari na kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ufanyaji ama ununuzi wa biashara kama vile Magari, nazi, Karafuu, Tende na kadhalika.

Muungano huu unatuzidishia fursa ya mianya ya uwanja mpana tena usio na kikomo wa ufanyaji biashara, Muungano huu hautubagui ama kutojulisha au kuwa na upendeleo wa upatikanaji wa Elimu bora, huduma za kijamii bora, Muungano hautugawi wala kuwa na upendeleo bali umejaa uwiano sahihi wa upatikanaji wa mabo yote ya msingi yaliyomo ndani ya “Hati ya Muungano” (Articles of union). Muungano huu ni nguzo imara katika muktadha mzima wa nyanja za kimaisha yetu.

Ni ukweli uliodhahiri kuwa haitakaa itokee Muungano kama huu (wa Tanganyika na Zanzibar) hapa Barani Afrika umoja ushirikiano, ushikamano, amani na utulivu ni sehemu mojawapo ya manufaa ya Muungano huu.

Njia mojawapo ya kuwaenzi vyema waasisi wetu ni kwa kuudumisha Muungano wetu ambao ni urithi wa aina yake waliotuachia. Watanzania yatupasa tuenzi Muungano wetu kwa kuulinda na kuudumisha kwa vitendo kwani ni nguzo na fahari ya kipekee na ya aina yake Barani Afrika.

0767488622
 Ni siku ya Jumanne ya Februari 26, 2019 majira ya saa mbili na robo nikiwa naendesha gari kurudi nyumbani Madale! Kupitia mitandao ya kijamii naona uzi kwamba ndugu yangu Ruge ametangulia mbele ya haki! Moyo wa binadamu umeumbwa kwa kuogopa taarifa mbaya hasa za kifo tena cha mtu mnayefahamiana.

Nikiwa kwenye mshtuko na mtanziko huo, ghafla kwenye simu yangu unaigia ujumbe wa Mfalme! Ujumbe ambao unathibitisha kifo, safari hii si kupitia taarifa za Gerson Msigwa isipokuwa kupitia kwenye ukurasa wa twitter ya Mheshimiwa Rais, Dk John Magufuli. Kwa kweli umemwelezea Ruge vizuri zaidi!

Ujumbe huo ukanikumbusha thamani ya kila mwanadamu awapo duniani na baada ya kuondoka, utakumbukwa kwa jambo gani? baya ama zuri? Nikakumbuka tena kwamba Ruge hajafa isipokuwa amelala tu! Maana ameacha alama (icon) na benchmark nyingi ambazo kupitia hizo namwona akiendelea kuishi.

Jina Ruge katika tasnia ya burudani pamoja na mambo mengine ya kijamii ni sawa na maji! Usipoyanywa basi utayaoga, kama ikishindikana kuyaoga basi hata chooni utachambia. Ruge ulikuwa zawadi kwa familia na ukoo wa Mutahaba, kwa tasnia ya habari ulikuwa nguzo na katika tasnia ya burudani, ulikuwa funguo!
Tazama zawadi imepotea na nguzo imeanguka, lakini funguo imebaki! Kupitia kwako Ruge umewafungulia vijana wengi dunia kuwa wanachotaka! Bila ufunguo wako pengine leo vijana wengi wangekuwa kama kipofu asiyekuwa na fimbo nyeupe! Changamoto zingekuwa nyingi zaidi, lakini tazama leo umelala usingizi mzito lakini ufunguo umetuachia vijana, kikubwa ni kuutumia vizuri ili isije kutulazimu kubadili kitasa.

Kaka Ruge umeondoka, mdogo wako umeniachia funzo moja kubwa, roho ya kusamehe. Katika maisha yako hukuruhusu chuki na ugomvi vikutawale, hata pale vilipotokea ulihakikisha vinakwisha na maisha mengine yasonge mbele! Ninakumbuka siku Rais anazindua mradi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Hoima, Uganda. Pale ulitoa funzo kubwa kama lile alilolitoa Yesu Kristu akiwa amewambwa msalabani pamoja na wale wanyang'anyi wawili!

Rais alitaka Ruge usameheane na Gavana wa Darisalama, bila kinyongo tena kwa sura ya tabasamu ukaonesha kukubali na kuishi kile ulichokiamini. Sitaki kuzungumzia suala la ugomvi uliokuwapo baina yako na Mbunge wa sasa wa Mbeya Mjini, baadaye mkashikana mikono na maisha yakaendelea! Moyo wa aina hiyo unapatikana vifuani mwa wanadamu wachache ambao mmoja wao ni Ruge.

Ninasikitika ninaandika mambo yanayokuhusu wakati hutapata fursa ya kuyasikia, lakini nafarijika kwamba kupitia mafunzo hayo machache kutoka kwako wachache miongoni mwetu tunaweza kujifunza kuwa kama Ruge.

Pumzika kwa amani emanzi eya' Buhaya ninaendelea kuamini kwamba Mwenyezi Mungu amekuchukua baada ya kumaliza kazi ambayo alikutuma uje kuifanya hapa duniani! Amekuita ukafanye kazi nyingine huko mbinguni.

Omukama akuhumuze ne'milembe Amina.

Imeandikwa na Mkinga Mkinga.
Na January Makamba

Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia. Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia. Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona - hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako.

Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali kwa ajili ya kutoiangusha familia yako nzima iliyosimamisha kila kitu kukuuguza na Watanzania wote waliokuwa wanakuombea. Ulipigana kupona, sio kwa ajili yako, bali kwa ajili yetu. Hukuamka kitandani lakini hukushindwa mapambano kwasababu umeamkia ndani ya mioyo ya Watanzania. Huku tuliko karibu watu wote tunakumbuka ulivyotugusa. Jamaa yangu, tunakuomboleza wakati huu, halafu tutabaki tunafurahia nuru yako katika maisha ya wengi kwa urefu wa uhai wetu. Umekimbia mbio njema, umemaliza safari yako vyema.

Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako – kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.

Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga – mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako – mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, tupe ishara tufanyeje.

Nafarijika kidogo kwamba nilipata nafasi ya kukukumbatia kwa mara ya mwisho. Sikujua kwamba tunaagana. Ulinishika mkono kwa nguvu, hukutaka kuuachia, na ulitabasamu niliposema nakungoja Dar tukae pale THT, kama kawaida yetu, kujadili mawazo na mipango yako mingi.

Ingawa umeshawasili huko upande wa pili, familia yako na watu wengi watauaga mwili wako kwa heshima kubwa. Utajengewa kaburi. Nadhani litawekwa marumaru. Lakini tukitaka kukusalimia tena hatutakutafuta kaburini kwako. Tutakutafuta kwenye nyoyo za watu uliowagusa na kuwasaidia. Na ni wengi kweli. Kumbukumbu yako itabaki kwenye nyoyo zao na kwenye mafanikio yao. Watoto wako hawapo peke yao. Watalia sana, lakini ni kwa muda tu; kwasababu watafunikwa kwa upendo wetu sote na watafarijika, na watakuwa na fahari, kwa jinsi unavyosemwa na unavyokumbukwa.

Ndugu yangu, nisikuchoshe. Mengine tutaongea tutakapokutana tena kwasababu kwa hakika sisi sote, mmoja mmoja na kwa wakati wetu, kwa kadri ya mipango yay eye aliyetuumba, tutakufuata huko. Miaka yote nimekujua, sijawahi kukuona umepumzika. Pumzika kwa amani kwa sasa – na milele.

Ndimi, rafiki yako,

January Makamba

27 Februari 2019
Ujumbe huu ameuandika katika ukurasa wake wa Instagram

Na Steve Nyerere2

Kwanza nichukue fursa hii kuipongeza Azam Cinema Zetu kwa ubunifu mzuri kwenye suala hili la kuwatunuku wasanii wa filamu wanaofanya vizuri kwenye tasnia hii ya filamu Nchini.

Lakini pili, nitoe pongezi kwa wasanii wote ambao walishiriki kwenye ushindani wa Tuzo hizi za Cinema Zetu hapo jana (Jumamosi Februari 23, 2019).

Katika jambo lolote lile suala la utaratibu ni jambo muhimu sana kufatwa na hakuna anayebisha kwenye hili, ila huo utaratibu lazima uwende na uhalisia.

Jana yametokea mengi sana ya kufurahisha na kusikitisha kwenye Tuzo zetu ambazo zimeanza kuchukua umaarufu mkubwa hapa nchini.

Tunajua jambo hili bado ni geni kwenu Azam na tunaamini kabisa bado mna nafasi ya kulifanya kuwa bora kabisa na lenye heshima kubwa sana kwa Azam, Wasanii na Taifa kwa ujumla.

Mimi leo nataka nizungumzie maeneo matatu tu na ikiwapendeza mnaweza kurekebisha.

Kwanza, namna ya utoaji tuzo zenyewe, nani anashindanishwa na nani. Huwezi kusema msanii bora wa kike au wa kiume ukawashindanisha wasanii wakongwe na wasanii ambao wamecheza movie moja tu na hapohapo huyo aliyecheza movie moja ameshinda.

HAPANA lazima kuna sehemu mlikosea waandaji, na mnaweza kumpa mtu bichwa akajiona yeye ni msanii mkubwa sana maana ameshindanishwa na msanii mkubwa sana na amemshinda wakati kiuhalisia hawafanani hata kidogo kiuwezo na kila kitu.

Mimi nahisi mngeongeza vipengele hata cha msanii bora anayechipukia na siyo kufanya kama mlichokifanya jana kwangu mm naona kama ni udhalilishaji.

Hapa lazima waandaji mkae na kujitathmini maana watu wakichukizwa na jambo linalofanywa na kituo kikubwa kama Azam linaweza kusababishia watu kuichukia na brand yenyewe ya Azam kwahiyo umakini kwenye hili jambo unatakiwa uwe mkubwa sana. Lakini pia kwenye hili si vibaya nyie mkawa wasimamizi wakuu lakini mkachukua watu maalum wa kuwasimamia kitaalam zaidi maana mkitaka mfanye kila kitu nyie mnafeli, msichukulie kila kitu ni rahisi (simple) au kubana matumizi NO, chukueni wataalamu wa kuandaa shughuli kubwa kama hizi au kwa kizungu wanasema ku (outsource ) wabobezi wa shughuli kubwa kama hizi na wanakuwa na nyinyi kuanzia mwanzo wa maandalizi mpak mwisho hili naomba mlifanyie kazi.

Pili, haiwezekani watu wakajaa vile mpaka wakakosa viti WHY? Kama kadi
Ndugu wananchi, kumekuwapo na wizi mkubwa wa dawa za wagonjwa katika madirisha ya kuchukuliwa dawa hospitalini, wizi huu unafanywa na watoa dawa hasa kwa wagonjwa wanaotumia bima za afya, watoa dawa hawa huwa hawawapatii wagonjwa dawa zote ambazo anakuwa ameandikiwa na daktari na mda mwingine hufikia hatua hata kutokutoa dozi kamili katika dawa anazokupa, kwa mfano, daktari amekuandikia dawa 3 anakuambia umeandikiwa 2, kama umeandikiwa 5 anaweza kukuambia umeandikiwa 3, dawa zinazobaki anachukua yeye, huu ni wizi mbaya unaogharimu afya za watu, huu ni uuaji.

HATUA ZA KUCHUKUA.

1. Tusambaziane ujumbe huu ili kila mmoja adhibiti wizi huu na kuzuia madhara ya vifo yanayosababishwa na watoa dawa hawa.

2: Daktari anapokuandikia dawa hakikisha unamuuliza jumla ya dawa alizokuandikia ili kuhakisha unapatiwa zote katika dirisha LA dawa.

3: Endapo unamfahamu muhalifu yeyote wa namna hii mripoti polisi ili achukuliwe hatua za kisheria.

Zuia vifo visivyo vya lazima kwa kuhakikisha unapatiwa dozi kamili na dawa zote ulizoandikiwa na daktari.

Tusambaze ujumbe huu ili kuumbua uhalifu huu unaofanywa na watoa dawa hawa.
Sehemu ya Mataluma ya Reli yaliyoppo katik autekelezaji w amradi wa ujenzi wa Reli sgr Katika eneo la Soga Mkoani Pwani

Na. HABIB MCHANGE.

Ninamfahamu vema sana Zitto Kabwe, nina hakika kabisa hoja yake aliyoitoa leo kuhusu ujenzi wa reli ni ama hajui anachokisema au anaendelea na utaratibu wake ule ule wa kujifanya anajua kila kitu kuliko mtu yeyote hapa nchini

Kwa muda sasa Zitto amekuwa akipambana kuuaminisha umma kuwa ni yeye tu ndio Mtanzania mwenye akili kuliko mtu yeyote, mwenye kujua kila kitu kuliko mtu yeyote, mjanja kuliko kila mtu na ndie mwanasiasa mwenye kujua kuliko mwanasiasa yeyote kiasi cha kuwaona wenzake wote vilaza

Sisi tunaomfahamu Zitto na wenzake hatupati shida kuhangaika kumjibu anaporopoka maneno yake na data zake za kuunga unga

Zitto leo amesema serikali inakwamisha mradi liganga na mchuchuma kwa madai ya kitoto kabisa

Ama Zitto amesahau kuwa amekuwa kiongozi msimamizi wa Rasilimali mwenyekiti wa PAC kwa miaka mingi kuliko Mtanzania yeyote ikiwemo hiyo liganga na mchuchuma na wala hakuna cha maana alichoifanyia migodi hiyo mpaka leo



Pengine pia hajui kuwa serikali hainunui reli, hainunui taruma wala hainunui kitu chochote katika mradi wowote unaoendelea na badala yake manunuzi hufanywa na mkandarasi aliyeshinda zabuni na hivyo ni wajibu wake kuamua anunue nini wapi na kwanini huku serikali kazi yake ikiwa ni kuhakikisha inapatiwa huduma kwa kadri ilivyo kwenye mkataba

Leo Zitto hajui haya au porojo tu kama jana na juzi?.... anataka watanzania tushiriki kugombea tender zinazogombewa na makampuni ya kusambaza na kuuza chuma kweli?

Tumpuuzeni tu aisee na tuendelee kumuunga Mkono Rais Magufuli kwa kazi hii iliyotukuka anayoifanya

Nina hakika Zitto hana ufahamu wa kinachoendelea Site kuhusiana na mradi huu wa SGR.

Nimepita bahati ya kutembelea maendeleo ya mradi mkubwa na wa kihistoria wa ujenzi wa Reli yetu ya kisasa tena ya umeme wa Standard Gauge uliopangwa kujengwa kutoka DAR mpaka Mwanza na baadae kigoma na maeneo mengine ya nchi mradi ambao umewekwa kutekelezwa kwa awamu kadhaa huku awamu ya kwanza ikiwa ni DAR mpaka Morogoro KM 205 za njia kuu ya reli na zaidi KM 95 za mapishano na shughuli nyingine muhimu

Naomba nikiri hadharani, kabla sijaenda kujionea kinachoendelea Site akili na mtazamo wangu juu ya mradi huu yalikuwa kama Zitto na wengine wanavyowaza.

Sikuwa nikijua kuwa mradi huu umeenda kuzalisha maelfu ya ajira za moja kwa moja kwa vijana na watu wa rika nyingine hapa nchini.

Sikuwa nikijua kuwa mradi huu umeongeza kwa kiasi kikubwa sana mnyororo wa kiuchumi

Nimeshuhudia kwa macho yangu tena zaidi ya mara moja namna vijana wa kitanzania wakitengeneza Mataruma yanayotumika kujengea reli hii muhimu ya kihistoria

Nimeona kwa macho yangu vijana wa kitanzania wakipata ujuzi wa kukunja nondo kitaalam zinazotumika katika maeneo mbalimbali ya ujenzi

Nimeona kwa macho yangu namna ambavyo mradi huu umeongeza kwa kiasi kikubwa sana uhaba wa saruji hapa nchini kutokana na uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo katika ujenzi wa mataruma, madaraja, nguzo na majengo mengine.

Mradi huu umenionyesha kwa sababu gani Nondo zimepanda bei mtaani kutokana na uhitaji wake mkubwa kwenye ujenzi wa mradi,

Kwa kifupi kabisa,kama Mtanzania nimefurahi sana kuona mradi unatumia malighafi na bidhaa zilizotengenezwa ndani kwa zaidi ya asilimia 50 ya mahitaji yake

Zaidi nimefurahi kuona Mataruma yanayotandikwa katika reli hii yanatengenezwa Tanzania katika kiwanda cha mataruma kilichopo Soga na baadae kiwanda kingine kitakamilika katika site ya Kilosa

Kifupi tu niseme, kama kuna kitu Magufuli amewahi kukifanya na ataendelea kukumbukwa leo akiwa hai na kesho asipokuwepo basi ni uamuzi huu wa kiume wa ujenzi wa reli hii ya kisasa.

Magufuli ameendelea kutupa heshima sio tu watanzani lakini waafrika kwa ujumla wake kwa uthabiti na ushujaa huu.

Achana na habari ya mafanikio yake ya kihistoria katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo Afya, Elimu Bure, mapambano dhidi ya Rushwa, Ujenzi wa Miundombinu, ununuzi wa ndege na kadharika, Hii ya Standard Gauge ni Heshima itakayodumu vizazi na vizazi.

Tumesoma shule ya msingi na baadae sekondari kuwa reli maarufu nchini inayoanzia Dar mpaka Kigoma ikipita pia mwanza kutokea Tabora (Reli ya Kati) ilianza kujengwa na wakoloni wa kijerumani kati ya miaka 1905 na kuendelea.

Leo JPM ameamua kufuta historia hiyo ya wakoloni na kuandika historia mpya. Naam historia mpya hii inaandikwa kwa kutumia fedha za ndani tena bila hofu wala wasiwasi wowote

Magufuli ametufanya tutembee kifua mbele.

Ukianza safari pale stesheni ukaona jinsi watu wanavyopiga kazi, vyuma vikigongana, magari yaliyobeba materials yakiwajibika utaelewa nini ninachokisema

Ukisogea shauri moyo ilala ukashuhudia ujenzi wa daraja la juu la zaidi ya Kilomita mbili na nusu litakalobadilisha pia mwonekano wa jiji la DAR,

Ukaambaa ambaa na reli ukafika Pugu na kushuhudia ujenzi wa stesheni ya kisasa ya eneo hilo lililo kilomita 20 kutoka stesheni hakika utasema Magufuli ANATENDA

Akitoka pugu akaambaa ambaa na njia ya mkandarasi inayojenga reli hiyo kuelekea soga, njiani utajionea mwenyewe namna miamba ilivyopasuliwa, milima imechongwa tuta limewekwa kwa ustadi nakuhakikishia hautatamani kuacha kumpongeza JPM

Ukifika Soga ukaona kambi ya ujenzi wa reli hiyo, ukaona namna mataruma yanavyotengenezwa, ukaona reli iliyotandazwa juu ya tuta na ukasogea pembeni ukaona nyasi za kisasa zilizooteshwa kudhibiti uharibifu wa mazingira hauwezi kuelewa wala kusikiliza POROJO ZA ZITTO na wenzake

Ukisogea mbele ya soga kuelekea Ruvu, ukakutana na Daraja kubwa la upana wa mita 11 na upana wa zaidi ya mita 6 linalotenganisha barabara na treni huku treni ikipita juu barabara chini, nakuambia Zitto na wenzake wote wa aina yake lazima uwapuuze kama sio kuwadharau kabisa

Hebu sogea Ruvu basi kidogo, nenda kajionee namna maji yalivyofinyangwa finyangwa kuweka njia ili mitambo ipite wewe, Zitto huwezi muamini tena

Sogea basi Kwala pale, ujionee eneo kubwa linalojengwa Marshalling Yard eneo ambalo zaidi ya treni yenye urefu wa kilomita mbili zinaunganishwa na kupishana huku pembeni kidogo pakiwa na bandari kavu, halafu Zitto na wenzake wanaleta hadithi za Arifu lela olela?

Toka Kwala sasa sogea mpaka Ngerengere uone shughuli nyingine zinazoendelea, njoo mpaka Moro mjini ujionee mitambo inavyofanya kazi halafu usikilize takataka za kina zitto hizi, utatamani kutema mate chini.

Toka Moro elekea Dodoma kupitia Kilosa na GULWE, angalia namna ambavyo wanaume wanachoronga milima ya kilosa ili kupitisha Treni mita 90 Ardhini, halafu wahuni wachache wanasemaje?

Njoo mpwapwa uone namna vijana wanavyopiga kazi mchana na usiku kuelekea Ihumwa. Weweeee? Acheni tu jamani

Hapo sijakueleza kuhusu idadi ya ajira zilizozalishwa, unaambiwa zaidi ya watanzania 5900 wameajiriwa kufanya ujenzi wa mradi huu utakaodumu na kudumu katika akili za watanzania

Sijakwambia kuhusu madaraja, njia za juu, njia za chini, vivuko, majengo ya stesheni na mambo mengine.

Sijakwambia pia juu ya namna elimu inavyopandikizwa kwa wazawa wanaoshuhudia ujenzi wa mambo mbalimbali kutoka kwa wataalam wa kimataifa.

Kuendelea kuwasikiliza wapotoshaji wa aina ya Zitto ambao wao kila kitu wanataka kufanya siasa ama kiki ni kujipotezea muda tu. Standard Gauge inajengwa kwa kasi ya ajabu na mwaka 2020 Zitto na wenzake watasafiri na reli hiyo hiyo wanayoionea donge

Ndimi tena
Habib Mchange
0762178678
Morogoro, Tanzania