Wednesday, July 23, 2014

TOFAUTI ZA DINI ZISIWAGAWE WATANZANIA - MWINYI

 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.
 Rais wa Tanzania wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akisisitiza umuhimu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
 Baadhi ya akina mama na watoto waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na watoto wanaotoka katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima vya jijini Dar es salaam , wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi mbalimbali wakati wa Futari aliyooiandaa jana usiku katika viwanja vya Karimjee.
 Baadhi watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam wakijumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (wa pili kutoka kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Na Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es salaam.

Rais mstaafu wa awamu ya pili , Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao.

Kauli hiyo ameitoa jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.

“Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu” Amesisitiza.

Amewashukuru viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa mvua jijini Dar es salaam.

Bw. Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.

Amezitaka mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika maeneo hayo.

Katika hatua nyingine Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.

Amezitaka mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi.

Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na kuendelea kuvumiliana.

SAMAHANI KWA PICHA ZA KUTISHA; MKE WA MTU NI SIMU: MWANAUME MMOJA APIGWA SULULU BAADA YA FUMANIWA, MWANZA

 Shoka ikiwa imezama kichwani.
Jamaa akiwa kwenye ungalizi madokta wakihangaika kumfanyia upasuaji ili waweze kutoa sululu aliyokuwa imezamishwa kichwani. Baada ya madaktari wa Hospitali ya Bugando kupambana kuokoa maisha ya jamaa aliye fumaniwa huko Mwanza hatimaye wamefanikiwa kumtoa sululu hiyo kichwani na hali yake si nzuri.

MEYA WA ILALA JERRY SILAA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA UKONGA KUELEKEA MAZIZINI MPAKA MOSHI BAR

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huo ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90. Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu. Picha Zote Na Dj Sek Blog
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa  kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.

MKE WA POLISI AFIA NYUMBANI KWA DEREVA WA BODABODA

Na Mwandishi Wetu, Moshi. 

Jeshi la Polisi linamshikilia dereva mmoja wa pikipiki, maarufu kama bodaboda wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro baada ya mke wa askari polisi kukutwa amekufa chumbani kwa dereva huyo.

Tukio hilo ambalo limezua gumzo kubwa wilayani humo lilitokea juzi saa 12:00 jioni katika eneo la New Mwanga wilayani humo na mtuhumiwa akidaiwa kukutwa akiwa amelewa chakari.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea.

“Hilo tukio lina ukweli na bahati mbaya sana mumewe ndiyo kwanza amehamishiwa Geita na alikuwa akaripoti halafu aje kuchukua familia yake,” alisema Ndemanga.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, alisema hadi sasa haijafahamika nini kilitokea na kwamba hilo ni moja kati ya mambo ambayo polisi inachunguza.

“Hayo yote kwamba ilikuwaje akawa chumbani kwa huyo kijana, nini sababu za kifo yatajulikana kadiri upelelezi unavyoendelea,” alisema.

Imeelezwa kuwa jana ilikuwa siku ya askari huyo kuripoti katika kituo chake kipya cha kazi.

“Mpaka sasa hivi haijajulikana nini hasa kilitokea huko chumbani na ilikuwaje akawa chumbani kwa huyo dereva,” alisema mmoja wa watu waliokuwapo katika eneo la tukio ambaye hata hivyo, hakutaka kutaja jina lake na kuongeza kuwa jana saa sita mchana, mwili wa mwanamke huyo ulichukuliwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mwanga na kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi.

Taarifa za awali zinasema kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na mikwaruzo shingoni hali inayotia shaka kuwa huenda alinyongwa.

Habari nyingine zinadai kuwa siku ya tukio, mwanamke huyo alikuwa ameaga kuwa anakwenda kanisani lakini baadaye simu yake ilipopigwa ilikuwa ikipokewa na mwanamume.

Ilidaiwa kuwa mume wa marehemu alipojaribu kupiga simu ya mkewe, ilikuwa ikipokelewa na mtu aliyeonekana kuwa ni mlevi wa kupindukia hali iliyomtia wasiwasi na kuamua kuwapigia simu marafiki zake wa karibu ili wamsaidie kumtafuta ndipo walipopata taarifa kuwa ulikuwapo uhusiano kati ya shemeji yao na dereva huyo wa bodaboda.

Ilidaiwa kuwa marafiki hao walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa dereva huyo wa bodaboda ambako walimkuta akiwa amelewa na walipoingia ndani walimkuta shemeji yao akiwa ameshafariki dunia.”

TABIA 27 ZA WANAUME/­ WAVULANA WANAOJUA KUPENDA

1. Hupiga simu mara kwa mara kumuulizia mpenzi wake anaendeleaje.

2. Hujihisi vibaya pale anaposahau siku ya kuzaliwa (birthday) au siku mliyoanza mahusiano (anniversary) na huomba msamaha.

3. Hushukiza na zawadi mbalimbali hata kama sio muda maalumu.

4. Mara kwa mara hukuambia "NAKUPENDA">>>"I Love You".

5. Anajua kufanya mapenzi na wewe.

6. Anajua jijnsi ya kujali, kukumbatia, kuchumu na kutimiza mahitaji ya kimahaba kwa mpenzi wake.

7. Huhisi kuumia pale mpenzi wake anapopitia hali ngumu.

8. Hupenda kuona mpenzi wake ana furaha na hutamani kufurahi pamoja.

9. Siku zote hutafuta muda mzuri kutumia pamoja na mpenzi wake.

10. Kamwe hawezi kumpiga au kumuumiza kisaikolojia mpenzi wake.

11. Huoa bila kusubiria sanaaaa...

12. Husamehe na kusahau pale anapoumizwa hisia zake.

13. Hatotumia siri au udhaifu wako kukufanyia mabaya.

14. Hatotangaza kama mpenzi wake ana madhaifu fulani.

15. Ni mvumilivu na tayari kufanyia usulihisho kwenye matatizo ya uhusiano wake.

16. Anajua kwamba ni muhimu kwa mpenzi wake kutumia muda wake akiwa na marafiki zake, ndugu na familia yake.

17. Kamwe hawezi kutoka nje ya uhusiano wenu ( will not cheat on you).

18. Hawezi kuwachokoza marafiki zako wakike mpaka point ambayo itakuwa inakuboa au kukupa mashaka.

19. Hawezi kwenda nje ili mfanye mpenzi wake apate wivu.

20. Humheshimu mpenzi wake pale awapo na marafiki na familia yake.

21. Humsaidia mpenzi wake na kazi mbali mbali (mfano za nyunbani au masomo).

22. Hufurahia kampani ya marafiki na ndugu wa mpenzi wake.

23. Husaidia kufikia malengo na kutimiza ndoto za mpenzi wake.

24. Kamwe hakatishi tamaa mpenzi wake pale wanapokuwa wanaongea.

25. Hujali sana kuhusu mawazo, hisia na ushauri wa mpenzi wake.

26. Mara nyingi huwepo pale mpenzi wake anapohitaji msaada.

27. HUJUA KWAMBA NJIA YAKE SIO NJIA PEKEE...

Imeletwa kwenu na Fred Kihwele.

WALIMU WAGOMA KUPUGUZIWA MAFAO YAO YA KUSTAAFU

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Gration Mkoba akitoa taarifa ya chama hicho kwa waandishi wa habari leo kuhusu Mchakato na Mgogoro kati ya Chama hicho na Serikali. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa CWT Mwl. Ezekiel Oluoch.
---
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog.

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimepinga mpango wa serikali wa kupunguza mafao ya wastaafu ya wanachama wa mifuko ya Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na watumishi wanachama wa LAFP.

Imesemekana mpango huo kama utatekelezwa utapunguza kiinua mgongo cha walimu na watumishi wengine kwa zaidi ya nusu ya kile wanachopata kwa sheria iliyopo.

Akizugumza jijini Dar es salaam rais wa chama hicho, Gration Mkoba amesema kwamba wamepugunza malipo ya Pensheni ya Mkupuo kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 33.3 ya mshahara kwa mwezi kabla ya kustaafu.

Rais huyo ameeleza kuwa sababu kubwa inayotolewa na serikali kuhususiana na kupunguza mafao hayo ni hali mbaya kifedha jambo linalopingwa na wafanyakazi.

Naye mweyekiti wa chama cha wafanyakazi taasisi za elimu ya juu, Emil Karurange amesema kwamba wanaiomba serikali kusitisha zoezi hilo hadi hapo watakapo kaa na kujadili na wafayakazi wao.

Tuesday, July 22, 2014

MTOTO WA MPIGANAJI MICHAEL MACHELLAH, MAREHEMU EVERLYNE MACHELLAH AZIKWA LEO, DAR

 Mwili wa marehemu ukiwasili makaburini.
 Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
 Baba na mama wakiwekla shada la maua.
 Baba wa marehemu, Michael Machellah akiweka udongo katika kaburi wakati wa mazishi.
Mama wa marehemu akiweka udongo.
 Shangazi wa marwehemu akiweka shada la mau.

AIRTEL YAENDESHA SEMINAR ELEKEZI KWA VIONGOZI WA SOKA ILI KUJIANDAA NA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS 2014

Meneja Matuko wa Airtel Tanzania Rebeca Mauma akizunguma wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya washiriki wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars wakifutilia kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiteta na Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo.
Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisisitiza jambo wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu