.jpeg)
●Serikali Yatoa Pole, Yaahidi Hatua za Dharura
TABORA, TANZANIA — Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa salamu za pole kwa familia, ndugu, na jamii nzima ya Mkoa wa Tabora kufuatia ajali ya moto iliyotokea Julai 28, 2025 katika Makao ya Watoto Igamilo, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, na kuua watoto watano.
Kupitia Taarifa rasmi iliyotolewa Julai 29 na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Waziri Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio hilo ambalo limeacha majonzi na huzuni kubwa kwa taifa zima.
"Ni huzuni, ni majonzi. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mzito. Tunawaombea faraja, subira na nguvu katika kipindi hiki kigumu," ilieleza sehemu ya taarifa ya Waziri Gwajima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo. Wizara imesisitiza kuwa wamiliki na wasimamizi wa Makao ya Watoto kote nchini lazima kuhakikisha ukaguzi wa mifumo ya umeme na miundombinu ya kinga dhidi ya majanga ya moto unafanyika mara kwa mara ili kuzuia matukio kama haya.
Serikali pia imethibitisha kuwa watoto waliojeruhiwa katika tukio hilo wanapata matibabu bure, huku wengine wakihifadhiwa mahali salama wakisaidiwa kisaikolojia na kijamii kupitia Maafisa Ustawi wa Jamii na Halmashauri husika.
Wizara imesisitiza kuwa itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa tukio hilo na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuimarisha usalama na ulinzi wa watoto katika Makao yote nchini.














.jpeg)
.jpeg)




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.








