Articles by "MAISHA NA MAHUSIANO"
Showing posts with label MAISHA NA MAHUSIANO. Show all posts
*Awashauri CHADEMA kuacha maandamano

*Asisitiza umoja, mshikamano na maridhiano

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhman Kinana, ameshauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini nia njema aliyonayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maridhiano na kuwatumikia Watanzania.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina ubora wa sheria ya uchaguzi ambayo imepitihswa na Bunge hivi karibuni, baada ya wadau mbalimbali nchini kutoa maoni yao ambapo amesisitiza sheria hiyo ni bora kuliko iliyopo sasa.

Kinana aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na wana CCM na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo mbali ya kutumia muda mwingi kuzungumzia, maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM na CHADEMA pamoja vyama vingine vya upinzani, alisema kuna mambo mengi mazuri yamefanyika.

Alisema mambo mazuzi yamefanikisha kupata mwafaka ingawa CHADEMA haitaki kueleza ukweli ikiwemo serikali kukipatia chama hicho ruzuku ya Sh.bilioni 2.7 ambayo waliikataa kwa miaka mitatu nyuma.

Akielezea kuhusu sheria mpya, Kinana alisema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.

“Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?. Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.

“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu. Hebu tupeleke sheria mpya bungeni na kila hoja aliyopelekewa, aliyoambiwa kwamba haya ndio maoni ya wadau Rais akasema sawa, nakubali.
“Sasa niwasihi ndugu zangu Watanzania, tujipange kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, tujipange kwa uchaguzi mkuu mwaka 2025. Sheria hii ni nzuri, bora kuliko sheria yoyote iliyopo katika historia ya nchi yetu, inakidhi mahitaji na matakwa ya nchi na jumuiya ya madola, inakidhi mahitaji ya nchi za Umoja wa Afrika (AU), inakidhi vile vile mahitaji ya nchi za Kusini mwa Afrika ambao na sisi ni wanachama,” alisema.

Aliongeza kwamba hakuna tume ya miujiza zaidi itakayokuwepo, huku akifafanua kila jambo ambalo litafanyika lazima litakuwa na kasoro moja au mbili, na kuhoji kwani CHADEMA wao hawana kasoro?.

“Wanazo, sasa nawaambia ninyi chama kikuu cha upinzani kuweni basi na ustahimilivu kidogo, uungwana na kusikiliza wenzenu na kuona nia njema iliyopo katika Chama Cha Mapinduzi, kwa na serikali yake,” alisema.

Akifafanua zaidi Kinana alisema kuwa kushinda uchaguzi kunatokana na sera, mipango ya uchaguzi na kusikiliza watu, kwani unaweza kuwa na tume nzuri ya uchaguzi na matokeo yakawa ni ya hovyo, usiyoyataka.

Alitoa mfano wa moja ya nchi jirani ambayo walipigania sana kuwa na tume huru kwa miaka 20, wakaipata, lakini wamegombea mara nne hawakupata.

“Hawakuingia madarakani, wale waliotengeneza hiyo tume hawakupata, sasa wanasema Katiba hii haina maana waifute, wale walioingizwa na katiba baadae nao wakashindwa wanasema katiba hii haina maana. Kwa hiyo aliyeshinda anasema Katiba haina maana na aliyeshindwa naye anasema Katiba haina maana.

“Sasa kushinda uchaguzi sio Katiba tu, Nigeria baada ya wanajeshi kutoka baradakani walitengeneza Katiba mpya mwaka 1969 na kwa sehemu kubwa walienda kuchukua Katiba ya Marekani, tume ya uchaguzi ya Rais inateuliwa na Rais kwa kushauriana na baraza la ushauri.

“Baraza la ushauri ni nani? Rais ndio Mwenyekiti, makamu mwenyekiti ni makamu wa rais, wajumbe wengine marais wastaafu, hapo vipi? Kuna mtu anatoka nje ya mfumo?

“Hao ndio wanateua, mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume, uchaguzi unafanyika na watu wanakubali. Hapa tunatafuta malaika wa kuja kuongoza tume, kila utakachofanya unaambiwa kinakasoro, hivi mnavyoona yote tuliyokubali wanasema hamna kitu.

“Nimesikia wanaandaa maandamano Mwanza, Mbeya na Arusha na mimi nataka niwasaidie kutangaza kama watu wengine hamjasikia. Wanakwenda kueleza haya yaliyopitishwa na CCM na Bungeni hamna kitu.

“Tume si kila kitu, Namibia kamati inatengenezwa baada ya pale anayetua Rais, kuna nchi inaitwa Mauritius na hizi nchi zote ambazo nimezitaja ni za Jumuiya ya Madola, Rais anashauriana na watu wawili tu, anashauriana na waziri mkuu na kiongozi wa upinzani bungeni hakuna mtu mwingine,” alisisitiza.

“India wana mkurugenzi na wana makamishina. Nani anateua? Waziri Mkuu na Baraza lake la Mawaziri kwisha, yaani Rais Samia akae na baraza lake la mawaziri atengeneze orodha ateue, si moto utawaka hapa? Watasema tu maigizo.

“Sasa kuna shida hapa nchini kila unalofanya halina heri ndani yake, lakini vizuri haya mambo tukayaeleza maoni mengine yakatolewa unajua siku hizi kuna watu wanapita bila kupingwa lakini ni vizuri wanaopita bila kupingwa wakapigiwa kura ya ndio au hapana Bunge likasema sawa tumekubali.

“Wanauliza kwa nini? Wanasema kuna watu wengine wanafanya ujanjaujanja wa kupita bila kupingwa, hivyo wapigiwe kura tujue kama wanakubalika Bunge limesema sawa itapigwa kura ya ndio au hapana,” alisema.

KUHUSU MARIDHIANO

Akizungumzia maridhiano ambayo yamefanyika kwa nyakati tofauti, Kinana alisema kuwa wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wasiopungua 400 wako mahabusu wakikabiliwa na kesi zilizotokana na sababu mbalimbali za kiuchaguzi, lakini ulitengenezwa utaratibu wa kisheria waakachiwa huru.

Kinana alisema hakuna maridhiano bila ustahimilivu, Rais alialika taasisi za kidini na kiraia ili waelewane kujiuliza nini wanahitaji kwa lengo la kuhakikisha tunakuwa na taifa liwe la watu wenye mshikamano na kupendana.

Alisema Dk. Samia aliunda tume ya kusikiliza makundi ya Watanzania kusikiliza hoja zao ikiwemo Katiba, lakini mwishowe CHADEMA waligomea kwa sababu zao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (katikati), akizungumza wakati alipokuwa akiukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Matare uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Ikungi wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Juni 6, 2023.

Na Dotto Mwaibale, Ikungi

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amefurahishwa na kuridhishwa na usimamizi mzuri na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na kuwapongeza viongozi wote kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa thamani halisi ya fedha zilizotolewa na Serikali.

Serukamba ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake wilayani humo aliyoifanya leo Juni 6, 2023 ambapo alipata fursa ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhimiza ikamilike kabla ya Julai 1, 2023.

Aidha, Serukamba amewapongeza wataalam na wananchi kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia utalaam na nguvu kazi katika kutekeleza miradi hiyo ambayo imegharimu fedha nyingi.

"Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hii naomba tumuheshimishe Rais wetu kwa kuikamilisha haraka kabla ya Julai 1, 2023 ili ianze kutumika," alisema Serukamba.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imekuwa ikimpa raha kutokana na kufanya vizuri katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwa imekuwa ikipata mafanikio hayo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi, wataalam na wananchi.

Miradi aliyoitembelea na kuikagua ni mradi wa maji katika Kijiji cha Matare uliopo Kata ya Unyahati uliogharimu Sh. Milioni 386.8 ambao utawahudumia wananchi 5036, ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Matare na ujenzi wa mabweni mawili na bwalo katika Shule ya Msingi Ikungi.

Miradi mingine aliyoitembelea na kuikagua ni ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi ya Ikungi B, ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ikungi ambayo sasa imekuwa na kidato cha tano na sita, ukaguzi wa mradi wa Kikundi cha vijana kijulikanacho kama Ikungi Chapakazi ambao unajishughulisha na ufyatuaji wa matofali ambapo aliwataka wana kikundi hicho kurejesha mkopo waliokopeshwa na Halmashauri ya Ikungi ili waweze kukopeshwa vijana wengine.

Aidha, miradi mingine iliyokaguliwa na kuhimiza ikamilike haraka ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi ya Dung'unyi na ujenzi wa barabara ya Ikungi- Matongo yenye urefu wa kilometa moja.


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akipokea taarifa ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Matare.
Muonekano wa madarasa yanayo jengwa Shule ya Msingi Matare.
Muonekano wa kazi nzuri ya utunzaji wa mazingira katika Shule ya Msingi Matare inayofanywa na walimu wa shule hiyo kwa kuwashirikisha wanafunzi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (katikati) akiwa na viongozi wengine wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (mbele) akiongoza msafara wa viongozi mbalimbali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo kuelekea kutembelea jengo la Ustawi wa Jamii linalo ratibu na kusimamia shughuli za upingaji wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike na kiume na wanawake katika Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (mbele) akiongoza msafara wa viongozi mbalimbali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo kuelekea kutembelea jengo hilo.Muonekano wa jengo hilo.
Muonekano wa mabweni mawili yalio jengwa Shule ya Msingi, Ikungi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mabweni mawili na Bwalo katika Shule ya Msingi Ikungi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson.
Muonekano wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Ikungi B
Taswira ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ikungi.
Mhandisi wa Wilaya ya Ikungi, Edward Millinga (katikati), akitoa maelezo ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ikungi. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi
na wa pili ni Mkuu wa Shule hiyo, Madamu Neema Stephano.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (katikati) akiongoza msafara wa viongozi mbalimbali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Barabara ya Ikungi-Matongo.
Taswira ya mradi wa vijana Chapa kazi Ikungi, unaojishughulisha na ufyatuaji wa matofali.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Zilfat Muja (katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida (wa wanne kutoka kushoto) kuhusu mradi huo. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Ikungi, Haika Masawe, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mwanahamisi Omari, Mkuu wa wilaya hiyo, Thomas Apson na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga.


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoka kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Dung'unyi wakati wa ziara hiyo. Katikati ni Diwani wa Kata hiyo, na kushoto kwa diwani ni Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Yahaya Njiku.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati uzinduzi wa Filamu ya Tanzania'The Royal Tour' ambapo hafla ya Uzinduzi wa Filamu hiyo unafanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo Mei 8, 2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari wamewasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere tayari kwa ajili ya Uzinduzi wa Tanzania The Royal Tour ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Watanzania wa sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii kujitayarisha kupokea watalii watakaokuja kutalii nchini.

Ametoa rai hiyo leo Mei 8, 2022 wakati akizindua filamu ya Royol Tour katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzinduliwa rasmi nchini Marekani, kisha jijini Arusha na baadae Zanzibar.

“Mategemeo yangu baada ya filamu hii kuzinduliwa Tanzania inatakiwa kujitayarisha kupokea wageni wengi, wageni watakuwa wa tofauti tofauti hizo hata watakapokuja watakaa katika hoteli za tofauti.

“Hivyo nitoe rai kwa sekta za utalii kujitayarisha ili watalii wakija wakute hoteli zipo, wakute watu wa kupokea wageni wapo, wapokea wageni viwanja vya ndege nao wajiandea.

“Zile sifa ambazo zimeoneshwa kwenye filamu lazima uonekane, tunapaswa kujitayarisha, watu wa sekta ya utalii na sekta nyingine tujitayarishe, narudia tena lazima Watanzania wote tujitayarishe,amesema Rais Samia.

Aidha amesema kuzinduliwa kwa Filamu ya Royol Tour ni mwanzo tu wa kuzindua filamu nyingine za Royal Tour awamu ya pili na ya tatu kwani kuna picha nyingi ambazo zilichukuliwa ambazo zitatumika kutengeza filamu nyingine kwa lengo la kendelea kutangaza utalii wa Tanzania.

“Filamu hii ya Royal Tour ni mwanzo tu kwani nyingine zitakuja.Nimpongeze Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa ushiriki wake mzuri kwenye filamu hii na amekuwa na msemo wake kuwa yajayo yanafurahisha, hivyo tuseme yajayo yanafurahisha”amesema Rais Samia.
Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani kulia akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati akitoa taarifa kwa Umma Juu ya uwepo wa upungufu wa upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi kwa Wakazi wa Jiji la Tanga kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Rogers
Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani kulia akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati akitoa taarifa kwa Umma Juu ya uwepo wa upungufu wa upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi kwa Wakazi wa Jiji la Tanga kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Rogers Machaku
AFISA Uhusiano wa Tanga Uwasa Dovetha Mayala akisisitiza jambo
Sehemu ya waandishi wa Habari wakifuatilia matukioo mbalimbali kwenye mkutano huo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) imeeleza sababu za kuanza kwa mgao wa maji katika Jiji la Tanga kwamba inatokanana na kiasi kilichopo cha maji yanayozalishwa kiweze kusambazwa na kupatikana kwa watu wote .

Hivyo kusababisha uwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika maeneo ya Jiji la Tanga lenye wakazi wapatao 316,055 Tangu mwishoni mwa mwezi Septemba 2021.

Mgao huo unatarajiwa kuanza Octoba 9 mwaka huu katika maeneo ya Nguvumali, Kisosora,Mwamboni, Chumbageni, Kwaminchi,Chuda,Gofu,Ngamiani,Central,Bombo,Raskazone,Sahare,Usagara na Makorora.

Maeneo mengine yatakayoathirika na mgao huo ni Duga, Magomeni, Mabawa, Mwakizaro, Msambweni, Donge, Magaoni,TangaSisi, Mwang’ombe, Mwakidila, Mwahako, Masiwani, Mbugani, Machui, Tongoni, Kiwavu, Maere, Kivindani, Mtakuja na Kange Kasera.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani ambapo alisema hilo linatokana na kwa kuzingatia majira ya mwaka Jijini Tanga ambapo kipindi cha kiangazi huanza mwezi Agosti hadi Novemba kila mwaka.

Alisema ambapo kipindi hicho matumizi ya maji huongezeka na hivyo kujitokeza kwa upungufu wa maji maeneo mengi kutokana na maji yanayozalishwa kutokukudhi mahitaji ya maji kwa watu wote Jijini Tanga kwa kipindi hicho.

“Upungufu huu unatokana na ukomo wa uzalishaji maji wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji Mowe kwani uwezo wa kuzalisha na kusambaza maji ni wastani mita za ujazo 30000 kwa siku wakati mahitaji ya maji wakati wa kiangazi yanakadiriwa kufikia wastani wa mita za ujazo 37100 kwa siku.

Alisema mgao huo umezingatia uwepo wa maeneo mengine yenye ofisi za Umma,Vituo vya Afya ,Hospitali pamoja na taasisi za elimu ambako muda mwingi wa mchana huduma ya maji inabidi iwepo.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Meneja Ufundi wa Tanga Uwasa alisema kufuatia changamoto hiyo Rais Samia Suluhu pamoja na jitihada za Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu na ufuatiliaji makini wa karibu wa Waziri wa Maji Jumaa Aweso.

Alisema jitihada hizo zimeiwezesha Tanga Uwasa kupata fedha kiasi cha Sh.Bilioni 9.8 ili kutekeleza mradi mkubwa unaolenga kuongeza uwezo wa uzalishaji na usambazaji wa maji kutoka mita za ujazo 30,000 hadi 45,000 kwa siku ambapo ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Agosti mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Justice Kijazi, akizungumza kwenye kikao kazi cha tathmini ya hali ya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto wilayani humo jana kilichoshirikisha wanawake 120 waliokutanishwa na Shirika la SPRF chini ya ufadhili wa FCS ili kujadili namna bora ya kutokomeza matukio hayo kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) Dkt. Suleiman Muttani akizungumza kwenye mkutano huo ulioshirikisha wanawake 120 kutoka vijiji 12 kuzunguka wilaya ya Ikungi, Singida. 
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali zilizojikita katika kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.
Kikao kazi cha vikundi vya uhamasishaji kwa Sauti Ya Mwanamke na Sauti ya Mwanafunzi kikiendelea.
Maafisa Watendaji wa Shirika la SPRF wakifuatilia matukio yanayoendelea kwenye kikao hicho.
Jeshi la Polisi likishiriki ipasavyo kikao hicho.
Mmoja wa waratibu wa mradi wa Aware, Bernard Maira akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Sauti ya Mwanamke kwenye moja ya makundi ya uhamasishaji akizungumza.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi, Beatrice Maeda akizungumza.
Kikao kikiendelea.
Moja ya kikundi cha Uhamasishaji cha Sauti ya Mwanamke wilayani Ikungi wakieleza moja ya tukio la ukatili wa kijinsia walilofanikiwa kuliibua.

Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojikita zaidi katika mlengo wa shughuli za kupunguza umaskini kwa afya na ustawi nchini (SPRF) kupitia mradi wake wa ‘Aware’ jana limewakutanisha wanawake 120 kutoka vijiji 12 vya wilaya ya Ikungi, mkoani hapa kwa lengo la kuwaimarisha kuweza kukabiliana ipasavyo na matukio ya ukatili.

Jumla ya matukio ya ukatili wa kijinsia 104 yameripotiwa kufanyika ndani ya Wilaya ya Ikungi kwa kipindi cha kati ya Julai 2019 hadi Novemba 2020, ambapo kati ya matukio hayo 56 yalijitokeza katika kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, huku matukio mengine 48 ya aina hiyo hiyo yakijitokeza kipindi cha Machi hadi Novemba 2020.

Kwa mujibu wa SPRF chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) imebainika kuwa kati ya matukio hayo 56 yaliyoripotiwa kutoka vijiji 12 vya mradi huo kwa kipindi hicho cha Julai 2019 hadi Februari 2020 ni kesi 2 ndizo zilizofikishwa kwenye ngazi ya mahakama, na kati ya hizo kesi moja pekee ndiyo iliyotolewa hukumu.

Matukio mengine 7 ya ukatili yaliyoripotiwa yaliishia kwenye Kituo cha Polisi Ikungi kutokana na kukosa vielelezo na ushahidi shawishi, huku kesi 4 zikikomea kwenye vituo vidogo vya polisi, 7 kwenye ngazi za kata, 16 ngazi ya vijiji, 5 ngazi ya vitongoji na 14 zikiishia kutatuliwa kindugu kwenye ngazi ya familia.

Aidha, kwa upande wa matukio 48 yaliyojitokeza kwenye kipindi cha Machi hadi Novemba 2020 ni kesi 2 pekee ndizo zilizofikishwa na kuamriwa kwenye ngazi ya mahakama, huku matukio mengine 11 yakiishia Kituo cha Polisi Ikungi, 5 vituo vidogo vya polisi kwenye maeneo hayo, 1 ngazi ya kata, 12 vijiji, 6 Ustawi wa Jmii Wilaya, 2 Vitongoji na 7 zikiishia kutatuliwa kindugu kwenye ngazi ya familia.

Wakichangia ripoti hiyo kabla ya kufikia maazimio, baadhi ya wanawake kutoka kwenye majukwaa ya Sauti za wanawake na Sauti za Wanafunzi wilayani hapo walisema bado kuna udhaifu mkubwa katika kushughulikia utekelezaji wa sheria zinazopinga vitendo vya ukatili.

“Suala hili limeendelea kuwa sugu na linalochochea ongezeko la matukio ya kufedhehesha, undugu, ujamaa na urafiki ndio chanzo kikubwa kinachoathiri mwenendo wa mashauri haya ya ubakaji, ndoa za utotoni na mimba za umri mdogo hasa pale tunaporuhusu yamalizwe kwenye ngazi za familia,” alisema mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Anna Heneriko.

Mwingine Pili Hussein alisema kesi nyingi zimekuwa zikimalizwa kwenye ngazi ya vituo vya polisi na kwa maaafisa watendaji. Lakini kubwa zaidi kuna uvujishaji mkubwa wa siri kwa watoa taarifa jambo ambalo linafifisha hamasa ya mapambano dhidi ya vitendo hivyo. 

Kupitia mkutano huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Justice Kijazi aliwataka maafisa wa ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria katika kuhakikisha mashauri yote yanayoripotiwa yanafikishwa kwenye ngazi za utatuzi wa kisheria.

“Niwahakikishieni mama zangu wote mliopo hapa serikali yenu chini ya Rais John Pombe Magufuli ni sikivu sana, na inakwazwa sana na aina yoyote ya uhalifu na uvunjifu wa sheria kwa makusudi. Nimeguswa sana na matukio haya yanayofedhehesha mama zetu na watoto wetu…chukueni namba zangu za simu ili yeyote kati yenu atakayeona tukio lolote la ukatili likitendeka anijulishe,” alisema Kijazi

Aidha, Kijazi aliwataka aliwataka maafisa Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanashughulikia kikamilifu kesi za matukio yote ya ukatili yanaripotiwa kwa utimilifu unaozingatia matakwa ya kisheria kwa minajiri ya kutokomeza kabisa vitendo hivyo, sambamba na kuwezesha haki kuonekana kutendeka.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Ikungi kupitia mkutano huo liliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha pindi matukio hayo yanapojitokeza, na hasa kutoharibu wala kuwashawishi wahanga kuficha ushahidi ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe pindi matukio hayo yanapojitokeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SPRF, Dkt. Suleiman Muttani alisema lengo la kikao hicho ni kutaka kuyaimarisha kiutendaji majukwaa ya vikundi vyote vya uhamasishaji dhidi ya matukio ya ukatili, ikiwemo kundi la Sauti ya Mwanamke katika kuendelea kushirikiana na majukwaa mengine kutetea haki za wanawake na watoto.

“Azma ya mradi huu wa ‘Aware’ ni kuona mifumo ya serikali za mitaa imeimarika kwa kupokea na kuitikia kwa haraka utekelezaji wa mahitaji ya jamii hasa matakwa ya wanawake, watoto na makundi mengine athirika kuona wanatambua suala la ukeketaji, ndoa za utotoni, ukatili kwa wanawake na unyanyasaji kwa watoto haukubaliki,” alisema Muttani 

mpaka sasa kati ya matukio yote hayo yaliyoibuliwa kwa ushirikiano wa majukwaa yake mbalimbali ikiwemo Sauti ya Mwanamke, Sauti ya Mwanafunzi, Kamati za Mtakuwa na Wanaume Washawishi ndani ya Vitongoji na Vijiji ni kesi 48 pekee ndizo zilizofika kwenye ngazi za utatuzi huku nyingine utatuzi wake ukiishia kwenye ngazi za familia.