Articles by "SIASA"
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Wananchi wa Kijiji cha Mkungugu jimbo la Ismani katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakiwa katika foleni ya kupiga kura ya kumchagua Mbunge wao katuika uchaguzi mdogo uliyofanyika leo Juni 01, 2026.
Mwananchi Mkazi wa wa Kijiji cha Kihongorota katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa, Angelista Mwenda akipiga kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Ismani uliofanyika leo Juni 01, 2026.
Mwananchi Mkazi wa wa Kijiji cha Kihongorota katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa, Angelista Mwenda akipiga kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Ismani uliofanyika leo Juni 01, 2026.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akipita kuingia katika kituo cha Kura cha Ofisi ya Kijiji Mtera katika jimbo la Ismani Wilaya ya Iringa mkoani Iringa kukagua mwenendo wa zoezi la kupiga kura kwa wananchi wa Ismani lililofanyika leo Juni 01, 2026.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Mawakala katika moja ya vituo alivyotembelea.
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amesema zoezi la upigaji Kura wa Ubunge katika jimbo la Isman katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara limekwenda vizuri.

Mwenyekiti huyo wa Tume Jaji Mwambegele amesema hayo leo Juni 01,2026 akiwa katika ofisi za Kijiji Igingilanyi Wilayani Iringa mara baada ya kutembelea na kukagua zoezi la upigaji Kura linavyoendelea katika vituo vya kupigia Kura vya jimbo la Isimani ambako kunafanyika uchaguzi mdogo wa ubunge.

Amesema mwitikio wa wananchi wa Ismani katika kujitokeza kupiga kura umekua mkubwa na hata katika Kata nyingine 12 ambazo nazo zinachagua Madiwani hii leo wamejitokeza kwa Wingi.

Mwenyekiti huyo wa Tume Jaji Mwambegele ameshudia upigaji kura kwa baadhi yavituo vilivyopo katika vijiji vya Igingilanyi, Mkungugu, Kihongorota na Migori.

Kata 12 zilofanya uchaguzi leo ni Mzimuni iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni; Zongomera, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji Kasulu.

Nyingine ni Kata ya Kala iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Kibiti, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la kupiga kura kwa wananchi wa Jimbo la Ismani lililopo Halmashauri ya Iringa mkoani Iringa hii leo Juni 01,2026.


Wananchi wakiwa katika mistari tayari kuingia vituoni kupiga Kura.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la kupiga kura kwa wananchi wa Jimbo la Ismani lililopo Halmashauri ya Iringa mkoani Iringa hii leo Juni 01,2026.

Wananchi wakiwa katika mistari tayari kuingia vituoni kupiga Kura.
Leo, Jumamosi ya tarehe 09 Mei 2026, Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam imefanikiwa kufanya Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa katika Ukumbi wa VETA Kigamboni, yakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Khadija Said.

Maadhimisho hayo yamebeba ujumbe mkubwa wa kuimarisha upendo, mshikamano na malezi bora ndani ya jamii kwa vitendo kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo ikiwemo:-

Kutembelea watoto wenye mahitaji maalum
Kuchangia damu katika Hospitali ya Kigamboni.
Uzinduzi wa Kigoda cha Wazazi.
Kupanda miti katika Shule ya Dungu.

Wananchi, wazazi na wadau mbalimbali wamejitokeza kushiriki katika shughuli hizo zenye lengo la kujenga jamii bora na yenye maadili mema kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kauli mbiu '“ Malezi Bora na Uzalendo ni Msingi kwa Taifa"














Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka vijana nchini kulinda amani na kutokubali kutumika katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama na taswira ya nchi.

Rais Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo jirani na Uwanja wa Ndege wa Dodoma, akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam, aliposimamishwa na maelfu ya wakazi wa Dodoma waliokusanyika barabarani kwa ajili ya kumsalimia Kiongozi huyo.

Wananchi hao, wakiwemo vijana, maafisa usafirishaji, wafanyabiashara wadogo, machinga, Mamalishe na Babalishe, walijitokeza wakiwa wamevaa fulana na mabango yenye ujumbe wa “Never Again” (Yasijirudie) sambamba na bendera za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiupokea ujumbe huo, Rais Dkt. Samia amesema matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini hayapaswi kujirudia kwa kuwa yaliathiri taswira ya Taifa na maisha ya wananchi kwa ujumla, hususan vijana.

“Niwaombe sana vijana, katika miji yenu, katika kazi zenu, katika shughuli zenu zote, ambizaneni yaliyotokea yasijirudie tena, kwani yamelitia doa Taifa letu,” amesema Rais Dkt. Samia, akisisitiza wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha matukio hayo, ambayo si sehemu ya hulka ya Watanzania, hayapewi tena nafasi katika jamii.

Aidha, amewataka vijana kulindana, kuelimishana na kuwa walinzi wa amani katika maeneo yao ya kazi, biashara na shughuli za kila siku, na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kusikiliza hoja za wananchi na kufanyia kazi changamoto zinazogusa maisha yao.

Kuhusu mikopo kwa wafanyabiashara wadogo, Rais Dkt. Samia amesema Serikali imeanza hatua za kusimamia zoezi la utoaji wa mikopo kupitia taasisi zaidi za kifedha tofauti na ilivyokuwa awali, ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa mitaji kwa vijana na makundi mbalimbali ya wajasiriamali.

Amesema mahitaji ya mikopo kwa vijana ni makubwa, na Serikali itaendelea kuongeza rasilimali kadiri uchumi utakavyoruhusu.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amesema Serikali itatathmini uwezekano wa kuanzisha soko lingine la wafanyabiashara wadogo mkoani Dodoma, pembezoni mwa Soko la Machinga Complex lililopo sasa, ili kukuza fursa zaidi kwa wajasiriamali, kupunguza msongamano na kuboresha mazingira ya biashara.

Awali, wawakilishi wa wafanyabiashara wadogo walieleza namna Soko la Machinga Complex lilivyo mfano bora wa utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu upangaji wa biashara ndogondogo katika maeneo rasmi, salama na rafiki kwa shughuli za kiuchumi, pamoja na kuomba kuimarishwa kwa huduma za usafiri wa daladala kuingia eneo la soko, uratibu na usimamizi endelevu wa biashara katika maeneo rasmi, na ongezeko la huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo.

Kwa upande wao, Mamalishe na Babalishe waliwasilisha ombi la kuendelea kuboreshewa masharti ya mikopo ya makundi maalum inayotolewa na Serikali ili makundi zaidi, hasa ya kipato cha chini, yaweze kunufaika.

Nao, Maafisa Usafirishaji wameahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka za Serikali katika kulinda amani na kuzuia matumizi mabaya ya vyombo vya usafiri ikiwemo vitendo vya fujo.

Akihitimisha, Rais Dkt. Samia ameagiza viongozi wa Mkoa wa Dodoma kufanyia kazi hoja zilizotolewa na wananchi, na kutaka ripoti ya utekelezaji pindi atakaporejea Dodoma.











Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza Mkoani Morogoro leo tarehe 28 Aprili, 2026 wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi.



Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Watendaji wa Uchaguzi na mambo muhimu ya kuzingatia.

Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.



Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.Mkurugenziu wa Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Adam Mkina akiwasilisha mada

Meza Kuu ikiwa katika ukumbi wa mafunzo

Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu wakila viapo vya kujitoa uanachama chama cha siasa na kile cha kutunza siri.

Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu wakila viapo vya kujitoa uanachama chama cha siasa na kile cha kutunza siri.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

Watendaji wa uchaguzi wametakiwa kuepuka kufanya kazi kwa mazoea licha ya baadhi yao kuwa na uzoefu kwenye masuala ya uchaguzi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 28 Aprili, 2026 mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Ismani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 01 Juni, 2026.

“Nachukua nafasi hii kuwaasa kuwa, pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi, mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea. Kwani kila uchaguzi unatofautiana na uchaguzi mwingine,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa watendaji hao wa uchaguzi wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo watakayopewa na Tume ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanavishirikisha vyama vya siasa katika hatua zote kuelekea uchaguzi huo.

“Wakati wote wa mchakato wa uchaguzi huu, ni vema mkavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yenu kuhusu masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia utekelezaji wa majukumu yenu,” amesema Jaji Mwambegele.

Amewataka watendaji hao kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husika na kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.

Jaji Mwambegele amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanaajiri watendaji wa vituo wenye sifa, weledi, wanaojitambua na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi.

“Mhakiki vifaa vya uchaguzi mnavyopokea kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema na muweke utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi,” amesema.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamewahusisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu.

Kata 12 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi wa Udiwani ni Mzimuni iliyopo Manispaa ya Kinondoni; Zongomera, Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Nyingine ni kata ya Kala iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Kibiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.