1. Huna tena muda wa kushinda siku nzima na mpenzi wako mkipiga stori za mapenzi.

2. Ukifikiria kufanya mapenzi, mahali pekee panapokuja akilini ni kitandani.

3. Unaanza kujaza friji lako vyakula vingi kuliko pombe.

4. Muziki unaoupenda unausikia zaidi kwenye lifti au ndani ya gari ukienda na kurudi kazini.

5. Saa 11 alfajiri ni muda wa kuamka, siyo tena muda wa kurudi kulala.

6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa.

7. Marafiki wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko kwenda mtoko wa klabu.

8. Ukienda dukani, unaweka juhudi kubwa kuomba upunguziwe bei.

9. Idadi ya tisheti na jeans inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo.

10. Wewe ndiye wa kwanza kukumbuka kupiga simu polisi endapo kuna vijana wanaosumbua mtaani.

11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia huru kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako.

12. Hukumbuki tena maduka ya Azam Ice Cream au Samaki Samaki yanafunga saa ngapi.

13. Timu yako ya mpira ikifungwa, hutaki tena kutaniwa na mtu.

14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawalisha kwa kanuni za kisayansi, si mabaki ya chakula cha haraka.

15. Ukilala kwenye kochi, unaamka ukiwa na maumivu makali ya mgongo.

16. Unaiweka ratiba yako ya kulala katika kipaumbele cha juu.

17. Ukiwa nyumbani, muda wa ziada unautumia kulima bustani ya maua au mbogamboga badala ya kutazama filamu.

18. Kila kinachonunuliwa nyumbani, swali la kwanza ni: “Umenunua shilingi ngapi?”

19. Unaenda duka la dawa kununua ibuprofen na antacid, siyo tena kondomu au kipima mimba.

20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Nipashe na The Express badala ya Uwazi, Ijumaa au Kiu.

21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati bila kukurupuka.

22. Ukiwa baa, unanunua kinywaji unachokihitaji wewe, si kusema tena “zungusha kama tulivyo.”

23. Asilimia kubwa ya muda unaoutumia kwenye kompyuta unaitumia kufanya kazi, siyo kuchati.

24. Ukipata hamu ya kunywa kilevi, unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla ya kwenda baa.

25. Ukimuona rafiki yako ni mjamzito, unampongeza badala ya kuuliza, “imekuwaje tena?”

26. Ukienda kutembea mahali, unaanza kuulizia bei za viwanja.

27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako.

28. Ukiwa na marafiki zako, unapenda kujadili mfumuko wa bei na mifumo mibovu ya utawala.

29. Ukiwa unakula, unakuwa mkali chakula kikiwa na mafuta au chumvi nyingi.

30. Ukimaliza kusoma pointi hizi 29 hapo juu, unaanza kuhesabu ni zipi zinaingia kwako.

👉 Ukiona una angalau nusu ya sifa hizi 30, basi huhitaji kupigiwa kengele kukukumbusha—umri umeanza kukupa ishara zake. 😄
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: