Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Jeshi Lupembe, akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa ofisi ya wafanyabiashara ndogo ndogo wamachinga ambao utagharimu Sh.Milioni 46 wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo uliofanyia jana.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAMACHINGA Mkoa wa Singida wameiomba Manispaa ya Singida kuanzisha mnada (GULIO) wa kila Ijumaa mara ujenzi wa ofisi yao inayojengwa jirani na Uwanja wa Ndege Kata ya Mandewmjini hapa kukamilika.

Ujenzi huo unafanyika baada ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kutoa Sh.Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ya wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga ambao kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya kutokuwa na ofisi hivyo kushindwa kuwa na eneo lakuzungumzia mambo yao ya biashara.

Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Singida, Ismail Otta, alisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hiyo wanaiomba Manispaa ya Singida ianzishe mnada wa kila Ijumaaambao utasaidia kuwaleta wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali na watu kupata mahitaji yao na manispaa hiyokupata fedha kutokana na ushuru ambao utakuwa ukiipwa na wafanyabiashara hao.

Alisema kwa muda mrefu changamoto yao kubwa ilikuwa ni kutokuwa na ofisi jambo lililokuwa likisababisha wakose sehemu ya kukutana na badala yake walipohitaji kufanya mkutano walipigiana siku na kukutana maeneo tofauti tofauti hapa mchini.

Otta alitumia nafasi hiyo kumshukru Rais Samia kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa alipokutana na wamachinga jijini Dodoma ambapo aliahidi kutoa Sh.milioni 10 kwa kila mkoa kwa ajili ujenzi wa ofisi za wamachinga jambo ambalo amelitekeleza.

Alisema katika Mkoa wa Singida kumekuwa hakuna migogoro na mivutano ya wamachinga kutokana na ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Jeshi Lupembe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ofisi hizo ambao utagharimu Sh.Milioni 46 alisema ofisi hizo pia zitatumiwa na madereva wa bajaji na bodaboda.

Alisema kutokana gharama hizo Halmashauri ya Manispaa ya Singida itaongezea Sh.milioni 36 na kwamba ili kuzifanya ofisi hizo zichangamke kila siku ya Ijumaa ya kila wiki kutakuwa na gulio ambalo wafanyakazi watakuwa wakiuza bidhaa mbalimbali kama walivyoomba wafanyabiashara hao.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida,Yagi Kiaratu, alimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha hizo na kumhakikishia kuwa Manispaa itasimamia na kuongeza fedha za kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kupitia mapato yake ya ndani.

Alisema kujengwa kwa ofisi hizo kutakuwa na manufaa kwa pande zote mbili kwani ofisi hizo zikitambulika itakuwa rahisi kwa Manispaa au serikali itakapowahitaji viongozi wa wamachinga kuzungumza nao jambo fulani kwa ajili ya maendeleo.

"Halmashauri ya Manispaa ya Singida Ina lengo zuri kulifanya eneo hili kuwa mnada ambao utatoa fursa kila mtu kuleta bidhaa zake mwenye kuchoma nyama atachoma,mwenye kuleta viatu au kinywa ataleta na bodaboda wataweza kupata wateja kuwasafirisha," alisema.

Kiaratu aliwataka watendaji kila mtu kusimamia majumuku yake ili Halmashauri ya Manispaa ya Singida Singida iendelee kusonga mbele na kuiga mfano wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Lupembe ambaye wakati wa siku ya wafanyakazi Mei Mosi alitunukiwa tuzo kutokana na uchapa kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Jeshi Lupembe, akitoa taarifa wakati wa uzinduzi huo..
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akishiriki kuchimba mtaro wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Hassan Mkata akishirikikuchimba msingi huo.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Hassan Mkata, akizungumzia ujenzi huo
Mmoja wa viongozi wa Wamachinga, Mkoa wa Singida, Asha Shabani akishiriki kuchimba msingi huo 
Msingi ukichimbwa
Afisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Simkwembea akizungumzia ujenzi wa ofisi hiyo
Mwenyekiti waWamachinga Mkoa wa Singida. Ismail Otta akizungumzia mambo mbalimbali kuhusu kazi zao na ujenzi wa ofisi hiyo
Mwenyekiti wa Bodaboda na Bajaj Mkoa wa Singida, Abdu Mitigo 

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: