.jpeg)
●Serikali Yatoa Pole, Yaahidi Hatua za Dharura
TABORA, TANZANIA — Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa salamu za pole kwa familia, ndugu, na jamii nzima ya Mkoa wa Tabora kufuatia ajali ya moto iliyotokea Julai 28, 2025 katika Makao ya Watoto Igamilo, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, na kuua watoto watano.
Kupitia Taarifa rasmi iliyotolewa Julai 29 na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Waziri Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio hilo ambalo limeacha majonzi na huzuni kubwa kwa taifa zima.
"Ni huzuni, ni majonzi. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mzito. Tunawaombea faraja, subira na nguvu katika kipindi hiki kigumu," ilieleza sehemu ya taarifa ya Waziri Gwajima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo. Wizara imesisitiza kuwa wamiliki na wasimamizi wa Makao ya Watoto kote nchini lazima kuhakikisha ukaguzi wa mifumo ya umeme na miundombinu ya kinga dhidi ya majanga ya moto unafanyika mara kwa mara ili kuzuia matukio kama haya.
Serikali pia imethibitisha kuwa watoto waliojeruhiwa katika tukio hilo wanapata matibabu bure, huku wengine wakihifadhiwa mahali salama wakisaidiwa kisaikolojia na kijamii kupitia Maafisa Ustawi wa Jamii na Halmashauri husika.
Wizara imesisitiza kuwa itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa tukio hilo na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuimarisha usalama na ulinzi wa watoto katika Makao yote nchini.
Mkurugenzi wa BRAC Tanzania, Joydeep Sinha Roy akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bethasaida walipotembelea na kutoa msaada wa vifaa muhimu na rasilimaliza elimu kwa wasichana hao, hilo limefanyika wakati wa kuadhimisha miaka 53 toka kuanzishwa kwa Shirika hilo.



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele ametembelea na kukagua mafunzo ya vitendo kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo wa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga katika siku ya pili na ya mwisho ya mafunzo yao leo Februari 7,2025.
Uboreshaji wa Daftari utafanyika Mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza sambamba na Mkoa wa Pwani kuanzia Februari 13 hadi 19,2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Akizungumza na Maafisa hao Mhe. Jaji Mwambegele aliwasisitiza kutambua umuhimu wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kitaifa na kuwahimiza pia kushirikiana na wadau wa Uchaguzi wakiwepo Vyama vya Siasa alivyovitaka vihakikishe vinateua mawakala katika kila kituo ili waweze kusaidia kuwatambua wananchi kutoka maeneo husika.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Asina Omari, leo tarehe 07 Februari, 2025 ametembelea mafunzo ya Maafisa Uandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mwinyi, uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ikiwa ni siku ya pili ya Mafunzo hayo.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mikoa ya Pwani na Tanga katika Halmashauri za Wilaya Lushoto, Kilindi, Muheza, Korogwe, Mji wa Korogwe, Mji wa Handeni na Jiji la Tanga unatarajia kuanzia tarehe 13 Februari hadi 19 Februari, 2025 na vituo vya kuandikisha Wapiga Kura vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni kwa muda wa siku Saba.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira, amewataka watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ngazi Kata, kuwa waadilifu wakati wote wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao. Mhe.Rwebangira ametoa maelekezo hayo leo Februari 07, 2025, alipotembelea mafunzo kwa watendaji hao katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, ambapo pia amewasisitiza kuzingatia mafunzo hayo, ili wakaweze kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi. Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Februari 13, 2025 hadi Februari 19, 2025, katika mikoa ya Pwani na Tanga katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Dkt. Zakia Mohamed Abubakar ametembelea mafunzo ya Maafisa Uandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia mkoani Pwani ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mikoa ya Pwani na Tanga katika Halmashauri za Wilaya Lushoto, Kilindi, Muheza, Korogwe, Mji wa Korogwe, Mji wa Handeni na Jiji la Tanga unatarajia kuanzia tarehe 13 Februari hadi 19 Februari, 2025 na vituo vya kuandikisha Wapiga Kura vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 Jioni kwa muda wa siku Saba.
Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga , Mwanaidi Nondo, akiwa katika mafunzo hayo.


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Asina Omari, leo Februari 07 , 2025 ametembelea mafunzo ya Maafisa Uandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mwinyi, uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ikiwa ni siku ya pili ya Mafunzo hayo.

.jpeg)
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira akitembelea mafunzo kwa mafunzo ya vitendo kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo katika Hamashauri ya Wilauya ya Handeni mkoani Tanga,leo Februari 07, 2025, ambapo pia amewasisitiza kuzingatia mafunzo hayo, ili wakaweze kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi.
.jpeg)

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira akitembelea mafunzo kwa mafunzo ya vitendo kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo katika Hamashauri ya Wilauya ya Handeni mkoani Tanga,leo Februari 07, 2025, ambapo pia amewasisitiza kuzingatia mafunzo hayo, ili wakaweze kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua eneo la maafa ya ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo ambao wamelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Novemba, 2024.












