Articles by "DINI"
Showing posts with label DINI. Show all posts
WAUMINI wa Kanisa la Baptist Kinondoni mkoani Dar es Salaam wakiongozwa na Mchungaji wa kanisa hilo Samweli Kabonaki wamefanya ibada maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kipindi cha majanga yakiwemo mafuriko yanayosababishwa na vua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalmbli za nchi yetu na nchi jirani.Akizungumza wakati wa ibada hiyo ,Mchungaji Kabonaki amesema Watanzania na Dunia wanajua kipindi wanachopitia kutokana na uwepo wa majnga yanayoleta madhara katika maeo mbalimbali ya nchini na nje ya nchi."Tumeona ni vema Kanisa hilo likafanya maombi maalum kuombea nchi yetu na mataifa mengine na duna kiujumla,"amesema na kusisitiza katika kukabiliana na majanga hayo ni vema kila mmoja wetu akamtanguliza Mungu zaidi na yvema ikajulikana Mungu ambaye ndiye mwenye majibu yote na ni mponyaji Mkuu."









Ibaada ikiendelea


Waimbaji wa kwaya ya Shalom wakiimba wakati wa ibaada ya maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kipindi hiki cha majanga mbalimbali leo Mkoa wa Dar es Salaam.



















Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Jaffari Matundu, akizungumza na wadau (hawapo pichani) katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya benki na wadau wake wakiwemo wateja na jamii katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani katika tukio lililofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, akitoa pongezi kwa Benki ya Exim kwa kuandaa Iftar akielezea namna ambavyo imewaleta pamoja waumini wa dini ya kiislam kama ishara ya upendo, umoja na heshima kwa wadau wote katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (wa tatu kutoka kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar (watatu kutoka kulia) wakiwa na baadhi ya viongozi wa Exim Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali na wawakilishi wa Benki ya Exim wakifurahia Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwaleta pamoja katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuashiria furaha, umoja, na upendo katika tukio lililofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa benki hiyo wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwakutanisha wateja wake pamoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika tarehe 15 meezi Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
---
(Dar es Salaam, Machi 15 2024). Benki ya Exim imeandaa futari ya pamoja kwa wateja wake katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 15 mwezi Machi 2024.

Mgeni Rasmi katika tukio hili alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, akiwakilisha waumini wa dini ya Kiislam ambao wapo kwenye mfungo katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, aliipongeza Benki ya Exim kwa juhudi zake katika kukuza maendeleo ya kijamii na kueleza shukrani zake kwa mchango wa benki hiyo kwa jamii. Alisema, “Benki ya Exim inaonyesha dhamira ya kweli katika kutumikia wateja wake na jamii kwa ujumla, lengo kuu la Ramadhani ni kuleta watu pamoja, na usiku huu, benki ya Exim imehakikisha kuendeleza lengo hilo kwa vitendo”.

Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, aliwakaribisha wadau wote katika Iftar hiyo huku akitambua mahusiano mazuri ya tija yaliopo baina ya Benki ya Exim na wateja wake na umuhimu wa kuyaendeleza kwa ajli ya ustawi na maendeleo ya jamii.

“Wateja wetu ni zaidi ya wateja tu, ni sehemu muhimu ya familia yetu. Tunaona kila mmoja wenu kama mshirika na mwenzetu katika safari yetu ya mafanikio”, alisisitiza Jaffari Matundu.

Pia, Mkurugenzi huyo alizungumzia hatua na maboresho mbalimbali ambayo yamefanywa na benki ya Exim ili kuendana na mabadiliko katika sekta mbalimbali ikiwemo maendeleo ya teknolojia ya kidijitali na kusogeza huduma kwa wateja.

Jaffari alifafanua kuwa, “tumefanya maboresho makubwa katika mfumo wetu wa Benki ili kuendelea kuhudumia wateja wetu vizuri zaidi kwa kutoa huduma zinazoendana na mabadiliko ya kidigitali”.

“Vile vile tumeendelea kuongeza idadi ya Mawakala wetu (maarufu kama Exim Wakala) ili kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu popote walipo”, alimalizia Afisa Mtendaji Mkuu huyo.

Exim Bank pia imeboresha huduma za kidijitali kwa wateja wake ambapo wanaweza kupata huduma za kibenki popote pale walipo ndani na nje ya Tanzania. Hii ni kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja wao na maendeleo ya teknolojia yanayoendelea kutokea duniani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC inashiriki katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Utaratibu huu wa kushiriki katika maonesho mbalimbali nchini ni sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kutoa elimu ya Mpiga Kura endelevu ambapo wadau mbalimbali wa Tume hufika katika Banda hilo na kupata elimu hiyo.

Maonesho haya ambayo huandaliwa na Mahakama ya Tanzania ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya sheria na kuanza kwa mwaka mpya wa Mahakama.

Mwaka huu maonesho haya yamebeba kauli mbiu isemayo "Umuhimu wa Dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa:Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo Jumuishi wa Haki Jinai" yameanza tarehe 24 Januari,2024 na yanatarajia kumalizika tarehe 30 Januari, 2024.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Cuthbert Mapunda (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Cuthbert Mapunda (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bi.Neseria Leng’ida (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma
Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square.

Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakizungumza na mdau aliyetembelea banda la Tume katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma

Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakizungumza na mdau aliyetembelea banda la Tume katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw.Loshilu Saning’o (Kulia) akizungumza na mdau wa Uchaguzi aliyetembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Unguja. Tarehe 10 Septemba 2023: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma za kibenki zinazofuata misingi ya sharia hivyo kuwahamasisha Waislamu wengi kutumia huduma zake jambo linalochochea ujumuishi wa kifedha.

Rais Mwinyi ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufungua akaunti ya Al Barakah mwishoni mwa mwaka 2021 huduma hiyo ilipozinduliwa, ametoa pongezi hizo alipokabidhiwa kadi ya akaunti hiyo mwishoni mwa wiki alipotembelewa na ujumbe wa Benki ya CRDB ikulu mjini Zanzibar.
“Tulijua Al Barakah itakuwa na mafanikio lakini hatukutarajia kuwa yangepatikana ndani ya muda mfupi namna hii. Nawapongeza kwa mafanikio mliyoyapata na niwaahidi kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano na benki yenu kuhakikisha huduma hizi zinawafikia Waislamu wengi walipo visiwani humu ili kwa Pamoja tushiriki kulijenga Taifa letu huku tukimwabudu Mwenyezi Mungu bila kukiuka maagizo yake,” amesema Dkt Mwinyi.

Rais Mwinyi pia ameishukuru Benki ya CRDB kwa heshima iliyompa ya kuwa mteja wa kwanza kukabidhiwa kadi ya Akaunti ya Al Barakah na akasema jambo hilo limemhamasisha zaidi hivyo ataangalia namna ya kuongeza amana kwenye akaunti yake ili kufurahia huduma hizo zinazokidhi mahitaji yake ya kifedha na imani ya kiroho.
Akimkabidhi kadi ya Al Barakah, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB inayojumuisha Zanzibar na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Badru Idd amesema Rais Mwinyi sio tu alihamasisha kuanzishwa kwa huduma hizo bali alionyesha mfano kwa kuwa wa kwanza kufungua akaunti hiyo mwaka 2021 ambayo mpaka sasa ina wateja zaidi ya 70,000 nchini kote.

“Mpaka sasa hivi, tumekopesha zaidi ya shilingi bilioni 90 kwa misingi ya sharia na tumepokea amana za wateja zaidi ya shilingi 85 bilioni ndani ya miaka miwili ya kutoa huduma hizi. Huduma za CRDB Al Barakah Banking zinaendelea kutoa mchango mkubwa sana katika serikali yako ya Zanzibar na wananchi wake kwani tumekopesha zaidi ya shilingi 18 bilioni kwenye uchumi wa buluu na wafanyabiashara wamepata Zaidi ya shilingi bilioni 33,” amesema Idd.

Ili kusogeza huduma kwa wananchi visiwani humu, Benki ya CRDB ilifungua tawi mjini Wete lililozinduliwa na Rais Mwinyi mwaka 2021 alikoiomba benki kuanzisha huduma zenye misingi ya sharia na mpaka sasa, kwenye matawi manne ya Benki ya CRDB yaliyomo Zanzibar, wananchi wameweka amana za zaidi ya shilingi bilioni 28.
Kuhusu kadi za Akaunti ya Al Barakah, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Zinazofuata Sharia (Islamic Bankink) wa Benki ya CRDB, Rashid Rashid amesema zipo za aina nne na zote zinaweza kutumika katika majukwaa yote ikiwamo kwa mawakala zaidi ya 200 waliopo Zanzibar kama ilivyo kwa kadi zinazotumiwa na wateja wengine wote wa Benki ya CRDB.

“Pamoja na mafanikio haya makubwa, CRDB Al Barakah Banking tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwafikia wateja wetu na kuwapa amani wanayoitegemea kwa kuweka pesa zao katika akaunti za Al Barakah zinazofuatisha misingi ya sharia. Kila mteja mwenye akaunti hii, ana amani kwa kujua kwamba pesa zake ziko mahala salama na zina uangalizi maalum unaoendana na imani na maadili yake,” amesema Rashid.
Akizungumzia umuhimu wa huduma za fedha kwa maendeleo ya Taifa, Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Fedha Zinazofuata Misingi ya Sharia ya Benki ya CRDB, Abdul van Mohammed amesema kuna fursa nyingi ambazo Zanzibar inaweza kunufaika nazo iwapo itafungua milango.

“Zanzibar ndio yenye matumizi makubwa ya Islamic Banking Afrika Mashariki. Naomba Serikali iangalie uwezekano wa kuifanya kuwa ya kwanza kuuza hatifungani ya Kiislam ili kupata fedha zitakazochangia maendeleo ya watu wetu,” amesema Mohammed.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro , akizungumza na Waislam wa Kata ya Mtinko wakati wa harambee ya ujenzi wa msikiti iliyofanyika Septemba 3, 2023.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WADAU mbalimbali wameombwa kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Jaamigh uliopo Kata ya Mtinko Wilaya ya Singida, mkoani Singida ambapo jumla ya Sh. Bilioni 1.8 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo.

Katibu wa kamati ya ujenzi wa msikiti huo, Abdallah Rajab akizungumza wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa msikiti huo mbele ya Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro alisema hadi kukamilika kwa ujenzi huo Sh.Bilioni 1.8 zinahitajika.

Rajab alisema msikiti wa awali ambao ulijulikana kama Msikiti wa Ijumaa Mtinko ulijengwa mwaka 1949 ukiwa na uwezo wa kuhudumia waumini 100 kwa wakati mmoja.

Alisema kutokana na ongezeko la waumini msikiti huo ulipanuliwa mwaka 1990 na kuwa na uwezo wa kuwahudumia waumini 300 na unatumika hadi hivi leo.

Rajab alisema kutokana na ongezeko la waumini na kuanza kuswalia nje mwaka 2018 ndipo walipopata wazo la kuanzisha ujenzi wa msikiti wa sasa wa ghorofa ambao ujenzi wake ulianza mwaka 2019.

'' Ujenzi upo hatua ya kusuka bimu kwenye msingi na ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia waumini 1000 kwa wakati mmoja,'' alisema Rajab.

Alisema msikiti huo utakuwa na huduma za ofisi ya utawala, madrasa, vibanda vya biashara na huduma ya vyoo.

Alisema mahitaji makubwa ya hivi sasa ya ujenzi huo ni mchanga, saruji na nondo na kuwa katika hatua hiyo waliyoifikia ya ujenzi zimetumika Sh.Milioni 28,059,300 fedha zilizotokana na sadaka za waumini na wadau wengine mbalimbali na kuwa kwenye akaunti yao wana Sh.Milioni 3.

Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa msikiti wakishirikiana na kamati ya bodi ya msikiti, Jumuiya ya Wanawake wa Wakiislam } JUWAKITA }, wa kata hiyo na kamati ya ujenzi ilifanyika harambee ambapo zilipatikana zaidi ya Sh.Milioni 3.7.

Katika kuongeza nguvu ya kupatikana kwa fedha za ujenzi wa msikiti huo Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro anatarajia kufanya harambee nyingine hivi karibuni katika tarehe itakayo pangwa ambayo itawashirikisha wadau na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Mkoa wa Singida.

Kamati ya ujenzi wa msikiti huo inawaomba wadau mbalimbali kusaidia ujenzi huo na kwa mtu yeyote, wafanyabiashara, taasisi watakaokuwa tayari kuchangia chochote walichonacho iwe saruji, kokoto, mchanga na vifaa vingine vya ujenzi na kama ni fedha wanaweza kuweka katika akaunti namba 0152737109500 Benki ya CRDB Mtinko Masjid au wanaweza kuwasiliana na Mtunza fedha wa msikiti huo Said Salim Mdimi kwa namba ya simu 0788778591 kwani kutoa ni moyo na si utajiri. 

Katibu wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Singida, Said Ally Mang'ola akizungumza kwenye harambee hiyo.
Sheikh wa Kata ya Mtingo, Jumanne Ramadhan akichangia jambo wakati wa harambee hiyo.
Mwalimu wa Dini, Sheikh Isihaka Hassan akizungumza kwenye harambee hiyo.
Kikongwe Hadija Mandi akiwahamasisha Waislam kuchangia ujenzi wa msikiti huo.
Wazee wakiwa kwenye harambee hiyo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro|} katikati } akizungumza wakati akikagua ujenzi wa msikiti huo.
Muonekano wa ujenzi wa msikiti huo.
Kiongozi wa Kamati ya Wanawake wa Kiislam wa kata hiyo, Hawa Ayubu, akiongoza uhamasishaji wa kuchangia ujenzi huo.
Wakina mama wakiwa kwenye harambee hiyo.
Harambee hiyo ikiendelea.
Wakina mama wakichangia katika harambee hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Singida, Magharibi, Elibariki Kingu.

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa barabara ya kutoka Sepuka wilayani Ikungi hadi Kizaga wilayani Iramba ambayo ujenzi wake unatarajia kuzinduliwa kesho kutwa Septemba 9, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana alisema hana la kusema zaidi ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa Mungu ampe afya na maisha marefu ili aweze kuendelea kuliongoza taifa letu la Tanzania.

'' Naishiwa maneno ya kumueleza Rais Samia mama mwenye huruma na upendo kwa watanzania ambaye anakwenda kuyabadilisha maisha ya wana Singida Magharibi, Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kutokana na kazi yake hii kubwa iliyotukuka,'' alisema Kingu.

Kingu alisema uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kufanyika Septemba 9, 2023 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ambapo pia atakuwepo Waziri wa Fedha, Dk.Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi..

Pia hafla hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Kingu alisema kilio chake na hoja yake kubwa tangu ameingia bungeni ilikuwa ni ujenzi wa barabara hiyo na kuwa anamshukuru Rais Samia kwa kukisikia.

'' Toka mwaka 2015 nimekua nikipigania barabara hii na sasa yametimia, lakini ile ya Iyumbu hadi Tabora kupitia Singida nimeanza mwaka huu na tayari tumepewa pesa za kufanya upembuzi yakinifu,'' alisema Kingu huku akionesha tabasamu la furaha.

Aidha, Kingu alisema ujenzi wa barabara ya Singida Sepuka hadi Kizaga itafufua ukuaji wa uchumi katika Jimbo la Singida Magharibi na Mkoa wa Singida kwa ujumla.

Kingu alitoa wito kwa wananchi wa jimbo hilo waendelee kuunga mkono jitihada za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuupokea mradi huo kwa heshima kubwa na kutoa ushirikiano kwa wakandarasi watakao kuwa wanajenga.
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba, Magharibi.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa