Articles by "DKT MWINYI"
Showing posts with label DKT MWINYI. Show all posts
Na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG

Hanang', Katesh 27 Januari 2024: Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo ameongoza zoezi la upandaji wa miti lililoendana na ukataji wa keki kwa ajili kusherekea miaka 64 ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiongoza zoezi hilo la upandaji na kukata keki lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Katesh - Hanang, Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Miti zaidi ya 3,000 imepandwa katika maeneo yaliyoathiriwa na maporomoko ya tope, mawe na magogo ikiwa ni njia mojawapo ya kurejesha uoto wa asili uliopotea kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na mafuriko hayo yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2023. Kwa mwaka 2024, Mkoa wa Manyara umejipanga kupanda miti milioni 10.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mhe. Fredrick Sumaye Waziri Mkuu Mstaafu, Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Manyara, Wakuu wa Taasisi Mbalimbali, Wakuu wa Idara pamoja, wananchi pamoja na watoto walioathirika katika maporomoko hayo.

Pamoja na hayo, Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Wizara ya Afya umetekeleza zoezi la uhamasishaji wa mwezi wa saratani ya mlango wa kizazi, ambapo zaidi ya watu 328 katika Wilaya ya Hanang' wamejitokeza kufanya uchunguzi wa awali.

Aidha, elimu na hamasa inaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu kwa wale watakaobainika kuwa na viashiria vya saratani.
In an inspiring event that seamlessly blended creativity, innovation, and a steadfast commitment to shaping Africa’s future, Sahara Tanzania Limited, a Sahara Group downstream company, and Sahara Group Foundation, the social sustainability vehicle for Sahara Group, hosted the first edition of the Sahara STEAMers Programme National Demo Day competition.

The Sahara STEAMers programme, an afterschool initiative in partnership with STEMCafe, was established in 2022 with the primary aim of fostering innovation, creativity, and excellence in Science, Technology, Engineering, Arts, and Mathematics (STEAM) education among secondary school students in Africa.

Equipping participants with the knowledge and skills required to create innovative solutions addressing real-world problems across various sectors, including energy, agriculture, security, healthcare, and transportation, the programme is instrumental in creating a pipeline of Africa’s next generation leaders and social innovators.

The Tanzanian Demo Day Event this year featured students from Tambaza Secondary School and Kisutu Secondary School. Collaborating in teams, these students passionately presented their innovative solutions to a panel of judges. The Demo Day showcased a diverse group of young Tanzanian problem solvers with brilliant prototype designs aimed at tackling prevalent social issues in their communities.

Deeply impressed by the students' unwavering dedication to making a tangible impact in their communities at such a young age, Ejiro Gray, Director of Sahara Group Foundation, lauded the students' passion, intelligence, creativity, and problem-solving skills. She stated that, for some of the students, their participation in the Sahara STEAMers programme marked their first real interaction with technology and its practical applications in addressing real-world challenges.

Gray extended her heartfelt congratulations to all participants, urging them to persist in cultivating their newfound skills and embracing future opportunities to refine them for driving positive societal change. In conclusion, Gray affirmed that the inspiring display witnessed at the event was not merely a fleeting moment but a clear manifestation of the steadfast commitment of both Sahara Group Foundation and Sahara Tanzania Limited to empower young minds across Africa. This commitment is geared towards nurturing a future generation equipped to lead with innovation, compassion, and a lasting impact, thereby shaping a world where positive change becomes an inherent part of their journey.

Applauding the outstanding accomplishments of the participating students, Kunle Onadeko, Terminal Operations Manager at Sahara Tanzania Limited, underscored the pivotal role of the Sahara STEAMers programme in nurturing young talents and fostering their innovative skills. He expressed, "The Sahara STEAMers programme transcends being a mere initiative; it acts as a catalyst for transformative change.

Onadeko further emphasized that the quality of innovations on display is proof of the significant impact that comes from investing in young people and igniting their minds to see no limits. He encouraged the students to continue on this innovative thinking pathway, stating that the future of Tanzania, and Africa at large, is truly sustainably bright.

After an engaging and lively competition, the judges praised the students for their ability to conceive and develop viable solutions before announcing the winners.

Team Katone from Tambaza Secondary School clinched the top position with their innovative Smart Water Leveling System, an advanced sensor that delivers precise real-time water level data. The Smart Leveling System facilitates efficient water distribution and will further encourage sustainable water management practices.

In a close pursuit, Team Young Girls from Kisutu Secondary School achieved the first runner-up position with their groundbreaking Water Salinity and pH Monitoring device. This innovative tool detects contaminants promptly, allowing for a timely response to safeguard water quality for both consumption and environmental preservation.

Securing the second runner-up position was STF from Tambaza Secondary School. The team devised a Car Alcohol Detection System that effectively prevents drunk driving. This solution seamlessly integrates alcohol detection technology into vehicles' ignition systems, ensuring only sober drivers can start the vehicle.

As we celebrate the remarkable innovations showcased on this momentous day and witness the rise of Africa's next generation social innovators, it is evident that the nexus between education and innovation plays a pivotal role in Africa's advancement. Through empowering initiatives like the Sahara STEAMers programme, Sahara Tanzania Limited and Sahara Group Foundation are actively shaping a trajectory for a more resilient, prosperous, and sustainable Africa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Paje, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji CRDB Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, wakati alipotembelea banda letu kwenye ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na wananchi waliofurika kwa wingi katika viwanja vya Paje, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi akiwa pamoja na viongozi wengine wakipiga makofi na kufurahia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
Sehemu ya burudani kutoka kwa watoto wa Shule ya Assalam ya Kizimkazi.





MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Tanga Tony Mwanjota akizungumza wakati wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza wakati wa mafunzo hayo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba katikati akiwa meza kuu na viongozi wengine kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo kulia akiwa na washiriki wengine wakifiuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo kulia akiwa na washiriki wengine wakifiuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo
Na Oscar Assenga, TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amefungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya Watu na makazi yam waka 2022 kwa viongozi, watendaji, wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo ikiwemo makundi maalumu kwa Halmashauri za mkoa huo .

huku akieleza kuwa yatawajengea uwezo wakufunzi kuchambua na kutumia matokeo ya sensa ili yawe mwanzo wa dira ya kuwaongoza katika utekelezaji wa majukumu na malengo yao ya kila siku.

Kindamba aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Regail Naivera Jijini Tanga ambapo alisema mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutafsiri, kwahiyo nawaomba sana wakati mafunzo yakiendelea kuwa watulivu, ili yaweze kwenda kuwa msaada kwenye ngazi ya chini.

Alisema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu Mkoa wa Tanga idadi imeongezeka lakini siyo kwa idadi kubwa ya watu tofauti na Mikoa mingine Kitaifa.

Aidha alisema Idadi hiyo inaonesha kwamba kiwango cha kuongezeka kimetoka asilimia 2.2 mwaka 2012 na kufikia asilimia 2.5 2022, lakini pamoja na hayo, Mkoa wa Tanga inaonesha kwamba kasi yetu ya kukua iko chini sana ikilinganishwa na takwimu za sensa za Kitaifa ambazo sasa ipo asilimia 3.2.

Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa makini katika kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti na endelevu itakayowahakikishia wananchi huduma bora na za kiuchumi ili kuimarisha ustawi wao na maendeleo ya Mkoa.

Hata hivyo alisema ni muhimu kutambua Mkoa huo umefunguka kutokana na uwepo wa fursa mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta nao utakuja na watu wake hivyo wao wameamua Tanga iwe kituo cha kuvutia watu waje na hivyo wanapokuja na wenyeji nao wapo.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Tonny Mwanjota alisisitiza umuhimu wa wadau wa sensa na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu kwa baadhi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kusubiria majibu ya matokeo kwa upande wa watu wenye hali ya ulemavu.

Mwanjota amesema matokeo ya sensa bado yanaendelea kutolewa kwa awamu hivyo kwa ugumu wa takwimu kwa wenye ulemavu hivyo nayo yapo miongoni mwa yale ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Uongozi wa Taasisi ya Bahari ya Korea Kusini, ukiongozwa na Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt.Kim Jong Deog, (kulia kwa Balozi) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-6-2023, (kulia kwa Rais) Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Togolani Edriss Mavura.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Uongozi wa Taasisi ya Bahari ya Korea Kusini, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-6-2023, (kulia kwa Rais) Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Togolani Edriss Mavura na Mkuu wa Taasisi ya Bahari Kuroe Kusini Dkt.Kim Jong Deog, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe. Suleimann Masoud Makame.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar mgeni wake Mkuu wa Taasisi ya Bahari ya Korea Kusini Dkt. Kim Jong Deog, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-6-2023.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Mkuu wa Taasisi ya Bahari ya Korea Kusini Dkt. Kim Jong Deog, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-6-2023.(Picha na Ikulu)
Benki ya CRDB kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation, leo imezindua rasmi msimu wa nne wa mbio za CRDB Bank Marathon ikwa na lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia kuboresha afya ya mama na mtoto nchini. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa mahojiano ya wanahabari na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mheshimiwa Mariam Mwinyi, yaliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.

Akizindua msimu wa nne wa CRDB Marathon 2023, Mama Mariam Mwinyi aliipongeza Benki ya CRDB kwa msaada wake usioyumba kwa afya ya mama na mtoto kupitia mbio hizo. Katika hotuba yake, alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali, pamoja na wakimbiaji kutoka nje ya Tanzania, kujiandikisha kwa wingi katika mbio za CRDB Bank Marathon 2023.
Mama Mariam Mwinyi alisisitiza kuwa juhudi za pamoja za washirika na wakimbiaji ni muhimu katika kufikia lengo la kuchangisha fedha kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ziilizoanishwa katika malengo ya mbio hizi ikiwamo afaya ya mama na mtoto. Aliongezea kuwa kumsaidia mama ni kusaidia jamii nzima na akawataka watu binafsi kuunga mkono jitihada hizo na kuchangia katika mbio hizo.

Katika mahojiano hayo Mama Mariam Mwinyi alizungumzia wito wake binafsi katika kusaidia jamii uliopelekea kuanzisha taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation yenye lengo la kuboresha maisha ya Wazanzibari kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia zaidi afya ya mama na mtoto. Alitoa shukurani zake kwa benki hiyo kwa kuchagua kujikita katika sekta ya afya Zanzibar, eneo ambalo linamgusa sana na ambapo pia ni mdau mkubwa.
“Ustawi wa jamii yetu unahitaji kila mmoja wetu kuwa na wito wa kujitoa katika masuala mbalimbali ya kijamii,” alisema Mama Mariam Mwinyi. “Kupitia Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation tunalenga kuinua maisha ya Wazanzibari kiuchumi na kijamii kwa kutilia mkazo zaidi afya ya mama na mtoto, naipongeza Benki ya CRDB na washirika wake kwa kuungana nasi katika kuleta mabadiliko katika sekta ya afya Zanzibar kupitia CRDB Bank Marathon."

Mheshimiwa alitumia fursa hiyo pia kutangaza kuwa Mheshimiwa Dk Hussein Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, amekubali kuwa Mgeni Rasmi katika msimu wa nnne wa CRDB Marathon 2023. Mbio hizo zimepangwa kufanyika Agosti 13 katika viwanja vya The Green maarufu kama viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya CRDB Bank Foundation, alieleza kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha msimu wa nne unakuwa wa kipekee na uzoefu uliobora zaidi kwa wakimbiaji na washiriki wote. Tully anibainisha kuwa mbio za mwaka huu wamejipanga kuhakikisha usalama zaidi kwa wakimbiaji, na kusema kuwa katika upande wa burudani pia wamejipanga vilivyo na kuhimiza washiriki kujisajili wao pamoja na familia zao kwani mbio hizo pia zimezingatia burudani kwa watoto.

Mwambapa alibainisha kuwa msimu wa nne wa CRDB Bank Marathon unalenga kufikia malengo matatu muhimu. Kwanza, ujenzi wa kituo cha afya cha mama na watoto katika visiwa vya Zanzibar ni kipaumbele kikubwa. Mpango huo unaoendana na malengo ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, inayoongozwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi, unaimarisha zaidi dhamira ya Benki ya CRDB katika kusaidia afya ya mama na mtoto nchini.
Pili, kupitia mbio hizo Benki ya CRDB imejipanga kuendeleza jitihada za kusaidia matibabu ya akina mama walio na mimba hatarishi na kutatua changamoto ya fistula katika hospitali ya CCBRT. Mwambapa alisisitiza umuhimu wamsaada huo sio tu kutoa matibabu bali pia kuwawezesha akina mama hao kiuchumi ili kusaidia familia na jamii zao ipasavyo.

Aidha, CRDB Bank Marathon 2023 inalenga kuendeleza msaada wake kwa matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Mwambapa amesema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita bado ipo ya haja ya kuendelea kushughulikia changamoto hiyo ya kiafya inayowaathiri watoto nchini.
Tullo Mafuru, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Sanlam ambao ni washirika wakubwa wa CRDB Bank Marathon amesema taasisi yao inajivunia kuwa sehemu ya mbio hizo kwa misimu minne mfululizo. Tullo alisema Sanlam ikiwa kampuni inayoongoza katika sekta ya bima nchini afya ya wateja imekuwa kipaumbele kikibwa kwao, sababu ambayo imepelekea kusaidia kufanikisha malengo ya mbio hizo husasani katika kusaidia afya ya mama na mtoto.

Usajili wa mbio za CRDB Bank Marathon 2023 umefunguliwa rasmi kupitia tovuti rasmi ya mbio hizo www.crdbbankmarathon.com. Watanzania na washiriki wa kimataifa wanakaribishwa kujisajili na kushiriki mbio hizi za kizalendo zenye nia ya kuboresha ustawi wa jamii nchini ikiwamo afya ya mama na mtoto nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa, mwaka huu malengo ni kupata washiriki 7,000.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita mbio za CRDB Bank Marathon zimekua kwa kiasi kikubwa kwa, shukrani kwa washirika na wakimbiaji kutoka Tanzania na kutoka duniani kote. Kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, mbio hizo zimeweza kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 kusaidia changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

“Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kusaidia upasuaji wa watoto zaidi ya 300 wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, kusaidia ujenzi wa Kituo cha kisasa cha Mawasiliano katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, kusaidia matibabu ya akina mama walio katika mazingira hatarishi.
wajawazito katika Hospitali ya CCBRT,” alisema Mwambapa huku akiongeza kuwa fedha hizo pia zilisaidia uhifadhi wa mazingira kupitia kampeni ya Benki ya CRDB ya Pendezesha Tanzania, na Resi za Ngalawa wakati wa tamasha la Kizimkazi.

Mbio za CRDB Bank Marathon zimepata heshima kubwa kupelekea kupata usajili wa kimataifa kutoka kwa kutoka Chama cha Usajili na Upimaji wa Mbio za Kimataifa (AIMS) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo wa Riadha (World Athletics).
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) majukumu ya WCM Machi 2, 2023.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

KUMEKUWA na ongezeko kubwa la waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya sita, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma amesema.

Dkt. Mduma ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Machi 2, 2023 ambapo alidokeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Februari 2023 Waajiri wapya 5,250 wamejisajili WCF.

Alisema kwa taarifa zisizokaguliwa hadi kufikia Mwezi Februari 2023, WCF ilikuwa imesajili jumla ya waajiri 29,978,

Kati ya waajiri hao asilimia 99.27% ni waajiri wakubwa, huku asilimia 98.71% ni waajiri wa kati na waajiri wa chini ni asilimia 88.56%.

“Hatua za makusudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, za kuweka vivutio vya kufanya biashara na kuondoa vikwazo vilivyokuwepo ikiwa ni pamoja na kupunguza viwango vya uchangiaji na kutoa msamaha wa riba vimechangia ongezeko hilo.” Alisisitiza Dkt. Mduma.

Alisema kwa sasa mwajiri amepunguziwa mzigo wa kuchangia kwenye Mfuko ambapo serikali ilipunguza kiwango cha mchango kwa Sekta Binafsi kutoka asilimia 1% ya hapo awali kabla ya maboresho ya kisera hadi asilimia 0.5% ya sasa na hivyo kuleta ulinganifu wa michango kuwa sawa na Sekta ya Umma.

“Niwahakikishie wafanyakazi kuwa mafao yanayotolewa na WCF yataendelea kutolewa kwa ubora ili kuendelea kuleta nafuu na faraja kubwa kwa wafanyakazi.” Alisema.

Lakini pia alisema Serikali iliendelea kuleta unafuu zaidi kwa waajiri kwa kupunguza kiwango cha kodi ya malimbikizo ya madeni ya michango ya nyuma kutoka asilimia kumi (10%) hadi asilimia mbili (2%).

“Hii yote inalenga kuhamasisha waajiri ambao hawajajisajili waweze kujisajili na watekeleze wajibu wao wa kulipa michango kwa ajili ya kulinda wafanyakazi wao dhidi ya majanga yatokanayo na kazi.” Aliongeza Dkt. Mduma.

ULIPAJI WA MAFAO

Kabla ya kuanzishwa kwa WCF, malipo ya fidia nchini kwa mwaka mzima yalikuwa chini ya shilingi milioni 200 lakini baada ya kuanzishwa kwa WCF malipo yanaongezeka mwaka hadi mwaka.

“Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha toka kuanzishwa kwa Mfuko, idadi ya wanufaika wa Mfuko imefikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya shilingi Bilioni 49.44.

Akifafanua kuhusu Mafao, Mkurugenzi Mkuu alisema kuna Mafao ya aina mbalimbali ambayo Mfuko unatoa ikiwa ni pamoja na Huduma ya matibabu, Malipo ya ulemavu wa muda, Malipo ya ulemavu wa kudumu yanayotolewa kwa mfumo wa Pensheni ya kila mwezi, Malipo kwa anayemuhudumia mgonjwa (mfanyakazi), Huduma za utengamao, Msaada wa mazishi na Malipo kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki.

FIDIA MTANDAONI

Akieleza zaidi kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika Dkt. Mduma alisema Mfuko umeendelea kusogeza huduma karibu na wadau wake na sasa huduma zote muhimu zinapatikana nchi nzima kwa njia ya mtandao.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na Usajili wa wanachama ambapo mwanachama wa Mfuko huu ni waajiri, kupata cheti cha Usajili, Kuwasilisha Michango ya kila mwezi, Mfuko unapokea michango kupitia Nambari ya Udhibiti (Control Number) ambayo hupatikana kwa njia ya mtandao.

Huduma zingine ni Kuwasilisha Taarifa za Michango, Kufanya mabadiliko ya taarifa za wafanyakazi wao, Kuwasilisha Taarifa ya Ajali, Ugonjwa au Kifo cha Mfanyakazi kilichotokana na kazi na Kufuatilia mwenendo wa madai.

Aidha Dkt. Mduma aliwakumbusha waajiri wote Tanzania Bara kuwa, Kwa mujibu wa sheria, Mwajiri ndiye mwenye jukumu la kuchangia kwenye Mfuko na ni kosa la jinai kwa mwajiri kumkata mshahara Mfanyakazi wake kwa ajili ya kuchangia WCF.

Pia alisisitiza kwamba kupungua kwa kiwango cha uchangiaji hakutaathiri utoaji wa Mafao kwani Mfuko umeshirikiana na wataalam wa uhimilivu na kujihakikishia kuwa WCF itabaki imara na kuwa endelevu.

UWEKEZJI

Kuhusu uwekezaji, Dkt. Mduma alisema Mfuko una jukumu la kuwekeza fedha za ziada (investable funds) kwa mujibu wa Sheria na Muongozo wa Uwekezaji kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2015 uliotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (The Social Security Schemes Investment Guidelines, 2015).

“Asilimia 89.76 ya uwekezaji wa Mfuko upo kwenye Hati Fungani za Serikali, lakini pia Mfuko umewekeza katika Kiwanda cha Chai Mponde kilichoko Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.” Alibainisha

Aidha alisema hadi kufikia tarehe 30 Juni 2022, Mfuko umekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 241.48 toka kwenye mapato yatokanayo na uwekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akiwaeleza waandishi wa habari majukumu ya WCM Machi 2, 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akiwaeleza waandishi wa habari majukumu ya WCM Machi 2, 2023.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa, akizungumza (Kulia) ni Dkt. John Mduma.
Mtaalamu wa Takwimu WCF, Bw. James Tenga
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mfanyabiashara wa bidhaa za vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja.Bw.Seif Khamis Ali, alipofanya ziara ya kustukiza leo 18-2-2023 na katika marikiti kuu darajani na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia mchele wa Mbeya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-2-2023,na kuzungumza na Mfayabishara wa Bidhaa za Vyakula katika marikiti hiyo Bw.Seif Khamis Ali na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kusalimiana na Watalii wakitembelea Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kutembelea Wafanyabishara ya vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Unguja leo 18-2-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Mfanyabishara wa Nyama ya Ng’ombe katika Soko la Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-2-2023, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti hiyo kuangalia hali ya bidhaa ya vyakula.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akilipia Nyama ya Ng’ombe baada ya kuinunua kwa Bw.Ali Hashim mmoja wa Wafanyabiashara katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo 18-2-2023, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu)