Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kujipamba na Qurani Tukufu kwa kuishi kwa kufuata miongozo na mafundisho yake, huku akiwasisitiza kuifanya Qurani kuwa dira ya maisha yao ya kila siku.

Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito huo leo Januari 31, 2026, aliposhiriki Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qurani yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Altijarah Al Arabia ya Oman na Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, yaliyofanyika katika Msikiti wa Jamiu Zanzibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema kuishi kwa mujibu wa Qurani kunajenga maadili mema, heshima na mshikamano katika jamii, mambo ambayo ni msingi muhimu wa amani, utulivu na maendeleo endelevu ya Taifa. Aidha, amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla kuendeleza umoja, kusaidiana na kushikamana ili kupata baraka za Mwenyezi Mungu.

Katika hotuba yake, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuimarisha malezi bora ya vijana, kuishi kwa kupendana na kulinda amani ya nchi, akieleza kuwa misingi hiyo ni nguzo muhimu katika kujenga jamii yenye maadili na Taifa lenye maendeleo.

Rais Dkt. Mwinyi pia ameipongeza Taasisi ya Altijarah Al Arabia ya Oman pamoja na Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuandaa mashindano hayo, akitambua mchango wao mkubwa katika kuihudumia jamii kupitia sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, chakula na huduma za kijamii. Amehimiza kuendelezwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi hizo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa manufaa ya wananchi.

Vilevile, amewapongeza washiriki wote wa mashindano hayo ya kimataifa na kuwahimiza kuendelea kushikamana na Qurani Tukufu sambamba na taaluma walizonazo ili kufanikisha mafanikio zaidi duniani na Akhera.

Mashindano hayo yamewakutanisha washiriki sita kutoka nchi za Ujerumani, Uganda, Tanzania, Urusi, Canada na Brazil, ambapo Ndg. Usama Barghouth kutoka Ujerumani ameibuka mshindi wa kwanza baada ya kuonesha umahiri mkubwa katika kuhifadhi Qurani, na kutunukiwa kombe, cheti pamoja na zawadi ya shilingi milioni 20.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: