Dar es Salaam — Benki ya Exim Bank Tanzania imeandaa hafla ya futari kwa wateja wake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mahusiano ya karibu yanayojengwa juu ya uaminifu, uwajibikaji na maadili ya pamoja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Jaffari Matundu, alisema mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya kutafakari na kuimarisha misingi ya maadili mema katika maisha na biashara.
Alisisitiza kuwa benki hiyo inathamini mahusiano na wateja wake zaidi ya miamala ya kifedha, akieleza kuwa dhamira yao ni kujenga imani, kupanua fursa na kugusa maisha ya watu kwa namna chanya.
Katika hatua ya kuendeleza ujumuishi wa kifedha, benki hiyo imeendelea kupanua mtandao wake wa matawi kwa kufungua ofisi katika maeneo ya Kahama, Ubungo na Paje, huku mipango ikiendelea kufungua tawi jingine Geita, lengo likiwa kusogeza huduma karibu zaidi kwa wafanyabiashara na wananchi.

Matundu alisema uaminifu wa wateja ndio mtaji mkubwa wa benki hiyo, akiahidi kuendelea kutoa huduma bora zinazolenga kusaidia ukuaji wa biashara na maendeleo ya wateja wake kwa muda mrefu.
Hafla hiyo iliwakutanisha viongozi wa dini, wateja na wageni waalikwa mbalimbali katika mazingira ya mshikamano, tafakari na kuimarisha ushirikiano kwa maendeleo ya pamoja.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: