Articles by "HABARI MAKAMU WA RAIS"
Showing posts with label HABARI MAKAMU WA RAIS. Show all posts
Na Mwandishi Wetu, JAB.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amempongeza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Silaa kwa kuunda Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari mapema mara baada ya kuteuliwa.

Balile amesema hiyo ni hatua kubwa kwani imechukua miaka Nane tangu kutungwa kwa Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 inayotamka uundwaji wa bodi hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Novemba, 2024 wakati akiwasilisha hoja za jukwaa hilo mbele ya Waziri kwenye Kikao cha kwanza cha kufahamiana na Wajumbe wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) kilichofanyika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.
“Tunakushukuru sana Mheshimiwa kwa sababu imechukua miaka Nane tangu Sheria imepita 2016 na Bodi ilikuwa haijawahi kuundwa na leo tumesikia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Bw. Patrick Kipangula, siyo mgeni sana kwetu lakini leo tumemsikia kwa cheo kipya, tunashukuru sana na tunampongeza sana,” amesema Balile akionesha kuridhishwa na Hatua hiyo ya Waziri Silaa kuunda Bodi ya Ithibati.

Waziri Silaa aliiteua Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Septemba 18 na kumteua Mwandishi wa Habari Nguli Tido Mhando kuwa Mwenyekiti wa Kwanza na wajumbe wengine sita kutoka Taasisi za Habari kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Huduma za Habari.

Wajumbe wa Bodi hiyo ni Bw. Thobias Makoba, Mgaya Kingoba, Dkt. Rose Reuben Mchomvu, Dkt Egbert Mkoko na Laslaus Komanya.
Akizungumza na Wadau wa Habari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, tarehe 19 Novemba, Waziri Silaa alibainisha kuwa uzinduzi rasmi wa bodi hiyo muhimu utafanyika mapema mwezi Disemba, 2024 na kwamba itafungua njia ya safari ya kuanzisha Baraza Huru la Habari na pia Mfuko wa Mafunzo kwa Wanahabari na tathimini ya hali ya uchumi kwa vyombo vya habari.

Katika hoja yake Balile alimuomba Waziri kuwa na kikao kazi kitakachogusia Sera ya Habari, Sheria na mfuko wa mafunzo ili kupata uelewa wa pamoja wa namna ya kuiboresha tasnia ya Habari na Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Ombi kama hilo pia liliwasilishwa na Mwenyekiti wa CoRI, Ernest Sungura aliyemuomba Waziri katika vikao vijavyo kuwa na majadiliano ya namna Baraza Huru la Habari lililoundwa na Sheria ya Huduma za Habari litakavyoendesha majukumu yake ili kujitofautisha na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ili kuondoa mgongano.
Picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifafanua jambo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Kulia ni mtangazaji wa kipindi hicho, Janeth Leornard na Rajab Rajab.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifafanua jambo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Pamoja nae ni mtangazaji wa kipindi hicho, Janeth Leornard.
Mtangazaji wa kipindi Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1, Bi.Janeth Leornard akimuuliza swali Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akifanya mahojiano kwenye kipindi cha by Jambo kinachorushwa na TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024. Kushito ni Rajab Rajab mtangazaji mwenza orwa kipindi hiko.
*************
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa na mambo mapya kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha wafungwa kwa upande wa Tanzania Bara na wanafunzi wa vyuo vya mafunzo kwa upande wa Zanzibar na kuwaruhusu wapiga kura kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zao kwa njia ya mtandao.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa hewani na kituo cha televisheni cha TBC1 jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 2024, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K amesema kuwa Tume tayari imeweka utaratibu wa kuwaandikisha wafungwa na wanafunzi hao na mfumo wa kuboresha taarifa mtandaoni upo tayari.

Kailima amefafanua kuwa utaratibu wa kuandikisha wafungwa na wanafunzi utazingatia matwaka ya sheria ambapo waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita ndio watakaoandikishwa.

Akizungumzia suala la kuanza mchakato wa uboreshaji wa Daftari mtandaoni, Bw. Kailima amesema Tume imejenga mfumo ujulikanao kama OVRS (Online Voters Registration System) utakaomwezesha mpiga kura anayeboresha taarifa zake kuanzisha mchakato mtandaoni na baadae kwenda kwenye kituo ili amalizie taratibu na kupata kadi yake ya mpiga kura.

Uboreshaji wa taarifa kwa njia ya mtandao una masharti, kwa wale ambao wanataka kurekebisha taarifa zao ni lazima wawe na namba ya NIDA, lakini, mpiga kura anayehamisha taarifa zake hatalazimika kuwa na namba ya NIDA., amesema Bw. Kailima.

Amefafanua kuwa namba ya NIDA ni muhimu kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa za mpiga kura ambazo zinarekebishwa kwenye Daftari.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amefafanua kuwa, wanaokwenda vituoni kujiandikisha kwa mara ya kwanza hawatalazimika kuwa na namba ya NIDA.

Akitoa hotuba ya kutangaza tarehe ya uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari ambao unatarajiwa kufanyika mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024, Mwemyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele alisema kuwa kwa Tanzania Bara kuna vituo vya kuandikisha wapiga kura 130 vilivyopo kwenye magareza na kwa Zanzibar kuna vituo 10 vilivyopo kwenye Vyuo vya Mafunzo.
Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakisherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakipita mbele ya jukwaa kuu.
Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakiwa katika maandamano ya Kuingia katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanafanyika Kitaifa.
Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakiwa katika Picha ya Pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa yanafanyika jijini Arusha.
Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakiwa katika Picha ya Pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa yanafanyika jijini Arusha
-----
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo tarehe 1 Mei, 2024 imeungana na Watanzania kote nchini kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama Mei Mosi.

Sherehe hizo ambazo zimefanyika kitaifa jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa huku mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwakabidhi mipira baadhi ya manahodha wa timu za michezo mbalimbali mara baada ya kufungua rasmi Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanayofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora tarehe 06 Juni 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipuliza filimbi kuashiria Ufunguzi rasmi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanayofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora tarehe 06 Juni 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi, Wakufunzi, Walimu , Wanafunzi na Wananchi mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yanayofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora tarehe 06 Juni 2023.



MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kuboresha mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania yaani UMITASHUMTA na UMISSETA na kuyafanya kuwa kisima cha wanamichezo mahiri wa Taifa.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kitaifa yanayofanyika katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora. Ameeleza kwamba Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuunga mkono wanamichezo na kuzipa kipaumbele sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili ziweze kufaidisha vijana wengi zaidi. Pia amesema kupitia michezo serikali itaendelea kutoa fursa kwa wanamichezo wanaofanya vizuri zaidi kushiriki katika mashindano ya kimataifa ili kuendelea kuwajengea uzoefu.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango ametoa wito kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha kila shule ya Msingi na Sekondari ina mwalimu wa michezo walau mmoja ili kuweza kuimarisha michezo shuleni na kuwezesha somo la michezo kufundishwa kitaalamu. Pia amewataka kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo yanalindwa, na kutobadilishiwa matumizi. Aidha amesema ujenzi wa shule mpya unapaswa kuwa na maeneo ya kutosha kwa ajili ya viwanja vya michezo na upandaji miti.

Hali kadhalika Makamu wa Rais amewasihi wasimamizi wa elimu katika ngazi zote nchini kuzingatia ratiba ya michezo shuleni ili kuwapa wanafunzi muda stahiki kushiriki katika michezo hali itakayopelekea kuibua na kuendeleza vipaji vyao.

Vilevile Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Michezo kuangalia namna ya kushirikiana na wadau wengine wa michezo kubuni na kuandaa mipango ya kuwaendeleza vijana wenye vipaji katika michezo na pia kuwapa motisha wanafunzi wanaoshiriki na kufanya vizuri katika michezo. 

Amesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki kwa kushirikiana na Wizara ya Michezo zinapaswa kutafuta fursa mbalimbali za ufadhili ili kuwezesha wanafunzi kubadilishana uzoefu (exchange programs) na kunolewa zaidi katika vilabu mashuhuri vya michezo duniani au kutoka kwa wataalamu wa kimataifa katika fani mbalimbali za michezo.

Kwa upande wake Waziri Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Angellah Kairuki amesema Wizara imeendelea kutoa fedha kila mwaka kwaajili ya mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA pamoja na kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo kwaajili ya shule za msingi na sekondari.

Mhe. Kairuki amesema mashindano hayo yameweka mchango na alama kwa kutoa wachezaji katika timu ya taifa na ambao wameendelea kuiwakilisha vema nchi katika mashindano ya kimataifa. Ameongeza kwamba zaidi ya asilimia 80 ya wachezaji katika timu za taifa za vijana kama Serengeti Boys, Serengeti Girls na Ngongoro Heroes wametokana na mashindano hayo.




Awali akitoa taarifa ya mashindano hayo, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amesema lengo kuu la Mashindano hayo ni kukuza vipaji vya michezo na taaluma za wanafunzi. Ameongeza kwamba uendelezaji wa UMITASHUMTA na UMISSETA unatekeleza azma ya serikali ya kukuza sekta ya michezo kwa kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji pamoja na kujenga umoja wa kitaifa, upendo na mshikamano. Ametaja faida za michezo hiyo ikiwemo kuimarisha afya na ukakamavu miongoni mwa washiriki, kubadilishana ujuzi,maarifa na uzoefu katika michezo pamoja na kuimarisha taaluma ya michezo miongoni mwa wanafunzi.

Mashindano ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2023 yanahusisha wanamichezo wanafunzi 3,164 huku mashindano ya UMISSETA kwa mwaka 2023 yatahusisha jumla ya wanafunzi wanamichezo 3,360.
MWANZA

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani 2023.

Maadhimisho ya mwaka huu yanayo kwenda na kauli mbiu isemayo 'Tanzania Bila Ajali Inawezekana Timiza Wajibu Wako’ yamefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) ambaye ametoa wito kwa watanzania wote kuzingatia sheria za barabarani zilizowekwa ili kupunguza ajali.

"Jukumu la usalama barabarani ni la kila mmoja wetu na sio Serikali pekee. Tushirikiane kwa pamoja kuonyana kila mmoja wetu anapovunja sheria za usalama barabarani kwa ajili ya kupunguza ajali na kuokoa maisha", alisema Waziri Mkuu wakati akifungua rasmi Maadhimisho hayo jijini Mwanza.

Sambamba na kufungua maonesho hayo, Mhe. Waziri Mkuu alikabidhi vyeti vya udhamini na ushiriki ambapo WCF ni mmoja kati ya wadau hao.

Akizungumza kwa upande wa WCF mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. James Tenga amesema Jeshi la Polisi limekua mshirika wa karibu na WCF katika kurahisisha utoaji wa fidia kwa wakati kwa wafanyakazi wanaopata ajali hususan za barabarani.

"Jeshi la Polisi limeendelea kuwa mshirika muhimu sana wa WCF. Polisi wamekuwa na msaada mkubwa sana katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa kutoa taarifa za uthibitisho wa ajali hususan za barabarani na kuhakikisha haki inapatikana kwa wafanyakazi waliopata ajali wakiwa katika utimizaji wa majukumu ya kazi kulingana na mikataba yao ya ajira’. Amesema Tenga.

“ Kauli mbiu ya 'Tanzania Bila Ajali Inawezekana Timiza Wajibu Wako’ inaendana na majukumu ya Mfuko ya kuhakikisha tunashiriki katika kupunguza ajali zinazotokana na kazi nchini, sambamba na kupunguza vifo kutokana na ajali za Barabarani kwa Wafanyakazi wakati wakitekeleza majukumu yao ya kazi.”

"Tunategemea Ushirikiano wa WCF na Jeshi la Polisi kuendelea kuimarika ili kuongeza tija kwenye utoaji wa haki ya msingi ya fidia kwa wafanyakazi na kupunguza matukio ya ajali za barabani".

Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani 2023 yamefanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha ambapo taasisi mbalimbali za Umma na binafsi zimeshiriki.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiambatana na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango,leo tarehe 17 Machi 2022 ameshiriki Kumbukizi ya Mwaka Mmoja wa Kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli , iliofanyika Chato mkoani Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume na baadae atazindua matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi 2020/21, kwenye ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Novemba 24, 2021. Kulia ni Mkewe Mary Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar kuzindua Matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi 2020/21
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa meneja chapa wa mamlaka ya bandari ya Singapore bwana Eugene Tay namna banadari hiyo inavyotumia teknolojia katika kurahisisha upakiaji na upakuaji makasha.Novemba 18,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akitazama kupitia chumba maalum zoezi la upakiaji na upakuaji wa mizigo kisasa katika Bandari ya Singapore wakati alipotembelea bandari hiyo . Novemba 18,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka Mkuu wa Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore Chris Chan kuhusu matumizi ya bandari hiyo kwa kutumia mitambo maalum ya Tehama katika kupakia na kupakua mizigo kwenye meli wakati alipotembelea Bandari hiyo Novemba 18, 2021.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore Chris Chan wakati alipotembelea Bandari hiyo Novemba 18,2021. Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Balozi wa Tanzania Nchini India Baraka Luvanda.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 18 Novemba 2021 ametembelea Bandari ya nchi ya Singapore na kujionea namna inavyofanya kazi.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alishuhudia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kufanya kazi katika bandari hiyo ikiwemo upakuaji na upakiaji makasha na mizigo, ukaguzi wa mizigo pamoja na ufuatiliaji makasha wakati wote yanapokMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 18 Novemba 2021 ametembelea Bandari ya nchi ya Singapore na kujionea namna inavyofanya kazi.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alishuhudia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kufanya kazi katika bandari hiyo ikiwemo upakuaji na upakiaji makasha na mizigo, ukaguzi wa mizigo pamoja na ufuatiliaji makasha wakati wote yanapokuwa safarini.

Akitoa maelezo namna bandari hiyo ilivyopiga hatua kubwa katika kipindi cha muda mfupi makamu wa Rais wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore anayeshugulikia masuala ya biashara bwana Ong Seow Leong amesema bandari hiyo imewekeza katika mafunzo pamoja na ubunifu uliopelekea kuongezeka kwa teknolojia inayotumika hivi sasa katika kutoa huduma ikiwemo kuweza kufanikiwa kushusha na kupakia makasha laki moja ndani ya siku moja.

Amesema bandari ya Singapore imekua na mtandao na bandari zingine duniani hivyo kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi wa bandari hiyo. Aidha ameongeza kwamba Bandari ya Singapore imekuwa ikiweka mkazo katika kutafuta masoko pamoja na kufanya tafiti zinazoweza kuongeza watumiaji wa bandari hiyo.

Katika hatua nyingine Bwana Leong ameeleza kuwa ni lazima kuwepo na mipango ya muda mrefu katika uendeshaji wa bandari na tayari nchi ya Singapore inaendelea na ujenzi wa bandari mpya na ya kisasa ambayo kwa miaka ijayo itaweza kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania itashirikiana na Uongozi wa Bandari ya Singapore katika kutoa mafunzo kwa watumishi wa bandari za Tanzania pamoja na kupeleka watalaamu wa bandari kutoka Singapore kwenda Tanzania ili kushirikiana katika kufanya maboresho ya haraka hasa bandari ya Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore Mhe.Teo Sieng Seng mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi Nchini Singapore. Pembeni ni Balozi wa Tanzania nchini India Baraka Luvanda pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk. Novemba 15, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore Mhe.Teo Sieng Seng mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi Nchini Singapore. Makamu wa Rais yupo Nchini Singapore kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ). Novemba 15, 2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Waziri wa Uchumi na Biashara za kimataifa wa Ufaransa Mhe. Franck Riester, Ikulu Jijini Dar es salaam. Oktoba 19,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha Umoja Waziri wa Uchumi na Biashara za kimataifa wa Ufaransa Mhe. Franck Riester mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam. Oktoba 19,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchumi na Biashara za kimataifa wa Ufaransa Mhe. Franck Riester,(Kulia) Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mabalozi kutoka Tanzania na Ufaransa , Ikulu Jijini Dar es salaam. Oktoba 19,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Oktoba 19,2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uchumi na Biashara za kimataifa wa Ufaransa Mhe. Franck Riester, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine Waziri Riester ameleta salamu maalum pamoja na mwaliko Rasmi wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Waziri Riester amesema Ufaransa inatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania ikiwemo kuboresha mazingira ya biashara pamoja na kuleta usawa wa kijinsia mambo ambayo pia yanatiliwa mkazo na serikali ya Ufaransa.

Amesema Ufaransa imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania kwa manufaa ya nchi zote mbili huku akitoa mfano wa kuanzishwa kwa usafiri wa ndege wa moja kwa moja kutoka Paris Nchini Ufaransa hadi Zanzibar ulioanza hivi karibuni ambao ulisimama kwa miaka 47. Waziri huyo wa Uchumi wa Ufaransa ameambatana na Wafanyabiashara mbalimbali kutoka Ufaransa wenye nia ya kuwekeza nchini

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji kutoka Nchini Ufaransa na kuwahakikishia Tanzania ni Nchi salama kuwekeza iliojaariwa rasilimali nyingi na fursa lukuki. Amesema pamoja na changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na Uviko 19, serikali imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali kupambana na hali hiyo ikiwemo kutoa chanjo ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha amesema Ufaransa imekua kati ya wadau wakubwa wa maendeleo nchini Tanzania na uwekezaji katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Miundombinu , Elimu pamoja na Maji huku akiwakaribisha kuwekeza katika sekta ya Afya hususani ujenzi wa viwanda vya dawa, sekta ya Utalii na Nishati.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mawaziri kutoka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania.