Articles by "HABARI MAHAKAMANI"
Showing posts with label HABARI MAHAKAMANI. Show all posts
Wakili Peter Njau akiongea na vyombo vya habari.

Na Vero Ignatus, Arusha.

Mahakama kuu kanda ya Arusha imesimamisha utekelezaji wa Amri iliyokuwa imetolewa na serikali kupitia tangazo LA serikali namba 673 ya mwaka 2024 la kufuta vijiji na kata na vitongoji katika wilaya ya Ngorongoro.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Ayubu Mwenda Augusti 22,2024 ambapo alisikiliza maombi madogo ya zuio yaliyowasilishwa na ndugu Isaya Ole posi mwananchi wa ngorongoro kwa kupitia Wakili wake Peter Njau

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Jaji Mwenda aliridhia maombi hayo madogo na kukubali zuio la kusimamisha tamko hilo kupisha usikilizaji wa maombi ya msingi ,hadi amri ya Mahakama itakavyoelekeza na vinginevyo.

Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea Peter Njau alisema awaki kwa wananchi wa ngorongoro kuliweza kitokea taharuki kutokana na tangazo lililokuwa umetolewa na serikali kupitia mamlaka ya mji mdogo wa ngorongoro la kuwataka wakazi wake kuhama, ila baada kusikikizwa kwa pande zote mbili Jaji aliweza outta Amri ya kuzuia

"Mteja wangu aliweza kuniomba kumuwakilisha katika shauri kuweza kuomba Mahakama itazame uhalali wa Amri ole ni kuweza kuleta shauri lile mahakamani na kulisajili maombi madogo na yalisikilizwa kwa pande zote mbili na aliweza kutoa Amri ya kuzuia" Alisema Wakili Peter Njau"
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor akifungua kikao kazi maalum kwa ajili ya kupokea maoni na mapendekezo ya kuanzishwa kwa Mfumo wa kuratibu Ajira, Maadili na Nidhamu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama leo tarehe 6 Agosti, 2024 mjini Morogoro.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzaniua Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa Kikao Kazi Maalum kwa ajili ya kupokea maoni na mapendekezo ya kuanzishwa kwa Mfumo wa kuratibu Ajira, Maadili na Nidhamu wa Tume leo tarehe 6 Agosti, 2024 mjini Morogoro.
Sehemu ya Viongozi wa Tume, Mahakama pamoja na Wadau wakiwa kwenye kikao kazi maalum kwa ajili ya kupokea maoni na mapendekezo ya kuanzishwa kwa Mfumo wa kuratibu Ajira, Maadili na Nidhamu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama leo tarehe 6 Agosti, 2024 mjini Morogoro. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya.
Sehemu ya Watumishi wa Tume, Mahakama pamoja na Wadau wakiwa kwenye kikao kazi hicho. Wa pili Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa Bi. Souz Ngate.
Sehemu ya Viongozi wa Mahakama na Wadau wakiwa kwenye kikao kazi hicho. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimawatu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume, Mahakama pamoja na wadau mara baada ya kufungua kikao kazi maalum kwa ajili ya kupokea maoni na mapendekezo ya kuanzishwa kwa Mfumo wa kuratibu Ajira, Maadili na Nidhamu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama leo tarehe 6 Agosti, 2024 mjini Morogoro.

Na Lydia Churi na Evelyne Odemba- Morogoro.

Tume ya Utumishi wa Mahakama inakusudia kuanzisha mfumo wa kielekitroniki utakaoratibu masuala ya Ajira, Maadili na nidhamu kwa watumishi wa Mahakama.

Katika mchakato wa kuanzishwa kwa Mfumo huo, leo Agosti 6, 2024 Tume imekutana na wadau wake muhimu katika kikao kazi kilichoanza mjini Morogoro kwa lengo la kupokea maoni na mapendekezo kwa lengo la kuanzisha mfumo huo utakaorahisisha utendaji kazi na kuleta uwazi zaidi.

Akifungua rasmi kikao kazi hicho, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor alisema kuanzishwa kwa mfumo wa Kielekitroniki wa Ajira, Maadili na nidhamu ndani ya Tume ya Utumishi wa Mahakama ni muendelezo wa safari mageuzi ya mfumo ya Mahakama ya Tanzania ili kuboresha shughuli za utoaji haki nchini.

”Katika dunia ya sasa teknolojia inakua kwa kasi na shughuli nyingi za Serikali inafanywa kwa mfumo huo, kwa kutambua hili, Tume imeona ni vema kuwa na mfumo wa kielekitroniki utakaoratibu masuala ya Ajira, Maadili na Nidhamu kwa watumishi wa Mahakama”, alisema.

Aidha, Jaji Mansoor alitoa rai kwa wadau kutoa michango ya mawazo itakayozaa matunda yatakayowezesha kujengwa kwa mfumo bora zaidi wa ajira ambao utafungamanishwa na mfumo wa kielekitroniki wa uendeshajiwa Kamati za maadili ambazo Wenyeviti wake ni wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya.

Awali akitoia neno la utangulizi, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kupata maoni ya wadau kuhusu uanzishwaji wa mfumo ambao utaleta mabadiliko ya Utendaji kazi wa Tume.

“Nia yetu ni kuona kwamba Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania inaenda kuwa kitovu cha mageuzi ndani ya Afrika na duniani kote katika matumizi ya TEHAMA”, alisema.

Alitaja baadhi ya mada zilizowasilishwa katika kikao kazi hicho kuwa ni pamoja na rasimu ya mafunzo kuhusu mfumo huo, rasimu ya masuala ya ajira, kushirikishana uzoefu wa masuala ya TEHAMA na kujadiliana namna ya kuboresha mfumo huo ulioanza kujengwa.

Alisema kuwa ujio wa mfumo huo utasaidia katika kusimamia rasilimali watu, ajira, maadili na nidhamu na utakuwa na manufaa kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama na watanzania kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Bw. Jocktan Bikombo alisema kuwa Tume imedhamiria kuanzisha kuanzisha Mfumo ambao utasaidia kupanua wigo wa kiutendaji kazi wake.

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo cha kikatiba kilichopewa jukumu la kusimamia uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania. Moja ya jukumu lake ni kusimamia Maadili ya Maafisa Mahakama ili kuhakikisha Mhimili wa Mahakama unatekeleza jukumu lake la msingi na la kikatiba la kutoa haki kwa wananchi.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Dkt.Damas Ndumbaro (Mb) akipokea machqpisho mbalimbali kutoka kwa Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rehema Nyagawa wakati alipotembelea banda la Tume Leo Januari 26,2023 katika maonesho ya wiki ya sheria kitaifa inayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Dkt.Damas Ndumbaro (Mb) akipokea machqpisho mbalimbali kutoka kwa Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, akipatiwa eklimu ya mpiga kura wakati alipotembelea banda la Tume Leo Januari 26,2023 katika maonesho ya wiki ya sheria kitaifa inayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo leo Januari 23,2023 wakati alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesho ya wiki ya sheria kitaifa inayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani Mhe. Salma Mussa Maghimbi tarehe 27 January, 2023 ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodom.
Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani Mhe. Salma Mussa Maghimbi tarehe 27 January, 2023 ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodom.
Jaji Mfawadhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani Mhe. Salma Mussa Maghimbi akipatiwa machapisho mbalimbali ya Tume.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh.Rosemary Staki Senyamule akipokea machapisho mbalimbali ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Tume, Titus Mwanzalila (kushoto) wakati kiongozi huyo alipotembelea Banda la Tume, Januari 26,2023 katika maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Anthony Mwakitalu ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupatiwa Elimu ya Mpiga Kura katika Maonesho ya Wiki ya Sheria Januari 25,2023. Maonesho ya Wiki ya Sheria yanaendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Anthony Mwakitalu ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupatiwa Elimu ya Mpiga Kura katika Maonesho ya Wiki ya Sheria, Januari 25,2023. Maonesho ya Wiki ya Sheria yanaendelea katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Viziwi Tanzania Makao Makuu Dodoma Mchungaji Frank Sarungi tarehe 27 Januari 2023, ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Rehema Nyagawa akizungumza Katibu wa Wanawake Chama cha Viziwi Tanzania Mkoa wa Dodoma Bi Amina Issah wakati alipotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Watu wenye ulemavu wafurahishwa na kuwepo kwa wakalimani wa lugha ya alama inayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Banda la maonesho la Tume katika maoneolsho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura, Bi. Giviness Aswile alipotembelea banda la Tume
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe akizungumza na wadau alipotembelea banda la Tume
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Leonard Tumua akiwa katika banda la Tume
Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Amos Akim aakiwa katika Banda lka Tume.

Na Faustine Kapama na Magreth Kinabo-Mahakama

JAJI Mkuu wa Uganda, Mhe. Alfonse Chigamoy Owiny-Dollo leo tarehe 24 Mei, 2022 ameanza ziara ya siku tatu kuitembelea Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu ambapo amekutana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Wakiwa ofisini hapo, viongozi hao wamefanya mazungumzo mafupi yenye lengo la kujenga ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kimahakama na yale yanayohusu vyuo kuiwezesha Mahakama ya Uganda kujifunza jinsi ya kuijengea uwezo Taasisi ya Mafunzo ya Mahakama nchini Uganda (JTI).

Mhe. Owiny-Dollo, ambaye ameambatana na ujumbe wa maafisa 12 kutoka nchini Uganda alisema kuwa wamekuja nchini Tanzania kupata maarifa na wanatumaini kujifunza mengi kutoka katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na pia kupata uelewa jinsi ya kuijengea uwezo wa Taasisi yao.

Kwa upande wake, Mhe. Prof. Juma alisema kuwa anashukuru kwa ugeni huo kwa kuja nchini kwa sababu wamekuwa wakikutana Majaji Wakuu katika mikutano yao mbalimbali, lakini hawajawahi kukutana kujadili kuhusu vyuo vyao vya uongozi na sheria ili kubadilishana uzoefu.

“Hivi karibuni tulikutana nchini Zimbabwe (majaji wakuu) kuzungumzia masuala ya matumizi ya teknolojia na nadhani hili ni eneo jipya tunalotakiwa kwenda nalo,” alisema Mhe. Prof. Juma ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na pia Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald Ndika.

Jaji Mkuu wa Tanzania alibainisha kuwa tayari ameshakiagiza Chuo cha IJA kuandaa kozi za kuwajengea uwezo maafisa wa Mahakama ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.

"Nimekiomba chuo chetu kuangalia jinsi tunavyoweza kwenda kidigitali ili watusaidie katika eneo hili. Mahakama haiwezi kubaki nyuma katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwa Dunia na Serikali inatumia teknolojia hiyo," alisema.
Jaji Mkuu aliueleza ujumbe kutoka Uganda kuwa Mahakama ya Tanzania imewashirikisha wadau wengine katika mnyororo wa utoaji haki katika safari hiyo ya mabadiliko. Aliwataja baadhi ya wadau hao kama Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali(DPP), Jeshi la Magereza, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) na wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo aliwakaribisha wageni hao Tanzania na katika Chuo cha IJA ambapo aliwaahidi kuwa wakiwa Lushoto watapata fursa ya kutembelea maeneo ya chuo na vivutio mbalimbali vilivyopo katika Wilaya ya Lushoto.

Viongozi wengine waandamizi walioambatana na Jaji Mkuu wa Tanzania katika kuwakaribisha wageni hao ni Mkuu wa Chuo cha IJA na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Paul Kihwelo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina.

Miongoni mwa viongozi walioambatana na Jaji Mkuu wa Uganda ni Jaji Kiongozi wa Uganda, Mhe. Dkt. Flavian Zeija, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Uganda, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa JTI Uganda, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya JTI Uganda, Msajili wa Taasisi ya JTI Uganda na viongozi wa International Development Law Organization Uganda (IDLO).

Katika ziara yake, Jaji Mkuu wa Uganda anatarajia pia kutembelea maeneno mbalimbali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na vivutio mbalimbali vilivyopo katika Wilaya ya Lushoto.

Wakiwa IJA, wageni hao watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na viongozi wa Chuo hicho ikiwemo namna kinavyofanya kazi. Ziara hiyo ni sehemu ya ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Uganda na ujirani mwema kati ya nchi hizi mbili.
*Waridhishwa na Mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama 
*Wapewa picha ya hali ya uboreshaji huduma za Mahakama

Na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imetembelea Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania ambapo imeonyesha kuridhishwa na Mradi huo na kuipongeza Mahakama kwa uboreshaji wa miundombinu ya majengo yake.

Akizungumza leo tarehe 24 Mei, 2022 mara baada ya ukaguzi wa Mradi huo unaojengwa katika eneo la ‘NCC Link’ mkoani Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Sillo (MB) amesema kuwa Mahakama imepiga hatua kubwa katika uboreshaji wa huduma kwa lengo la kuwafikia wananchi.

“Kwanza nichukue fursa hii kwa niaba ya Kamati yetu ya Bunge ya Bajeti kumpongeza sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia uboreshaji wa Mahakama hapa nchini, tumepita kwenye jengo la Kituo Jumuishi na vilevile tumekagua Mradi huu mkubwa ambao ni wa kihistoria kwa Afrika, na jengo ambalo linatajwa kuwa la sita kwa ukubwa (6) kati ya majengo ya Mahakama duniani, kwa kweli ni maboresho makubwa sana katika mustakabali wa kutoa haki,” amesema Mhe. Sillo.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa wao kama Kamati ya Bajeti wameridhishwa na matumizi ya fedha na mwenendo wa ujenzi wa Mradi huo na kusema kuwa ni wakati muafaka sasa kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuendelea kuboresha taasisi nyingine zilizo chini ya mwamvuli wa Wizara hiyo ili waweze kwenda pamoja na kasi ya Mahakama.

Aidha, kabla ya kutembelea Mradi huo, Wajumbe hao walitembelea na kukagua jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki-Dodoma ambapo pamoja na ukaguzi walipata semina fupi iliyolenga kuwapa taswira ya hatua iliyofikiwa na Mahakama katika uboreshaji wa huduma zake.

Akizungumza wakati akiwasilisha Mada ya Utekelezaji wa Uboreshaji Huduma za Mahakama: Mafanikio na Changamoto, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel amewajuza Wabunge hao kuwa safari ya uboreshaji wa huduma za Mahakama ni muhimu kwa kuwa umelenga katika kurahisisha upatikanaji wa huduma mahsusi ya Mahakama ya utoaji haki kwa wananchi.

Prof. Ole Gabriel amewahakikishia Wabunge hao kuwa Mahakama itaendelea kutunza rasilimali hizo ambazo Mahakama imeaminiwa na Serikali na kuahidi kuwa wataendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi.

Wakichangia mada katika semina fupi iliyoandaliwa na Mahakama, Wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Makamo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Omari Kigua (MB), Mhe. Dkt Charles Kimei (MB), Mhe. Shamsi Nahodha na wengine wameipongeza Mahakama na kuiomba Wizara ya Katiba na Sheria kuboresha pia Taasisi nyingine zilizo chini ya mwamvuli ili ziweze kwenda sambamba na kasi ya uboreshaji wa huduma za Mahakama.

Naye, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geophrey Pinda amesema kuwa Wizara inaendelea na jitihada za kuboresha Taasisi za Sheria zilizo chini yake ili kwenda na kasi ya Mahakama hatimaye wananchi waweze kupata huduma ya haki bila vikwazo vyovyote.

Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao makuu ya Mahakama ambao umefikia asilimia 58 ya ujenzi wake utagharimu fedha za kitanzania shilingi 129,740,285,556.02 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 29 Desemba mwaka huu.
Mahakama Kuu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai ole sabaya na wenzake wawiliwaliokua wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja.

Uamuzi huo umetokea baada ya kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima kesi,pamoja na kutofautiana na mashahidi

"Hata hivyo, Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi."

Rufaa hiyo ya jinai namba 129/2021 imeletwa na Sabaya na wenzake hao wakipinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Aidha Sabaya na wenzake walikuwa wakipinga hukumu dhidi yao kwakuwa Mnamba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao ya msingi.

Waomba rufaa hao wanawakilishwa na Majura Magafu, (wakili) Moses Mahuna (wakili) Fauzia Mustafa,( wakili) Sylvster Kahunduka (wakili) Edmund Ngemela na Fridolin Bwemelo (wakili )ambao kwa pamoja walipinga hoja za wajibu rufaa na kuomba mahakama iridhie hoja zao 14 za rufaa na kuwaachia wateja wao huru.

Wajibu rufaa hiyo Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi Ofmedy Mtenga, Verediana Mlenza na Baraka Mgaya ambao, wanapinga hoja za mawakili wa waomba rufaa na kuiomba mahakama itupilie mbali rufaa hiyo.
Awali Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 kila mmoja, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu ikiwamo unyang'anyi wa kutumia silaha.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Mei 9, 2022 kuanza kusikiliza kesi ya kukutwa na nyara za serikali dhidi ya watuhumiwa 11 wakitanzania na raia mmoja wa Guinea baada ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo kukamilika na washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Washtakiwa hao ni Ally Ganzuuu Sharifu raia wa Guinea, Victor Mawala, Haruni Kassa, Abbas Hassan, Solomoni Mtenya, Musa Ligagabile, Khalfani Kihengele, Ismail Kassa, Kassim Saidi, Peter Nyachiwa, John Buhanza na Mussa Abdallah.

Mapema wakili wa Serikali, Candid Nasua alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Akisoma maelezo hayo mbele ya Hakimu mkazi Mwandamizi Roda Ngimilanga, Nasua amedai, washtakiwa hao ambao ni wafanyabiashara wanadaiwa, kati ya Aprili Mosi 2016 na Juni 24, 2016, Polisi walipata taarifa za kiuchunguzi kuwa kuna mtandao mkubwa wa uhalifu wa nyama pori ambao walikuwa wanauza, wananunua, wanapokea, kuhamisha na kusafirisha nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo.

Imedaiwa, wakiwa wanakaribia kusafirisha idadi kubwa ya meno ya tembo kutoka Tanzania, Juni 22, 2016 huko katika eneo la Maduka mawili Chang'ombe, askari walifanikiwa kuwakamata washtakiwa Haruni Kassa, Kihengele na Kassa.

Amedai upekuzi ulifanyika nyumbani kwa mshtakiwa Haruni Kassa kwa kusaidiana na mbwa maalum wa ukaguzi wa meno ya tembo ambapo walikuta chumbani shuka jeupe lililodariziwa likiwa limefunika silaha aina ya shotgun, risasi tano na simu mbili huku kwa mshtakiwa Abdallah anayeishi maeneo ya Mwanagati, walikuta begi la bluu lililokoza likiwa na meno ya tembo.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Juni 23, 2016, mshtakiwa Haruni Kassa, aliongoza polisi kwenda kumkamata mshtakiwa Hassan ambaye katika upekuzi alikutwa na simu sita, laptop mbili, magari matatu na matairi 170 ya pikipiki.

Mshtakiwa wanne anadaiwa kuwapeleka polisi kumkamata Juma Baguma ambaye kwa sasa ni Marehemu ambapo alimtaja mtu maarufu wa ununuzi wa meno ya tembo anayeishi nje ya nchi huku pia Akiwaongoza kumkamata mshtakiwa Anguzuu ambaye katika upekuzi huko nyumbani kwake Tabata Segerea, uliofanywa na askari pamoja na mbwa maalumu wa kunusa walikamata gari aina ya Isuzu Canter ambalo baada ya Mbwa huyo kunusa na gari kufunguliwa mlango, walikuta mashine za kupimia uzito mbili na katika bodi ya gari walitengeneza sehemu maalum ya kuhifadhia meno ya tembo.

Aidha askari pia walilikamata gari lingine aina ya Mitsubishi iliyokuwa ikitumika kusafirisha meno hayo.

Inadaiwa wakati wakiendelea na upekuzi, simu ya marehemu Baguma iliita aliamliwa kupokea ndipo katika maongezi yao alikuwa amepigiwa simu na mshtakiwa Mtenya akimtaka yeye na mshtakiwa Hasaan wakaonane Kimara Stop Over ili awauzie meno ya tembo.

Baguma aliongozana na Polisi hadi Kimara ndipo mshtakiwa Mtenya na Ligagabile walipokamatwa na katika upekuzi walikutwa na vipande sita vya meno ya Tembo katika gari, Toyota Fancago yenye namba za usajili T540 DDS.

Pia inadaiwa polisi wakiongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa walikwenda nyumbani kwa mshtakiwa Anguzuu ambapo walivunja mlango na kwa msaada wa mbwa wa kunusa walifanikiwa kukuta vipande 660 vya meno ya tembo kwenye viroba, vyenye thamani ya USD 12,145,000 ambazo ni sawa na Sh 4, 656,795,000 na USD 5652 ambazo sawa na Sh 12,270,492 na mashine za kupimia uzito.

Imedaiwa washtakiwa wakati wakihojiwa walikiri kufanya biashara hiyo haramu kwa muda mrefu, mshtakiwa wa kwanza alikubali kutumia gari iliyotengenezwa maalum kwa kuhifadhia meno ya tembo wakati wakisafirisha kuyapeleka kwenye stoo yao iliyopo Mbezi Msakuzi.

Aidha washtakiwa wakihojiwa mahakamani hapo wamekubali taarifa zao binafsi lakini wamekana kuhusika kutenda makosa hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 9, mwaka huu.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza alipokuwa akifunga Kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama awamu ya pili jana tarehe 14.04.2022 jijini Arusha. Amewahimiza watumishi wa Mahakama kutoa huduma bora ya haki kwa wote na kwa wakati.

Na Mary Gwera, Mahakama-Arusha

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Watumishi wa Mahakama nchini kuwa na desturi ya kufanya tathmini ya huduma wanazotoa kwa jamii ili kujua kama zinakidhi matarajio ya wananchi ya upatakanaji wa huduma ya haki kwa wakati.

Akizungumza jana tarehe 14 Aprili, 2022 jijini Arusha wakati akifunga Kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama awamu ya pili, Prof. Ole Gabriel amesema kuwa kwa kufanya hivyo utekelezaji wa Mpango Mkakati na Mradi wa uboreshaji wa huduma za Mahakama utafanikiwa.

“Moja ya mambo muhimu ya kuzingatia katika utekelezaji wa Mpango Mkakati ni kujua au kujiuliza wewe kama Mtumishi ni nini unachokitoa katika jamii, je unatoa huduma kwa uwazi, je huduma unayotoa inafikika kwa wananchi na je haki unayotoa ni ya kiwango gani? Hivyo ni muhimu kuzingatia haya ili kazi iweze kufanyika kwa ufasaha,” amesema Mtendaji Mkuu.

Aidha, Prof. Ole Gabriel pia ametoa rai kwa Watumishi kuacha tabia ya kulaumiana katika utekelezaji wa majukumu badala yake kufanya kazi kama timu moja na hatimaye kutoa mrejesho wa masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za Mahakama.

“Tusipende kulaumiana, tuwe na tabia ya kutoa mrejesho wa hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mpango Mkakati na Mradi wa Uboreshaji wa huduma za Mahakama, kwa kufanya hivi tutafanikiwa,” amesisitiza Prof. Ole Gabriel.

Kadhalika, Mtendaji huyo aliongeza kwa kubainisha baadhi ya mambo yanayokwamisha utekelezaji wa Mipango Mikakati mingi ambayo ni pamoja na ukosefu wa watu wenye fikra kubwa (great minded people), kutokuwa au kukosa umoja ‘team spirit’ miongoni mwa watekelezaji wa Mradi pamoja na Uongozi kutoshiriki katika maandalizi ya Mpango Mkakati.

Kwa upande wake, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma amewataka Wamiliki wa Maeneo ya Utekelezaji wa shughuli za Mradi (Strategic Objective Owners) kuwa na umiliki wa dhati wa maeneo yao na vilevile kutoa ushirikiano kwa Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama (JDU) ambacho kinaratibu utekelezaji wa shughuli zote za Mradi.

“Napenda kuwapongeza Waandaaji wa kikao hiki (JDU) pamoja na Washiriki wa Kada zote walioshiriki katika kikao kazi hiki, kazi iliyofanyika ni kubwa. Hivyo niwatake ‘SO-Owners’ kumiliki maeneo yenu pamoja na kutoa ushirikiano kwa Kitengo cha Uboreshaji wa Huduma za Mahakama (JDU) kwa kuwasilisha taarifa zinazotakiwa na mengineyo,” amesema Mhe. Chuma.

Mpango Mkakati wa Pili wa Mahakama (2020-2025) utatekelezwa kwa kiasi kikubwa na nyongeza ya Mkopo wa Benki ya Dunia wa Dola Milioni 90 baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Mradi uliokuwa na matumizi ya Dola milioni 65 ambazo Benki ya Dunia iliikopesha Serikali ya Tanzania kwa matumizi ya kuboresha huduma ndani ya Mahakama ya Tanzania.

Kikao kazi hicho kilichohusisha jumla ya Washiriki wapatao 250 wakiwemo Majaji, Wasajili wa Mahakama, Watendaji wa Mahakama na baadhi ya Watumishi wa Kada mbalimbali wakiwemo wa ngazi za chini (Wasaidizi wa Ofisi, Katibu Muhtasi, Watunza Kumbukumbu na wengineo) kililenga kufanya tathmini ya Mafanikio, changamoto ya Mradi wa awamu ya kwanza pamoja na mapitio ya awamu ya pili ya Mradi.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama.
Sehemu ya washiriki wa Kikao kazi hicho kilichohusisha jumla ya Washiriki wapatao 250 wakiwemo Majaji, Wasajili wa Mahakama, Watendaji wa Mahakama na baadhi ya Watumishi wa Kada mbalimbali wakiwemo wa ngazi za chini (Wasaidizi wa Ofisi, Katibu Muhtasi, Watunza Kumbukumbu na wengineo).
Mkuu wa kitengo cha Uboreshaji wa huduma za Mahakama, Naibu Msajili Mhe. Dkt. Angelo Rumisha akifafanua jambo wakati wa kufunga Kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama awamu ya pili.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa meza Kuu na baadhi ya Viongozi walioshiriki kwenye Kikao Kazi hicho, wa pili kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha Mhe. Ruth Massam, wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Leonard Magacha na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso wakati wa kikao hicho
Sehemu ya washiriki wa Kikao kazi hicho kilichohusisha jumla ya Washiriki wapatao 250 wakiwemo Majaji, Wasajili wa Mahakama, Watendaji wa Mahakama na baadhi ya Watumishi wa Kada mbalimbali wakiwemo wa ngazi za chini (Wasaidizi wa Ofisi, Katibu Muhtasi, Watunza Kumbukumbu na wengineo) kililenga kufanya tathmini ya Mafanikio, changamoto ya Mradi wa awamu ya kwanza pamoja na mapitio ya awamu ya pili ya Mradi.
Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Mhe. Ruth Massam akitoa neno wakati wa hafla ya kufunga Kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama awamu ya pili.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga Kikao kazi cha Mapitio ya Mpango Mkakati wa pili wa Mahakama wa 2020/2021-2024/2025 na Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama awamu ya pili.
(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)

Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewakikishia Wakazi Wa Tarafa ya Kiponzero kuwa kurejeshwa Kwa shughuli za kimahakama katika Kata ya Maboga hakutoathiri shughuli za kimahakama zinazoendelea kata ya Ifunda.

Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwasikiliza viongozi wa vijiji na kata katika tarafa ya Kiponzero juu ya ukarabati jengo la Mahakama na ujenzi wa choo katika mahakama hiyo iliyopo katika kijiji cha Kiponzero
Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewakikishia Wakazi Wa Tarafa ya Kiponzero kuwa kurejeshwa Kwa shughuli za kimahakama katika Kata ya Maboga hakutoathiri shughuli za kimahakama zinazoendelea kata ya Ifunda.

Akizungumza na viongozi wa vijiji na kata za Tarafa ya Kiponzero Mkuu wa Wilaya huyo alisema kuwa alipata malalamiko ya kuhamishwa kwa mahakama kutoka Kiponzero kwenda Ifunda jambo ambalo limenipelekea kulifanyia kazi suala hilo kushirikiana na mamlaka husika.

Alisema kuwa mahakama ya mwanzo Kiponzero itarudi na kufanya kazi zake katika kijiji cha kiponzero kama ambapo ilikuwa awali na kuwahudumia wananchi wote wa Tarafa ya Kiponzero

Moyo alisema kuwa kilichobakia ni makubaliano ya wananchi kuanza kuchangia ujenzi wa choo na kukarabati jingo la mahakama ambapo kinatakiwa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000)

Alisema kuwa viongozi wa vijiji vyote kumi na tano wamekubali kuchangia kiasi cha shilingi lakini nne (400,000) na mwisho wa michango ya wananchi ni tarehe 30/4/2022 ili zoezi la ukarabati na ujenzi wa choo uanze mara moja.

Moyo alisema kuwa Mahakama iliyopo Ifunda itaendelea na shughuli zake Wakati huo huo Mahakama ya mwanzo ya Kiponzero pia itakuwa ikitoa huduma kwa lengo la kusaidia wananchi kupata huduma za kimahakama kwa urahisi zaidi.

Alisema kuwa Tarafa ya Kiponzero inajiografia ngumu kidogo hivyo serikali imeamua kuwa wananchi ambao wapo karibu na mahakama ya Ifunda wataendelea kupata huduma za kimahakama Ifunda hivyo hivyo na wananchi waliopo karibu na kijiji cha Kiponzero nao watapata huduma hiyo.

katika kikao hicho viongozi wa Tarafa hiyo wamekubaliana Kwa pamoja Ili kufanikisha Ukarabati wa jengo la Mahakama ya Kiponzero Wananchi watachangia kiasi cha shilingi milioni sita na kinachosalia kitatolewa idara ya mahakama.

Aidha mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ametembelea ujenzi wa ofisi ya Afisa Tarafa ya Kiponzero na ujenzi unaendelea vizuri na hivi karibuni ofisi hiyo itaanza kufanya kazi.

Moyo alisema kuwa baada ya wiki mbili wananchi wa Tarafa ya Kiponzero wataanza kupata huduma kutoka kwa Afisa Tarafa katika makao makuu ya Tarafa hiyo katika kijiji cha Kiponzero.

Aliwaomba wananchi kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan ili aweze kuwaletea maendeleo na huduma zote muhimu karibu na wananchi.

Nao baadhi ya wenyeviti na watendaji wa vijiji,kata na Tarafa hiyo wamesema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan kuamua kuwasogezea huduma ya kimahakama karibu yao.

Walisema kuwa kulingana na ukubwa wa Tarafa hiyo kulikuwa kunawatesa baadhi ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kimahakama ili kupata haki zao ambazo wanakuwa wanazidai kisheria.
Amina said ni m kazi wa kijiji cha Maboga alisema kuwa wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi kwa kuwa mahakama ilikuwa mbali na maeneo yao kiasi kwamba kesi nyingi walishindwa kuzifaatili kutokana na kutumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo.