Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachilia huru mfanyabiashara maarufu Jennifer Jovin, anayefahamika zaidi kwa jina la Niffer (26), pamoja na mwenzake Mika Chavala (32), baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuondoa mashtaka dhidi yao.
Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatano Desemba 3, 2025, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya, mara baada ya DPP kuwasilisha hati ya Nolle Prosequi—taarifa rasmi ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka—kwa mujibu wa kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, marejeo ya mwaka 2023.
Hakimu Lyamuya alisema kuwa baada ya hati hiyo kuwasilishwa, mahakama haina mamlaka ya kuendelea kusikiliza shauri hilo, hivyo ililazimika kuwaachia huru washtakiwa hao mara moja.
Hati ya Nolle Prosequi hutoa mamlaka kwa DPP kusitisha mashitaka wakati wowote kabla ya hukumu kutolewa, bila kuhitaji kutoa sababu mahakamani.



Toa Maoni Yako:
0 comments: