.jpeg)
Na Happiness Katabazi.
RAIS Samia Suluhu Hassan Leo amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani George Mcheche Masaju Kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Kwa Mujibu wa taarifa kwa umma iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Leo Juni 13 imesema ...
Hongera sana mtani na rafiki yangu Masaju kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu .
Januari 10 mwaka 2025 , Rais Samia alimteua Jaji Masaju kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Aprili 21 mwaka 2023 , Rais Samia aliteua Jaji Masaju kuwa Mshauri wake wa masuala ya Sheria ( Advisor to the President - Legal Affairs) Na wakati akimteua kushika nafasi hiyo Jaji Masaju alikuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Novemba 5 mwaka 2015 , Masaju aliteuliwa mara ya pili kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Rais wa awamu ya Tano Marehemu Dr. John Magufuli ndiye akimteua Masaju kuwa AG .
Mara ya kwanza ilikuwa ni serikali ya awamu ya nne Januari 2 Mwaka 2015, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amestaafu wadhifa wa Cheo cha Rais , alimteua Masaju Kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ikiwa ni siku chake aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema ambaye kwasasa ni marehemu kujihudhuru wadhifa huo.
February mosi mwaka 2018 Rais Magufuli alimteua Masaju kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini.
Masaju ni miongoni mwa Wanasheria wa serikali wazalendo na wanaowaaminiwa kiutendaji na ndiyo maana zilipokuwa zikifunguliwa Kesi ambazo zilikuwa zikivuta hisia za watu Wengi Masaju alikuwa akivaa suti na gauni lake la uwakili na kutinga Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na kuiendesha Kesi hiyo yeye Mwenyewe akisaidiwana na vijana wake.
Na nilipokuwa Mwandishi wa Habari za mahakamani,nilipokuwa nikimuona Masaju Kubeba gauni jeusi na begi lilokuwa na Nyaraka za kuendeshea Kesi basi nilikuwa Nasema Kimolo moyo Kuwa upande wa wa pili Katika Kesi hiyo ujiandae kikamilifu .
Ushahidi mchache wa haya ninayoyasema kuhusu Masaju ambayo nilikushuhudia kwa macho yangu mwanzo hadi Mwisho ni Rufaa ya Kesi maarufu ya mgombea Binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila Katika Mahakama ya Rufaa nchini Masaju alikuwa kiongozi wa Mawakili wa serikali kuendesha Kesi hiyo ya kihistoria ambayo ikisikilzwa na jopo la Majaji Saba waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu wa wakati huo , Agustino Ramadhani, Masaju alifanikiwa Kujenga hoja na hatimaye jopo lilikubaliana naye na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu ambayo iliruhurusu Mgombea Binafsi.
Ushahidi wa pili, ni Mwaka 2014, katika kesi ya Kikatiba Na.24/2013 , Masaju aliwakilisha upande wa Mwanasheria Mkuu Katika Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Kituo ca Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)dhidi ya Waziri Mkuu iliyokuwa ukiomba Mahakama Kuu itoe Tafsiri ya Ibara ya 100 Kuwa wabunge wana Uhuru bila mipaka kwani Pinda alitoa Kauli Bunge akitaka Polisi iwapige wanaovunja Sheria za nchi.
Juni 6 Mwaka 2014 , Jopo la Majaji wa Tatu wa Mahakama Kuu Dar es Salaam, Fakji Jundu, Dk.Fauz Twaibu na Augustine Mwarija walitoa uamuzi wa Kuitupa Kesi hiyo kwa sababu Imeona walalamikaji walikuwa hawana Haki ya kisheria ya kushitaki Pinda.
Jopo hilo lilitoa uamuzi huo ambapo jaji Jaji Jundu alisema anakubaliana na pingamizi la awali lilowasilishwa na wakili wa mdaiwa (Pinda), Ambaye ni Naibu Mwanasheri Mkuu wa Serikali, George Masaju, ambalo lilikuwa likiomba Mahakama itoe amri ya kuifuta Kesi hiyo kwasababu walalamikaji hawana Haki a kisheria ya kuwashitaki wadaiwa na kwamba Waliokuwa na Haki ya kushitaki Pinda ni wananchi na siyo Taasisi hizo za walalamikaji.
LHRC na TLS walimshtakiwa Waziri Mkuu Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kauli aliyoitoa bungeni Juni 20 mwaka 2013.Ilidaiwa Katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo Waziri Pinda akijibu alisema, ‘ukifanya fujo…unaambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi, utapigwa tu, muwapige tu sababu tumechoka’.
Jaji Jundu alisema, Masaju Aliwasilisha pingamizi la awali akiomba kesi hiyo itupwe kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza, waliofungua hawakustahili kuifungua na iko kwa ajili ya kupoteza MUDa wa Mahakama.
Katika uamuzi huo, majaji walikubaliana na hoja tatu za pingamizi kuwa walalamikaji katika kesi hiyo hawakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo na kwamba walikosea taratibu za ufunguaji wa kesi kama hizo kwa kuwa walikiuka amri na kanuni zinazoongoza Mashauri ya Madai (CPC).
Katika hoja ya kwanza kuwa Pinda kama mbunge analindwa na Katiba, jopo hilo lilisema kuwa ni kweli wabunge wanalindwa na Katiba Ibara ya 100 (1) kuhusu haki na upendeleo (Previledge), yaani haki na uhuru wa mjadala na maoni. Hata hivyo, lilikataa hoja za utetezi kuwa wabunge wana kinga isiyo na mipaka ya kutokushtakiwa kwa kauli au jambo lolote walilolitamka bungeni.
“Ibara ya 100(1) ya Katiba haiwezi kujadiliwa mahali popote ikiwemo mahakamani, ibara hiyo inasema kwamba, kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.
“Ibara ya 100(2) inaweza kujadiliwa mahakamani, inasema kwamba bila kuathiri katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yoyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
“Mwananchi mmoja mmoja aliyeathirika na jambo lililozungumzwa na mbunge bungeni anaweza kushtaki lakini si taasisi kama ilivyo katika kesi hii,”alisema.
Alisema kutokana na sababu hizo, mahakama inatupilia mbali kesi hiyo kwa sababu waliofungua kesi, LHRC na TLS hawakustahili kisheria kufungua kesi hiyo kwa sababu hawakuathirika.
Kesi ya Tatu ni Kesi iliyovuta hisia za watu Wengi ni Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa Mwaka 2014 na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Kubenea alikuwa anaomba Mahakama hiyo itoe amri ya muda ya Kuzuia Bunge Maalum la Katiba lisiendelee na kazi kwasababu linavunja Sheria.
Hata hivyo Masaju aliwasilisha mapingamizi mawili ambayo yaliomba Mahakama hiyo itupilie Mbali Maombi ya Kubenea Kwani hayana Msingi na Mahakama hiyo ilitupilia mbali Maombi ya Kubenea na Bunge linaendelea na kazi zake.
Mifano ni mingi ya Kuonyesha Masaju Kabla ya kuteuliwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Januari 2 na Novemba 5 Mwaka 2015 , kuna kazi nzuri ya kuiwakilisha upande wa serikali Katika Kesi mbalimbali mahakamani aliifanya hivyo anastahili.
Ni neema ya Mungu na na rekodi yake ya Utendaji Kazi ndiyo imesabisha Marais wa wawili ya marehemu Dk.John Magufuli na rais wa Sasa Samia Suluhu Hassan wakuteue kushika nyadhifa hizo ikiwemo hii ya Jaji Mkuu ambayo umeteuliwa Leo Juni 13 mwaka huo ili amsaidie kuchapa kazi.
Wosia wangu wa Masaju endelea na msimamo wako ule ule wa kusimamia haki na Kusema ukweli bila woga.
Masaju ambaye kabla ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali na aliwahi kuwa mshauri wa Rais Kikwete katika masuala ya sheria ni mtu asiye penda kuburuzwa na mambumbumbu wa Sheria, ni mtu anayejali utu,heshima na Kupenda watu watii Sheria za nchi na ni mzalendo kwa taifa lake.
Hongera Mtani wangu Masaju, Mungu akuongoze katika nafasi hii ya Jaji Mkuu wa Tanzania.
0716 774494
6/13/2025


Toa Maoni Yako:
0 comments: