Articles by "h"
Showing posts with label h. Show all posts
MENEJA wa Wakala wa Vipimo (WMA) Phanuel Matiko, akizungumza na waandishi wa habari katika banda la WMA kwenye maonesho ya wakulima kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Na Okuly Julius - DODOMA.

MENEJA wa Wakala wa Vipimo (WMA) Phanuel Matiko amesema ili wakulima kuepuka kipimo cha lumbesa wanatakiwa kuacha tabia ya kuuzia mazao yao Shambani.

Matiko ameyasema hayo leo Agosti 7, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema kuwa ili wakulima kuepuka kipimo cha lumbesa wanapaswa kuacha tabia ya uuzaji wa mazao yao ya kilimo shambani.

"Wito wangu niwaombe wakulima kuacha tabia ya kuuza mazao yao shambani ili kuepuka lumbesa bali watumie mizani kwa kuuza mazao yao kwa kilo.

"Wakulima hawapaswi kuuza mazao yao kwa kutumia debe au kisado au vitu vingine vinavyofanana na hicho bali watumie mizani ili kuepuka lumbesa kwenye uuzaji wa mazao yao,"amesema.

Amesema pia wao ni wadau wakubwa kutokana na jukumu lao la kupima usahihi wa mizani, mita za maji, umeme pamoja na pampu za mafuta.

"Moja ya majukumu yetu ni kupima usahihi wa mizani ili kile ambacho mtu atanunua kiwe kweli kinalingana na fedha yake lakini pia hivi sasa tunapima mita za umeme na maji.

"Tunakagua alichokitumia na kulipa kama ni sawa. Pia kwenye ukaguzi wa Pampu za mafuta tunakagua kiasi cha mafuta hivyo hata mkulima akipeleka trekta kujaza mafuta basi asiibiwe iwe kwenye ujazo sahihi,"amesema.

Hata hivyo amewahamasisha wakulima pamoja na wananchi kutembelea banda la WMA ili kupatiwa elimu mbalimbali inayohusu majukumu yao katika Wakala huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuweka mifumo imara ya kitaasisi na kisheria itakayowapa vijana fursa pana ya kushiriki na kushirikishwa katika michakato yote ya maendeleo hapa nchini.

Amefafanua kuwa Dhana ya Ushiriki wa Vijana katika kujenga uchumi imara, ustawi na maendeleo endelevu inatokana na kuwa vijana ndio nguvu kazi, vijana ni kundi kubwa ukilinganisha makundi mengine ya kijamii, vijana ni wabunifu, vijana ni wavumbuzi na vijana ni wadadisi.

Mhe. Ndalichako ameyasema hayo leo tarehe 12 Agosti, 2022, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”.

“Vijana ni watu wenye mawazo mapya, Vijana ndio chachu ya mabadiliko yenye tija ya Kisayansi na Kiteknolojia na Vijana ndio warithi na waendelezaji wa historia na falsafa ya Mataifa yao.”

Mhe. Ndalichako amesisitiza kuwa kiwango cha ushiriki wa vijana kwenye shughuli za kiuchumi na za kijamii kwa ajili ya ujenzi wa Taifa hapa nchini kipo kwa 80%.

“Matokeo ya utafiti wa nguvu kazi ya Taifa ya Mwaka 2020/21 yanaonesha kuwa, idadi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 inakadiriwa kufikia watu Milioni 18.3. Kati yao, vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa maana ya economically active population ni Milioni 14.6.”

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa kati ya watu Bilioni 8 Duniani kote, Idadi ya Vijana ni Bilioni 1.8.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu imeratibu Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, Vijana Tanzania Bara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walitekeleza masuala mbali mabli kama vile; Kongamano la Kitaifa na shughuli za kujitolea kwenye usafi wa mazingira katika fukwe za bahari na Bonanza la Michezo.

Wazo la kuwa na Siku ya Vijana Kimataifa lilitolewa na vijana kwenye Mkutano wa Vijana wa Dunia (World Youth Forum) uliofanyika Mjini Vienna nchini Australia Mwaka 1991. Kuanzia tarehe 12 Agosti, 2000 nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiangalia sehemu ya bidhaa za wadau wa masuala ya Vijana walioshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”
Baadhi ya Vijana wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Kauli mbiu kwa mwaka huuni; “Kila Mmoja Anahusika katika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara na Ndg. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Agosti 10, 2022
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dodoma kabla ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara kulia ni Ndg. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Agosti 10,2022.

MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Joelson Mpina amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara.

Mpina amechukua na kurejesha fomu hiyo leo Agosti 10, 2022 ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa chama hicho kwa mwaka 2022.

Mbunge huyo wa Kisesa amechukulia fomu hizo katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma na kukabidhiwa fomu hizo na Ndugu. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma.

Mpina amechukua fomu hizo leo Dodoma ikiwa ni siku chache tangu kuhitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Operesheni Venance Mabeyo katika Kambi ya Kikosi cha Jeshi Makutupora Dodoma mafunzo yaliyomalizika Agosti 5, 2022.