Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara na Ndg. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Agosti 10, 2022
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dodoma kabla ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara kulia ni Ndg. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Agosti 10,2022.
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Joelson Mpina amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara.
Mpina amechukua na kurejesha fomu hiyo leo Agosti 10, 2022 ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa chama hicho kwa mwaka 2022.
Mbunge huyo wa Kisesa amechukulia fomu hizo katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma na kukabidhiwa fomu hizo na Ndugu. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma.
Mpina amechukua fomu hizo leo Dodoma ikiwa ni siku chache tangu kuhitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Operesheni Venance Mabeyo katika Kambi ya Kikosi cha Jeshi Makutupora Dodoma mafunzo yaliyomalizika Agosti 5, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments: