Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na
Wafanyabiashara ndogondogo juu ya kuwatafutia maeneo rasmi ya kufanyia
biashara ambayo yatakuwa mazingira rafiki kwa kufanya biashara zao , leo
jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara ndogondogo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara Ndogondogo wakijiandikisha majini yao ili
wapatiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira
rafiki, leo jijini Dar es Salam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo ‘Machinga’ katika soko katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kufuatia Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka Wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ wasibuguziwe na watafutiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema maeneo ya wafanyabiashara hayo tayari yameshatengwa huku yakiwa na mazingira ya kuweza kufanya biashara.
Mjema ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kuzungukia masoko ambayo wanatarajia kuwahamishia wafanyabiashara walio katika Manispaa ya Ilala, Mjema amesema la soko la Kivule na Kerezange kwa sasa yapo tayari huku akiahidi kushughulikiwa kwa changamoto ya miundombinu ya barabara na stendi ya mabasi.
Mjema amesema katika kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ni pamoja kuwa kituo cha Daladala ambapo abiria wanashuka na kupata mahitaji yao katika masoko.
Amesema soko la Tabata Muslim liko katika hatua za mwisho mpaka mwezi wa 12 masoko yote yatakuwa katika mazingira rafiki ya kufanya wafanyabiashara ndogodogo waweze kufanya biashara zao.
Mjema amesema kutokana na kuondoka kwa wafanyabiashara hao kutakuwepo wa eneo moja barabara ambazo wafanyabiashara wataruhusiwa kufanya biashara kando kando ya barabara ambazo ni Ijumaa, Jumamosi pamoja na Jumapili kuanzia majira saa sita mchana kwa wafanyabiashara .
Lumumba na Mkunguni kwa siku ya la Lumumba a machinga kwa ajili ya kufanya biashara kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ambapo barabara hizo ni Lumumba na Mkunguni huku muda wa kuanza kufanya biashara hizo ni kuanzia saa sita mchana na eneo hilo linauwezo wa kukaa zaidi ya wafanyabiashara 1800.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesimamia uadikishwaji wa machinga waliokuwa wafanyabiashara zao kandokando ya barabara za mabasi yaendayo haraka, na kuwataka ambao hawajajiandikisha wajiandikishe mapema ili wapatiwe maeneo rasmi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: