Mkurugenzi wa Raslimali Watu kutoka Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa programu ya 'Code Like A Girl' yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ambayo yanafadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Raslimali Watu kutoka Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis (kulia) akamkabidhi zawadi Mwanafunzi Bless Alexander, mhitimu wa mafunzo ya programu ya 'Code Like A Girl' yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) yanayofadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam

Vodacom Tanzania na dLab Wawezesha Wasichana Kupitia Programu ya CODE LIKE A GIRL7 Marchi 2025, Dar es Salaam - Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab inaendelea kuwawezesha wasichana wenye umri wa miaka 14-18 kwa ujuzi wa STEM kupitia programu ya 'Code Lie A Girl'. Mpango huu umewawezesha zaidi ya wahitimu 3,000 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, na Mwanza.
Hafla ya mahafali iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza na wanafunzi na kuwakabidhi zawadi wahitimu huku akisisitiza dhamira ya Vodacom ya kuwawezesha wasichana kwa ujuzi wa programu (coding) na uvumbuzi. Programu hii pia inahimiza ujumuishi kwa ushirikishaji wa wasichana wenye ulemavu, ikionyesha azma ya Vodacom ya kuziba pengo la kijinsia katika teknolojia ya kidijitali.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: