Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Fedha wa Japan, Mhe. Shin-ichi Yokohama,jijini Tokyo.
Na Mwandishi Wetu.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), yupo Tokyo nchini Japan kwa ziara maalum yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya GPE na serikali ya Japan katika kutatua changamoto za elimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.
Mazungumzo hayo yalijikita katika ushirikiano wa kifedha ili kusaidia miradi ya elimu inayosimamiwa na GPE, ikiwemo upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa nchi zinazoendelea.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Japan, Mhe. Shin-ichi Yokohama, pamoja na Naibu wake, Mhe. Atsushi Mimura, jijini Tokyo
Katika siku yake ya kwanza Tokyo, Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Japan, Mhe. Shin-ichi Yokohama, pamoja na Naibu wake, Mhe. Atsushi Mimura. Mazungumzo hayo yalijikita katika ushirikiano wa kifedha ili kusaidia miradi ya elimu inayosimamiwa na GPE, ikiwemo upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wa nchi zinazoendelea.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Bw. Akihiko Tanaka, Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA) pamoja na maafisa wengine waandamizi kwenye makao makuu ya shirika hili jijini Tokyo. Shirika hili limekuwa na mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo barani Afrika, na mazungumzo yalihusu namna JICA inaweza kusaidia jitihada za GPE katika kukuza elimu bora.
Baada ya mazungumzo hayo, Rais Mstaafu Kikwete alikutana na Bw. Akihiko Tanaka, Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA). Shirika hili limekuwa na mchango mkubwa katika miradi ya maendeleo barani Afrika, na mazungumzo yalihusu namna JICA inaweza kusaidia jitihada za GPE katika kukuza elimu bora.

Katika siku zinazofuata, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. T. Miyaji, pamoja na wabunge wa Bunge la Japan, ambapo ajenda kuu itakuwa nafasi ya elimu na teknolojia katika maendeleo ya jamii. Pia, atashiriki mijadala maalum kuhusu elimu na teknolojia, kufanya mahojiano na vyombo vya habari, pamoja na kukutana na Mhe. Tetsuro Yano, Rais wa Taasisi ya AFRECO, ambayo inahusika na kukuza ushirikiano kati ya Japan na Afrika.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Dkt. Kikwete katika kuboresha mifumo ya elimu duniani, hasa katika nchi zinazoendelea. Japan ni mshirika muhimu wa maendeleo ya elimu barani Afrika, na ushirikiano huu unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wengi zaidi wanapata fursa ya elimu bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments: