Na Oscar Assenga, TANGA

KONGAMANO la Tathimini ya Ujenzi wa Hospitali itakayosimamia maadili ya Kiislamu limefanyika Jijini Tanga huku wadau wa maendeleo nchini wakiombwa kuchangia kufanikisha ujenzi huo ambao utakuwa chachu kwa kutoa huduma kwa maadili ya kiislamu.
Akizungumza wakati wa kongamano hilo Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanga Islamic Development Foundation (TIDF) ujenzi wa Hospitali hiyo Shehe Mohamed Jumaa Mzaruba alisema ujenzi ulianzishwa mwaka 2013 lakini umekuwa ukisuasua kutokana na kutokuwa taarifa za ukweli kuwafikia watu badala ya za ukweli ambazo zingeweza kusaidia kufanikisha ujenzi huo.

Alisema kwamba wanawaomba wadau kutoka maeneo mbalimbali kujitokeza kuchangia ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo itakuwa ni faraja kubwa kwao kutokana itakuwa ikisaidia kuwezesha kutoa huduma kwa maadili ya kiislamu.
Aidha alisema kwamba hilo jambo ni huduma ya kijamii hivyo wanaomba wadau mbalimbali kutoka dini tofauti tofauti kuchangia ujenzi huo ambao umechukua muda mrefu ili liweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

Mwenyekiti huyo alimuomba Rais Dkt Samia Suluhu kuwasaidia katika ujenzi wa Hospitali hiyo itakayojengwa eneo la Tumbirii Kata ya Masiwani Jijini Tanga
Naye kwa upande wae Mlezi wa Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Tanga Farida Mwakichui alisema wanashukuru mkoa kupata neema kubwa waislamu walioanzisha taasisi hiyo kwa ajili ya hospitali ya kiislamu.
“Tunafurahi tunashukuru na tunamuomba awajalie waweze kufikia malengo waliojiwekea lengo kubwa kumstiri mwanamke na mwanaume wamethubutu kufikiria hilo na wanamuomba mwenyezi mungu aliwezeshe maana watakuwa wamenusurika na aibu ya kufedheheka “Alisema
Aidha alisema ujenzi wa hospitali hiyo utakapokamilika utawawezesha kupata stara zao kwa wakimama ambao wanakwenda hospitali kupata huduma mbalimbali za matibabu.
Awali akizungumza mmoja wa viongozi wa Kundi la Sema na Tanga Ahmed Awadhi aliaamrufu Ahmed Mbu alisema jambo hilo ni nzuri kutokana na wakina mama watapata stara kutokana na kwamba wanawake watatibiwa na wanawake na wanaume kwa wanaume na vizuri sana

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: