Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili) kushoto, akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (kulia) akimvalisha beji mshindi wa sita wa mashindano ya Tigo Kili Marathon kwa upande wa wanawake Mary Naali katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gamo (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 mshindi wa tatu Vicoty Chepkemei, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gamo (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 1 mshindi wa pili wa mashindano Tigo Kili Half Marathon, Eunice Echumba, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
Washindi wa kwanza mpaka wa tatu wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Leonidaz Gamo (kushoto), kulia ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage pamoja na na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gamo (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh.500,000 mshindi wa tatu Theophil Joseph, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa Wanaume, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gamo (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 1 mshindi wa pili wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, Emmanuel Giniki (wa pili kushoto) ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Matacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalange.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gamo (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 2, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon Ismail Juma baada ya kushinda katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mkoani Moshi, katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
Washindi wa kwanza mpaka wa tatu wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, kwa upande wa wanaume, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Leonidaz Gamo (kushoto), kulia ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage pamoja na na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili kushoto) akisoma risala katika mashindano ya fainali ya mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa kwanza kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gamo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa RT William Kalage na Mwenyekiti wa KAA Liston Metacha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Tigo Diego Gutierez (kushoto) akizungumza na Kaimu wake Cecile Tiano (katikati) pamoja Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini David Charles kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon yaliyofanyika juzi Mkoani Moshi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: