Haya ndio yanayoniumiza baada ya Kifo cha Jemedali, Mpiganaji, Mzalendo, Mtu wa watu Kepteni John Damiano Chintentema Komba a.k.a Lijogolo, Wamuyaya.
1. Nani ataendeleza mapambano ya kuwapigania wananchi wa Nyasa kwa kiwango ambacho Komba alikifanya.
2. Nani atawasaidia wananchi wa Nyasa wanaoezuliwa nyumba zao kila mwaka kwa mamia kutokana na vimbunga vya Nyasa kama Komba?
3. Nani atalipa ada za wanafunzi wa Sekondari na vyuo waliokua wanalipiwa na Komba kwa mamia?
4. Nani ataendeleza Mapambano ya kuhakikisha Nyasa inafikiwa kwa barabara ya lami na umeme unasambaa haraka kama ambavyo Komba alianzisha?
5. Nani atawapenda wananchi wa Nyasa kiasi cha kuwa nao, kuwatembelea kila mara, kuwasikiliza na kutekeleza matakwa yao?
6. Nani ataendeleza kasi ya kuzipatia kompyuta, Majenereta, Vitabu na vitu vingine shule za Sekondari za Nyasa kama Komba?
7. Nani atawasaidia vijana kwa kuwakopesha Pikipiki, na vifaa vingine vya ujasiriamali mali kama Komba?
8. Nani atakua tayari kufirisika kwa kuwagharamia wananchi wake kuchangia Maji, ujenzi wa shule, Zahanati, na vikundi vya kiuchumi kwa fedha zake za mfukoni kama alivyofanya Komba?
9. Nani atakipenda Chama chake, kukitetea na kukisaidia kamq alivyofanya Komba kule Nyasa?
10. Nani atakua tayari kujenga majengo katika mwambao wa ziwa Nyasa ili mradi kuongeza thamani ya eneo hili ambalo limekua nyuma kwa miaka mingi kama alivyofanya Komba?
11. Nani atakua na upendo na ndugu jamaa na marafiki na kucheka na kila mtu bila kujali hali yake.
12. Na mengine Mengi, Basi Bwana.
KEPTENI KOMBA UMETUTOKA UMETANGULIA MBELE ZA HAKI, HII NI RATIBA YA MWENYEZI MUNGU AMBAYE KAZI YAKE HAINA MAKOSA.
UMEMALIZA KAZI YAKO DUNIA, UNASTAHILI KUVALISHWA TAJI. MCHANGO WAKO KWA TAIFA, KWA WANANCHI WA NYASA NA KWA CHAMA CHAKO CHA CCM HAUJAJIFICHA.
WEWE MBELE SISI NYUMA BABA. LALA SALAMA, UPUMZISHWE KWA AMANI
Lijogolo, Wamuyaya Kepteni John Damiano Chintentema Komba. Wamuyaya!
Toa Maoni Yako:
0 comments: