
Kupitia ujumbe aliouchapisha, Mwijaku amesema jamii ilikosa kuchagua upande mapema wakati tukio husika lilipotokea, akidai kuwa kulikuwa na ukimya hata katika kipindi ambacho kulikuwa na dalili za tatizo, ikiwemo “wakati wa nyuma” kabla mambo hayajafikia hatua ya sasa.
“Kwa nini sasa? Kwa nini sio wakati ule mambo yalipokuwa yanafanyika?” alihoji Mwijaku, akisisitiza kuwa msamaha unaotolewa kwa kuchelewa hauwezi kufuta ukweli wa kile kilichotokea wala kurejesha uaminifu wa jamii kwa haraka.
Aidha, amesema watu wengi wamekuwa wakipandikiza chuki kwa jamii kupitia watu wanaowapenda kwa dhati, hali ambayo imeifanya jamii ishindwe kupaza sauti na kusema ukweli mapema. Kwa mujibu wake, matokeo yake ni jamii kujikuta imegawanyika na kushindwa kufikia msimamo wa pamoja.
Hata hivyo, Mwijaku amesema licha ya yote, jamii inapaswa kubaliana kupitia burudani ya muziki, akieleza kuwa muziki ni nyenzo muhimu ya kuunganisha watu bila kujali tofauti zao. Amehimiza pande zote kuacha lawama na kuangalia mbele kwa maslahi mapana ya jamii.
Akihitimisha ujumbe wake, Mwijaku amesema ni muhimu kwa jamii kujifunza na kuamka juu ya siasa za chuki zinazotokana na watu wachache, akieleza fahari yake kwa Boss Majizo kwa kuthubutu kusema kilicho moyoni mwa watu wengi.
Kauli ya Mwijaku imepokelewa kwa hisia tofauti mitandaoni, huku baadhi wakimuunga mkono na wengine wakimtaka aendelee kuhimiza mazungumzo ya wazi na maridhiano ya kweli ndani ya jamii.
Amesema mkutano huo unatoa fursa ya kutathmini mafanikio ya utekelezaji wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama, pamoja na kubainisha changamoto na mikakati mipya ya kuimarisha utekelezaji wake barani Afrika.Dkt. Gwajima ameeleza kuwa licha ya hatua nzuri zilizopigwa katika kupanua usawa wa kijinsia, wanawake bado wanakabiliwa na vikwazo mbalimbali huku akitaja mila na desturi kandamizi, changamoto za kiuchumi na athari wanazokutana nazo wanawake wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi kuwa miongoni mwa mambo yanayopunguza ushiriki wao katika uongozi na siasa.
Amesisitiza kuwa utekelezaji wenye tija wa ajenda ya WPS unahitaji ushirikiano mpana kati ya serikali, mashirika ya kiraia, wadau wa maendeleo na taasisi za kikanda huu akisema Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika na wadau wengine ili kuhakikisha wanawake wanapata nafasi stahiki katika meza za maamuzi na michakato ya ujenzi wa amani barani Afrika.
Hata hivyo, ameonya kuwa teknolojia hiyo hiyo imekuwa ikichochea aina mpya za ukatili wa kijinsia mtandaoni, ambao waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana.
Amefafanua kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kusambaza video za uongo, chuki, vitisho na matusi yanayolenga kuwachafua wanawake hadharani, jambo linalotishia usalama wao mtandaoni na kuwavunja moyo wanaotaka kushiriki katika uongozi na siasa.
Aidha amehimiza wadau wote kushiriki kikamilifu katika kutoa hamasa na elimu juu ya matumizi salama ya mitandao ili kulinda wanawake, wasichana na jamii kwa ujumla.
Dodoma, Tanzania – 12 Desemba 2025Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea jijini Dodoma.
Kupitia taarifa yake, Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo mzito na kutoa pole kwa Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, wananchi wa Jimbo la Peramiho, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki.
Rais Samia amemuelezea Marehemu Mhagama kama kiongozi shupavu na mtumishi wa umma aliyejitoa kwa moyo wake wote kwa kipindi cha zaidi ya miaka 38 ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Katika safari yake ya kisiasa, Mhagama aliwahi kuwa kiongozi wa vijana, kiongozi wa wanawake, waziri katika awamu mbalimbali za serikali, pamoja na kuwa mshauri wa wanasiasa na wananchi wengi.
“Kwa miaka 38, Mheshimiwa Mhagama amekuwa mwanachama mahiri wa CCM, kiongozi wa vijana, kiongozi wa wanawake, waziri katika awamu mbalimbali na mnasihi wa wengi katika siasa na maisha,” amesema Rais Samia katika salamu zake.
Rais Samia amewaombea wafiwa faraja katika kipindi hiki cha majonzi na kumkabidhi marehemu kwa Mungu, akisema: “Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.”
Mipango ya mazishi inaratibiwa kwa ushirikiano kati ya Serikali, Bunge na familia ya marehemu, na taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa.




















