Articles by "MAMA SAMIA"
Showing posts with label MAMA SAMIA. Show all posts
Kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi akikabidhi Mwenge Maalum wa Uhuru kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya kufikia kilele cha mbio za Mwenge huo Maalum kwa Mwaka 2021 leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipozuru Kaburi hilo leo Oktoba 14,2021. alipokua njiani akielekea katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kuzima Mwenye Maalum wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride rasmi lililoandaliwa na Vijana wa Chipukizi Tanzania, alipowasili katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita leo Oktoba 14,2021 kwa ajili ya kuzima Mwenye Maalum wa Uhuru baada ya kukamilisha mbio zake Tanzania nzima.
Vijana wa Halaiki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu sehemu ya uendeshaji Haki mara baada ya kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo tarehe 28 Machi 2021 .



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akitolea maelezo moja ya Taarifa zake za ukaguzi leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akitolea Maelezo moja ya Taarifa yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mwaka 2019/20
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga mara baada ya kutoka katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na viongozi wengine baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino
jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi
28, 2021.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Bashiru Ally pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bw. Charles Kichere baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Bashiru Ally, Katibu Mkuu Ikulu Dkt Moses Kusiluka na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi) Dkt. Laurean Ndumbaro baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiaga ili kuondoka eneo la tukio baada ya hafla ya kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na TAKUKURU iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumapili Machi 28, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano kipindi cha pili katika hafla iliyofanyika leo tarehe Machi 19, 2021 katika Ikulu ya Magogoni Mkoa wa Dar es Salaam. Ikiwa Hafla iliyofanyika kwa majonzi kwa sababu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mnzena Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akipokea salamu za kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo Machi 19, 2021.

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Machi 19, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Hafla ya Harambee ya kuchangia Mfuko wa Forum for African Woman Educationalis Zanzibar (FAWE) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo March 06, 2021 katika Ukumbu wa Serena Shangani Mjini Zanzinar, yenye “kauli mbiu ya kumuelimisha Mtoto wa Kike ni kuiwezesha Jamii”.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Tuzo kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Zanlink Zanzibar Bibi Yusrat Mkwale kwa kutambua mchango wa Taasisi hiyo wa kuichangia Taasisi ya Forum for African Woman Educationalism Zanzibar (FAWE) ) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo March 06, 2021 katika Ukumbi wa Serena Shangani Mjini Zanzibar, yenye kauli mbiu ya “kumuelimisha Mtoto wa Kike ni kuiwezesha Jamii”
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Forum for African Woman Educationalis Zanzibar (FAWE) Dkt. Mwatima Abdalla Juma kwenye Hafla ya Harambee ya kuchangia Mfuko wa Forum for African Woman Educationalis Zanzibar (FAWE) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo March 06, 2021 katika Ukumbi wa Serena Shangani Mjini Zanzibar, yenye kauli mbiu ya kumuelimisha Mtoto wa Kike ni kuiwezesha Jamii. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Tuzo maalum kwa Mwakilishi wa Taasisi ya DollHouse Boutique Bibi Khaitham Salim Turky kwa kutambua mchango wa Taasisi hiyo wa kuichangia Taasisi ya Forum for African Woman Educationalism Zanzibar (FAWE) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo March 06, 2021 katika Ukumbi wa Serena Shangani Mjini Zanzibar, yenye kauli mbiu ya “kumuelimisha Mtoto wa Kike ni kuiwezesha Jamii”.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi kupitia Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo Agosti 12,2020 Baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Redio hiyo na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Mradi wa Redio Jamii Kati FM na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo Agosti 12,2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Viongozi, watendaji na Wananchi mbalimbali katika Hafla ya Ufunguzi wa Redio Jamii Kati FM na Uzinduzi wa Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo Agosti 12,2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo aliyozawadiwa na Baraza la Vijana Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuzindu Kituo cha Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo Agosti 12,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Mboga aina ya Kisamvu inayotengenezwa na Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini Unguja Wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo Agosti 12,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makanali wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati wakiingia katika sehemu ya Ibada katika Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.





Gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati likiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.



Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akiwa pamoja na familia yake katika Misa hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika Misa hiyo ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa wakishiriki Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa.