SHIRIKISHO la Asasi za Kifedha Tanzania (TAMFI) limesema lina programu maalumu ya kuchangia uhifadhi wa mazingira na kupambana na ukataji miti kwa kuwezesha nishati safi ya kupikia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMFI, Winnie Terry katika kongamano la Wanawake katika fedha:Kukumbatia mabadiliko ya tabia nchi lililofanyika mwishoni mwa wiki.
"Ahadi yetu ya 'Kukumbatia Mabadiliko ya Tabianchi' inazidi mjadala tu; ni wito wa kuchukua hatua. Kwa kulingana na maono ya serikali ya ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, tunalenga kushughulikia vipengele muhimu vya maji, nishati mbadala, na mabadiliko ya tabianchi na kujitolea kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu namba kumi na nne (14)" alisema Winnie.
Mkutano huo uliopata ufadhili kutoka Foundation ya Charles Stewart Mott uliweka wazi ushawishi muhimu wa taasisi za kifedha kuwezesha wanawake ndani ya sekta ya fedha kuongoza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Akisisitiza athari zisizo sawa za mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake, hasa nchini Tanzania na kote duniani, Minzi alitaka ushirikishi katika kufanya maamuzi na kutekeleza mipango kwa vitendo. Alihimiza haja ya kuongeza sauti za wanawake katika fedha kama waendeshaji muhimu wa suluhisho endelevu kwa changamoto hizi za kimataifa.
Naye Ofisa Programu wa TAMFI, Deodati Bernard alielezea mchango mkubwa wa wanawake kwa maendeleo ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: