Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati uzinduzi wa Filamu ya Tanzania'The Royal Tour' ambapo hafla ya Uzinduzi wa Filamu hiyo unafanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo Mei 8, 2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari wamewasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere tayari kwa ajili ya Uzinduzi wa Tanzania The Royal Tour ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Watanzania wa sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii kujitayarisha kupokea watalii watakaokuja kutalii nchini.

Ametoa rai hiyo leo Mei 8, 2022 wakati akizindua filamu ya Royol Tour katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzinduliwa rasmi nchini Marekani, kisha jijini Arusha na baadae Zanzibar.

“Mategemeo yangu baada ya filamu hii kuzinduliwa Tanzania inatakiwa kujitayarisha kupokea wageni wengi, wageni watakuwa wa tofauti tofauti hizo hata watakapokuja watakaa katika hoteli za tofauti.

“Hivyo nitoe rai kwa sekta za utalii kujitayarisha ili watalii wakija wakute hoteli zipo, wakute watu wa kupokea wageni wapo, wapokea wageni viwanja vya ndege nao wajiandea.

“Zile sifa ambazo zimeoneshwa kwenye filamu lazima uonekane, tunapaswa kujitayarisha, watu wa sekta ya utalii na sekta nyingine tujitayarishe, narudia tena lazima Watanzania wote tujitayarishe,amesema Rais Samia.

Aidha amesema kuzinduliwa kwa Filamu ya Royol Tour ni mwanzo tu wa kuzindua filamu nyingine za Royal Tour awamu ya pili na ya tatu kwani kuna picha nyingi ambazo zilichukuliwa ambazo zitatumika kutengeza filamu nyingine kwa lengo la kendelea kutangaza utalii wa Tanzania.

“Filamu hii ya Royal Tour ni mwanzo tu kwani nyingine zitakuja.Nimpongeze Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa ushiriki wake mzuri kwenye filamu hii na amekuwa na msemo wake kuwa yajayo yanafurahisha, hivyo tuseme yajayo yanafurahisha”amesema Rais Samia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: