Naye Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi aliyataja matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto yanayoripotiwa zaidi Polisi kuwa ni ubakaji, mimba za utotoni,ulawiti, kushindwa kuhudumia familia, kutupa watoto na shambulio la aibu.
Mkuu huyo wa Upelelezi alishauri siku ya kusomwa kesi mtu aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia anatakiwa kuwepo mahakamani ili kutoka ushahidi huku akiviomba vyombo vya habari kutangaza matokeo ya kesi za ukatili wa kijinsia na watoto hasa adhabu zinazotolewa kwa wahusika wa matukio ya ukatili ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto , Tedson Ngwale alisisitiza Maafisa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Watendaji wa kata kusimama vema katika nafasi zao ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa Watoto ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya ndoa kabla ya kufungwa ili kubaini umri wa wanandoa na hali za shule na kufanya ufuatiliaji wa Watoto wote wanaohamishwa shule ili kujua kama kweli shule walizohamishiwa wameripoti.
Akitoa mada kuhusu changamoto katika kuendesha kesi za jinsia na watoto mahakamani na ushauri ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto Wakili wa Serikali Mwandamizi Salome Mbuguni kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga aliwataka wazazi na walezi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mary Peter Mrio akizungumza kwenye kikao cha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto aliomba wadau wote kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wao washiriki wa kikao hicho walisema umaskini na utoro wa wanafunzi shuleni umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku wakibainisha kuwa kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia na Waathirika wa matukio ya ukatili kuchelewa kupata huduma inasababisha washindwe kupata huduma kwa wakati.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi na Wadau Wanaopinga Ukatili wa Kijinsia na Watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili mkakati wa mkoa wa Shinyanga katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto leo Jumanne Desemba 15,2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kikao hicho kimeandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa Ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania (WFT). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Toa Maoni Yako:
0 comments: