Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akitoa maagizo kuhusu ukarabatiwa miundombinu ya umwagiliaji Wilayani Bahi.
Mhe. Hussein Bashe Naibu Waziri wa Kilimo, akiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi akipokea taarifa ya utekelezaji wa Maagizo yake aliyoyatoa Mwezi June 2020
Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Dodoma,Raphael Laiza akipokea Maagizo ya Mh. Waziri Bashe, hayupo katika picha, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Kulia, Mkulima wa Bahi Sokoni Sechelela Mbigili akizungumza kuhusu athari za mafuriko katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Bahi sokoni, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
Mhe.Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiangalia sampuli ya ngano iliyofanyiwa majaribio kwenye skimu ya kilimo cha Umwagiaji Bahi Sokoni.
NaibuWaziriwaKilimo Hussein Bashe akikagua sehemu ya Madaraja yaliyojengwa na Kampuniya SGR ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
NA MWANDISHI WETU, BAHI
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema tafiti za kilimo cha ngano katika mikoa ya Dodoma, Mbeya na Arusha zilizofanyika hivi karibuni zimetoa matokeo chanya ambapo aina tatu za mbegu za ngano zilizofanyiwa majaribio zimeonyesha uwezo mkubwa wa kustawi nakutoa mavuno ya kuridhisha katika mikoa hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi wilayani Bahi , Naibu Waziri Bashe amezitaka taasisi za Utafiti wa kilimo (TARI), Taasisi ya Mbegu (ASA), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao nchini (DCD) kushirikiana katika kutekeleza mpango wakilimo hicho ili kupata matokeo chanya.
“Hatua hiyo inakwenda sambamba na sera ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 20 - 25 inayoelekeza taifa kuzalisha zao la ngano kwawingi ili kusitisha uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchini.” Alisisistiza
Naibu Waziri Bashe alimaliza kwa kusema kuwa, kwa kuanzia zoezi hilo litatekelezwa katika Skimu kumi na nne Wilayani Bahi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: