Meneja Miradi wa Foundation for Civil Society Bw Francis Uhadi akiongea na wana azaki katika mafunzo ya siku tatu ya kuzijengea uwezo asasi za kiraia zinazofadhiliwa na shirika hilo mapema jana jijini Dododma.

Wakati Tanzania ikiwa katika mabadiliko makubwa ya kuhakikisha kuwa inakuwa ni nchi ya uchumi wa kati na viwanda wadau mbalimbali wameendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa mijadala, na mafunzo mbalimbali kwa wadau wake kwa lengo la kujengeana uwezo wa kuwafikia wananchi.

Moja kati ya wadau wakubwa wa maendeleo nchini ni Taasisi ya uwezeshaji wa asasi za kiraia ya
Foundation for Civil Society (FCS) ambayo wao wameamua kuendesha mafunzo ya siku tatu kwa asasi zote inazozifadhili lengo likiwa ni kutoa mafunzo juu ya mambo mbalimbali ikiwemo uwezeshaji kwa watu wenye ulemavu, vijana, wanawake, haki za raia na demokrasia pamoja na ushiriki wa wananchi katika michakato ya maamuzi, mipango, bajeti, utekelezaji na ufuatiliaji katika sekta za huduma za umma na watendaji wake.

Mkutano huu wa mafunzo unashirikisha asasi za kiraia (AZAKI) zinazotekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiongea kuhusu mkutano huo wa mafunzo, Meneja Miradi wa Foundation for Civil Society Bw Francis Uhadi, amesema mafunzo haya yatachukua siku tatu yakishirikisha asasi 119 kutoka mikoa 22 ya Tanzania Bara na Zanzibar ambapo amesema kuwa anaamini mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa wadau hao katika kutekeleza shughuli zao za kuijenga jamii yenye maendeleo endelevu.

“Kuna mambo mengi ya kuongea kwenye agenda, yote yanalenga upitiaji wa mipangokazi na bajeti za miradi yote inayofadhiliwa na Foundation kwa sasa. Na hatua hii huwa tunaifikia baada ya kupitia asasi zote kila mwaka ili kutambua mapungufu ya kiufundi na changamoto nyingine katika utekeleaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya asasi hizi” ameongeza Bw Uhadi.

Wadau nchini wamekuwa wakiendelea na mijadala mbalimbali yote ikiwa ni kuiunga mkono serekali ya awamu ya tano ambayo imejikita katika kuleta maendeleo kwa wananchi kwa ujumla ambapo Mashirika binafsi yamekuwa wadau wakubwa katika maendeleo hayo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: