Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa Ndugu George Daniel Yambesi, akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Francis Makoye akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi.Edda Sanga akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Mwenyekiti wa chama cha wabunifu mitindo Ndugu. Merinyo Desumbuka akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fisoo akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Mwakilishi kutoka Basata Ndugu Onesmo Kayanda akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa Ndugu George Daniel Yambesi akibofya kitufe kuashiria uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
Onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa
Onyesho la Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa Ndugu George Daniel Yambesi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa tasuba pamoja na waalikwa.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imezindua mpango wa ufadhili wa masomo ujulikanao kama Sanaa tuition fee waiver scholarship kwa wanafunzi 20 kwa mwaka wa masomo 2018/2019.ambapo kwa upande wa Tanzania ufadhili huo utahusu wasichana 10 ,wanafunzi wengine kumi watatoka nchi wa washiriki wa jumuia ya Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo wilayani Bagamoyo, Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt. Herbert Makoye amesema “Taasisi imekuja na mkakati wa kutoa ufadhili wa ada ya masomo ili kuweza kuziba mapengo makubwa mawili ambayo yamedhihirika katika utoaji wa mafunzo. Kwanza kuna uwiano hasi kati idadi ya wanachuo wa kike na wale wa kiume.

Wanachuo wa kike wanaodahiliwa kila mwaka na Taasisi ni wachache sana (chini ya 30%) ikilinganishwa na wa kiume. Pili, pamoja na kupata hadhi ya kuwa kituo cha ubora uliotukuka kwenye ufundishaji katika nyanja za utamaduni na sanaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Taasisi haijaweza kudahili wanachuo kutoa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”alisema Makoye.

Aliongeza kuwa malengo makuu ya utoaji wa Ufadhili wa ada ya masomo ni Kuwezesha vijana wa kike wa Kitanzania wenye vipaji vya sanaa kupata nafasi ya kunoa vipaji vyao kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa kwenye Taaisisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

Lakini pia ni fursa kwa Taasisi kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania na kuingia katika soko na kuuza bidhaa zake kwa raia wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki

Naye mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TaSUBa ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Ndg. George Daniel Yambesi aliishukuru TaSUBa kwa ufadhili huo Kwa kuwa umeonyesha njia, kwa sababu ni kweli kabisa kuwa kuna vijana wengi wenye vipaji hasa wa kike ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za masomo.

Aidha ndugu Yambesi aliitaka TaSUBa ihakikishe ufadhili huu kweli unakwenda kwa walengwa; yaani vijana wenye vipaji vya sanaa na wana uhitaji wa ufadhili. Kwa kufanya hivi matunda ya ufadhili huu yataweza kweli kuonekana baada ya vijana hawa kuhitimu masomo yao.

Wakati huo huo ,baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza zimejitolea kufadhili malazi na Chakula kwa kipindi chote cha masomo kwa wanafunzi kumi wa kike kutoka Tanzania watakao faidika na ufadhili huo.

Uzinduzi huo ulisindikazwa na onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa na Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: