Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu ya Tigo kuja na vifurushi vipya vya intaneti ; 'Mega Mix'. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza kuanzishwa kwa ofa ya MEGA MIX ambayo itakuwa inatoa vifurushi vya intaneti ambayo vitawazawadia wateja dakika za ziada kwa ajili ya kupiga simu. Ofa hii itawapatia wateja urahisi wa kutumia vifurushi hivi vipya kupitia kifaa chochote kinachotumia intaneti zikiwemo simu za mkononi na modemu.
Akitangaza vifurushi vya Mega Mix kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo Ofisa mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev alivielezea vifurushi hivyo kama “hatua moja mbele ya mabadiliko katika soko inayotoa vifurushi sahihi zaidi: ikiwa ni suluhisho kwa watumiaji wote wa data ndani ya sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania.”
Shavkat aliongeza, “Wateja wetu hivi sasa wana uhuru wa kuchagua kutoka katika simu zao kifurushi chochote wanachokitaka kikiwa na dakika za ziada zitakazo wawezesha kuunganishwa na wapendwa wao wakati tunapoukaribisha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.”Aliendelea kusema,
“Kwa vifurushi vipya wateja wanaweza kuhabarishwa kwa wakati katika mtiririko wa kuunganishwa na wenzi wao na kuwa bega kwa bega na yanayotokea sehemu mbalimbali duniani. Vifurushi hivi vipya vinaendelea kuonesha jinsi Tigo ilivyojikita katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa pamoja na ubunifu kwa wateja wetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: