Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JUMUIYA ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) imesema itajenga shule ya Sekondari ya bweni kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanaokosa nafasi za kujiunga na sekondari za serikali katika jimbo la Busega.

Hayo yalibainishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito, Joseph Ginhu, wakati akitoa taarifa mbalimbali za jumuia hiyo katika mkutano wa BUDECO uliofanyika juzi, Dar es Salaam, ambapo pamoja na ajenda nyingine, kulikuwa na ajenda ya kuchagua viongozi wa kudumu.

Ginhu alisema shule hiyo itasimamiwa na kuendeshwa na jumuia hiyo, kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya elimu jimboni hapo.


Alitoa taarifa kwa wanachama kwamba, jumuia hiyo haipo kwenye mwamvuli wa kisiasa wala kumbeba kiongozi yeyote, haina dini wala ukabila isipokuwa ipo kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Busega.

Wajumbe mbalimbali waliochangia taarifa hiyo, wengi walilenga sekta ya elimu kutiliwa mkazo na jumuia, na kwamba kuwe na taasisi ya elimu, chuo cha ualimu ili kusaidia kumaliza tatizo la uhaba wa ukosefu wa walimu, na kwamba walimu watakaozalishwa na chuo hicho, wataingia katika shule mbalimbali za jimbo hilo.


Walishauri pia,kufunguliwe chuo cha mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana walioshindwa keundelea na elimu ya juu, na hiyo itasaidia kufungua gurudumu la maendeleo ya elimu katika jimbo hilo.


Mmoja wa walezi wa jumuia hiyo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alionya kusiwe na matarajio ya juu, kwani endapo yatashindwa ni rahisi kwa wanakikundi kukata tamaa.

Pamoja na hayo, Ginhu alisema wakati jumuia hiyo inazinduliwa rasmi mwezi Machi mwaka huu, na kufanya harambee waliazimia kuwa sehemu ya fedha itakayopatikana itanunua vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya kusaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa vitabu kwenye shule zilizopo jimboni Busega.


"Wilaya mpya na jimbo la Busega ina shule za sekondari 20, ambapo 18 ni za umma na mbili ni binafsi, na sasa tunafanya tathmini ya kuangalia upungufu wa vitabu na kiasi gani tunaweza kumudu, ambapo ripoti itakamilika mapema wiki ijayo nasi tutaanza kazi,"aliongeza.


Aidha, mara baada ya ajenda kwisha na kufanyika uchaguzi, Mwenyekiti huyo wa mpito alichaguliwa kuwa mwenyekiti rasmi, ambapo nafasi ya makamu mwenyekiti ilichukuliwa na Mashauri Nkonoki, Katibu Mkuu Mickness Mahela, Naibu Katibu Solobi Ngassa na Mwekahazina Julius Manyanda.


Bodi ya udhamini iliundwa na Jaji Mihayo, Jaji Mstaafu Agusta Bubeshi, Emmanuel Kamba,Rafael Ng'wenesho ma Lameck Kipilyango
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: