“Tunatambua uwezo mkubwa ulio ndani ya vijana wa Tanzania; wao ni wabunifu, wajasiriamali, viongozi, na waleta mabadiliko, hivyo wanastahili zana zinazounga mkono ndoto zao," alisema Brigita Stephen, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom. "Kupitia VYB, tunahakikisha kwamba vijana si tu wanaunganishwa bali pia wanapata rasilimali wanazohitaji ili kufanikiwa katika uchumi wa kidijitali, kwa sababu kufanikiwa kwa vijana hawa, ni kufanikiwa kwa taifa zima.
"Kampeni ya VYB imezinduliwa katika kituo cha mafunzo ya ufundi cha Vijana cha Don Bosco, ambacho kinajulikana kwa kujitolea kwake katika uwezeshaji na maendeleo ya vijana nchini. Akizungumza kuhusu umuhimu wa uzinduzi huu.
Maureen Njeri, Meneja Mkazi wa Mdundo aliipongeza Vodacom kwa hatua hii na kusema kwamba Ushirikiano wa Mdundo na Vodacom unathibitisha kauli mbiu ya Vodacom ‘Pamoja Tunaweza,’ “Tangu mwaka 2020, tumekuwa tukifanya kazi pamoja na tutaendelea kufanya kazi pamoja na Vodacom katika kuleta burudani bora kwa vijana. Yajayo yanafurahisha, kaa mkao wa kula,” alisema Maureen.
Alidadavua kwamba VYB inawawezesha wateja wa Mdundo kupata urahisi na uhalali wa kupata Top Dj Mixes katika miziki ya Bongo Flava, Singeli, Qaswida, Taarab, Gospel, Afro beats, Amapiano huku akiongeza kwamba kila siku Mdundo wanatoa Dj mixes mpya ambazo zinaweza kupakuliwa moja kwa moja kwenye simu kwa kutumia kifurushi maalum cha VYB.
“Kama Mdundo, tunahamasika kufanya kazi na na Wasanii Pamoja na watumbuizaji hapa nchini huku tukiwapa fursa ya kupata hela kutokana na bidi zao, Mdundo ina watumiaji hai takribani 31.8 milioni duniani huku hapa nchini wakiwa ni 3.1 milioni kwa mwezi, tunalenga kutoa mirahaba yenye thamani yad ola 3.2 bilioni kwa wasanii wa Afrika kwa mwaka ujao,” alifafanua Maureen.
“Ili kuingia kwenye jukwaa, mteja yeyote wa Vodacom aliyesajiliwa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) na mwenye umri kati ya miaka 15 na 28 ataandikishwa moja kwa moja kwenye programu ili kuhakikisha mpito rahisi ili vijana waweze kufurahia faida za VYB,” alihitimisha Brigita.